soul provider
JF-Expert Member
- Jun 21, 2014
- 1,355
- 2,194
Najitahidi kufanya hivyo kila ninapopata nafasi.Hujachelewa kaka, watolee sadaka zaidi ili wapate sehem yao!
Na hakuna zawadi nzuri kwa waliotangulia zaidi ya kuwatolea sadaka, au kulisha maskini kwa niaba yao
Fikra za hivi ndiyo zinatufanya Wa-Afrika tuwe maskini na kila kizazi kiwe kinaanza maisha na sifuri. familia ni baba, mama na watoto tu. kuwasaidia wazazi au ndugu zako ni kuwadhulumu watoto wako, pia siyo lazima.
Nini kifanyike. mtu anapomleta mtoto Duniani, inatakiwa amlee mpaka afikishe umri wa kujitegemea, wakati huo huo ajipange na maisha yako ya uzeeni, mtoto anapoanza maisha, mzazi anatakiwa kumpa mtoto kianzio cha maisha. Mfano: Fedha, nyumba, mifugo, shamba au Gari. Hivi ndiyo jamii zilizoendelea zinafanya, Mfano wa jamii hizi ni Waarabu, Wahindi na Wazungu.
Watu weusi lazima tubadilike kwenye swala la kuhamisha uchumi kutoka kwa baba kwenda kwa watoto na siyo kutoka kwa mtoto kwenda kwa baba. watoto tunawajibu wa kuwalea wazazi kijamii na siyo kiuchumi. Tukifanya hivi vizazi vijavyo vitaishi vizuri kiuchumi.
AminaUsijar Mungu atakufanyia wepesi
Soma tena posti yako. Unaposema kutenga kiasi Fulani cha kipato chako kwa akili ya wazazi, maana yake kuhamisha sehemu ya uchumi wako kwenda kwa wazazi.Hatuhamishi uchumi, kuna wazazi wanahitani msaada kutoka kwa watoto uchumi wao mbaya zaidi ya watoto. Wenye uwezo hupaswi kukaa miaka na miaka hata kijizawadi tu hamna? Halafu sijasema issue ya ndugu wengine hapo.
Tangu nasoma nilikua na katabia ka kununua zawadi special kwa Bi kubwa kila nilipokuwa naenda likizo home, mpaka leo huwa nafanya hivyo. Swala la pesa ananizidi mbali sana so sina mpango huo though huwa namnunulia muda wa maongezi siku moja moja.
kwenye dunia waogopen wakina Madam
nitakuambia majanga yaliyonikutaHahaha yamekukuta yapi ututoleee onyo hilo ndugu
Tumeishia kuchangia masherehe na kuweka heshima bar na mavazi tulio wengi. Tunaishi kama teenagers wa form two, show off wakati mama hana khanga na baba suruali ina kiraka cha kushonwa na mkono.
Asante kwa kutukumbusha mkuu.
Wanamuambia kusaidia wazazi nikuongeza umasikini ila kunywesha watu mademu laki 2 sio issue niuzungu[/
Tunajisahau sana mjini huku. Hahaha bado kuna watu wanahonga? We are doomed