Mada maalum:Je umetenga asilimia ngapi ya kipato chako kwa ajili ya wazazi wako?

Nimeeleza pia kuhusu wenye uwezo kushinda wewe waweza kuwaandalia zawadi kwa wakati fulani kumjali mzazi sio lazima pesa tasilimu
Mathlani Mimi nampa mtoto 200K kila mwezi ili aongeze kwenye kipato chake cha mwezi kutokana na kwamba pensheni yangu ya mwezi ni maradufu ya mshahara wake wa mwezi sasa akiniletea zawadi si nitaona ni ile pesa yangu anarudisha?
 
Duuuuu mimi bi mkubwa angu ni faita hakai kindez

Ila nishapaua nyumba naanza finishing soon kwa ajili yake

Hela huwa nampa yeye ndiye anasimamia

Nataka tuhame nyumba ya zaman japo iko poa tu

Huwa najitahd ispite miez mitatu bila kumtumia lak nne

She is every thing to me

Bado nitafanya mengi kwake, Mungu anajua
 
Hongera
 
Mkuu unacho sema ni kweli ila kumbuka kuwa sio wote tulio toka familia zenye uwezo wa kumwandalia mtoto mazingira ila tumetoka familia ambayo imepambana ili Mimi ni fanikikiwe na wakati huo wanapo ni hangaikia Mimi na familia inazidi kudidimia hapo ninacho kipata lazima nijaribu kukirudisha kama faraja yangu kwa wazazi wangu
 
Hilo lipo haimaanishi kwakuwa wananiweza usiwape hata zawadi mara moja moja
 
Asilimia kubwa ya watumishi wa zamani wamejenga nyumbani kwa kutumia hela za pensions hii ni kwa sababu walikuwa na mzigo mkubwa wazazi wao na ndugu waliwategemea mapato yao wakaelekeza kusaidia wazazi na ndugu mshahara ukawa ni hands to mouth. muda huo unakuta mzazi au ndugu ana nguvu za kufanya kazi ila kwa kuwa kijana ni mtumishi hataki kazi. Ndugu zangu mzazi anajukumu la kukuandalia maisha kumsaidia ni where necessary si kutenga asilimia kila mwezi kwa ajili yake wadada wengi ndoa zao zimevunjika kwa sababu ya kuelekeza mapato yao kwa wazazi wao badala ya kufanya maendeleo ktk familia yake
conclusion.
mzazi asaidiwe where necessary. pesa zako tumia katika kuandalia watoto wako maisha yao.
 
Mkuu kuna wakati hawa walio jenga nyumba zao kwa peshen kumbuka wewe kama ndugu au au mtoto ndo chanzo cha yeye kujenga nyumba uzeeni na hapo ndo huyo mzazi au mlezi huhitaji faraja kutoka kwako ikiwa nguvu zake alizeelekeza kukuwezesha wewe
 
Mibado nalelewa natumiwa kila mwezi make bado natafuta maisha kwahiyi wazazi wananijali ninachopata bado nikidogo kwahiyo wananiongezea ingawa naona ujasiliamali wangu unayumva kurokana napesa kupotea
 
Kila mshahara wangu wa mwezi nawapelekea pesa wazazi lakini sikufikiria kutoa kwa asilimia. Hii ni sawa kabisa JF members 5-10% ni sahihi iende kwa wazazi kila mwezi au kila unachopata(wasio na ajira rasmi). Asante kwa kutukumbusha jukumu letu
 
Muhimu sana kumpatia pesa wazazi mie natoaga tu sina kiwango maalum
 
Kila mshahara wangu wa mwezi nawapelekea pesa wazazi lakini sikufikiria kutoa kwa asilimia. Hii ni sawa kabisa JF members 5-10% ni sahihi iende kwa wazazi kila mwezi au kila unachopata(wasio na ajira rasmi). Asante kwa kutukumbusha jukumu letu

Karibu tukumbushane
 

Kuelekeza pato kubwa kwa wazazi na una ndoa ni uchizi sasa kutokujielewa. Na hao wanaowaza vipato vya wake zao hivyo hadi kutoa talaka mmmhhh
 
Uzi bora kwangu kutoka January mpaka March.
 
Madam Mwajuma umeongea point hadi basi!
Ni ukweli huwa tunajisahau, mimi mwenyewe naomba kujisema, kuna wakati huwa hadi najisikia aibu!
Huwa najitahidi kutumia wazazi angalau laki kila mwisho wa mwezi, ila kiukweli kuna saa naona haya maana kwangu mwenyewe hata laki4 kwa mwezi haitoshi (kwa maana kuwa siwi comfortable), laki inasaidia lakini nao pia hawawi comfortable, bado wataendeleza vijimizinga vya hapa na pale kufanya siku ziende!
Ahsante mwajuma once again kutukumbusha, labda wale wenzangu na mimi kuna vitu tutavifanyia marekebisho kidogo!
 
[emoji121]
NGOJA NISABUSKRAIBU HUU UZI!

MAANA HAKUNA NAMNA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…