"Mume wangu alipokuwa anaumwa nilikuwa napitia wakati mgumu sana kwasababu nilikosa mtetezi, aliyetakiwa kunitetea ndo huyo alikuwa amelala. Hali ya kuona mume wangu haongei, hawezi kufanya chochote nayo ilikuwa ni changamoto kubwa sana ambayo ilikuwa inanifanya kuna muda nilikuwa nakata tamaa na kujiuliza huyu atarudi kweli? lakini nashukuru Mungu amerudi"
"Ugonjwa wake ulikuwa na taarifa nyingi sana lakini taarifa mbaya zaidi zilikuwa ni zile za kumzushia amekufa wengine walisema ana ukimwi, hizo kwakweli zimeniumiza hata mimi kwasababu kwenye maisha ya kawaida watu wakisikia hivyo lazima waninyoshee kidole hata mimi lakini ndo maisha yako hivyo. Watu walikuwa wanatoa taarifa za uongo kwasababu walikuwa wanataka hela kwa Mange"
"Kwahiyo mtu anaweza akakurupuka tu akachukua kitu chochote akapeleka taarifa ya uongo au inaweza kuwa na ukweli kidogo na nyingine isiwe na ukweli kabisa, hiyo ilitupa ugumu mpaka ikapelekea tukawa tunazuia watu kuingia hospitali"
"Mimi kuvumilia huu mtihani ulionikuta naweza nikasema siyo mimi ni Mungu, lakini pia watu ambao wamenizunguka wakiwemo ndugu wa mume wangu, mama yangu mzazi, baadhi ya marafiki zangu ambao walikuwa wakinipa moyo. Kuna wakati nilikuwa nashindwa lakini wao walikuwa wananiambia no! usikate tamaa. Lakini kingine ni kwamba mimi sikubahatisha kuishi na Professor Jay, niliamua kuishi na madhaifu yake na yeye aliamua kuishi na udhaifu wangu"
"Naweza kuwashauri watu ambao wanataka kuingia kwenye ndoa wajue kwamba ndoa sio rahisi, ni kama kazi, ni kama ajira kwasababu ina vitu vingi sana, inahitaji uwe na akili nyingi sana jinsi ya kuishi na mwenzio. Yeye akujue na wewe umjue vizuri kwamba hapa amekosea, hapa nimekosea tunalitatua vipi hili tatizo, kwahiyo inatakiwa mtu awe na utayari wa kwa kwamba sasa naenda kuishi na mwenza wangu"- Mke wa Professor Jay.
Sent using
Jamii Forums mobile app