Mada maalum kwa wanandoa

Mada maalum kwa wanandoa

1Kuna mambo matatu yanipendezayo,
Ni mazuri mbele za Mungu na wanadamu;
Umoja wa ndugu,
Urafiki wa majirani,
Na mke na mumewe wanaopatana.
 
25
RSUVDC
YOSHUA MWANA WA SIRA 25
Wastahilio sifa
1Kuna mambo matatu yanipendezayo,
Ni mazuri mbele za Mungu na wanadamu;
Umoja wa ndugu,
Urafiki wa majirani,
Na mke na mumewe wanaopatana.
2Kuna watu wa namna tatu wanichukizao,
Na mwenendo wao unanikirihi;
Maskini mwenye kiburi,
Tajiri aliye mwongo,
Na mzee mzinifu asiye na ufahamu.
Wazee
3Katika ujana wako hukukusanya
Utapata wapi upatapo kuwa mzee?
4Ee ajabu ya uzuri wa uteuzi kwao wenye mvi, na kwa wakuu wajuao shauri! 5Ni nzuri kama nini hekima ya wazee, na mawazo yenye shauri ya wale walioheshimiwa! 6Ustadi wa kuzoea ni taji la wazee, na utukufu wao ni kumcha BWANA.
Mithali ya hesabu
7Kuna mambo tisa niliyoyafikiri,
Na moyoni mwangu nimeyaita heri;
Mtu mwenye kuwafurahia watoto wake,
Aliye hai akaona adui zake wamepotea,
8Heri yule mume mwenye mke wa ufahamu.
Naye yule asiyeteleza kwa ulimi wake.
Naye asiyemtumikia mtu asiyestahili,
9Naye yu heri aliyejipatia rafiki amini,
Naye asemaye masikioni mwa wasikivu,
10Naye aipataye hekima ni mkuu kama nini!
Lakini hakuna ampitaye mcha BWANA.
11Hakika kicho cha BWANA hupita mambo yote;
12Aliye nacho aweza kulinganishwa na nani?
Baadhi ya uovu uliokithiri
13Msiba wowote ila msiba wa moyo;
Uovu wowote ila uovu wa mwanamke;
14Baa lolote ila litokalo kwao wanichukiao;
Kisasi chochote ila kisasi cha adui;
15Hakuna sumu ipitayo sumu ya nyoka;
Hakuna hasira kuliko hasira ya mtesi.
Uovu wa mwanamke mbaya
16Ningependa kukaa na simba na joka kuliko kukaa nyumbani pamoja na mwanamke mbaya, 17Ubaya wa mwanamke huubadili uso wake kuwa wa kutisha, na kumtia sura yake giza kama ya dubu. 18Mumewe akikaa chakulani pamoja na jirani zake, bila kusudi aweza kupiga kite kwa majonzi. 19Ukorofi wote si kitu kama ukorofi wa mwanamke; mwenye dhambi na ampate kuwa sehemu yake! 20Kama kuipanda njia ya mchangani kwa miguu ya mzee, ndivyo alivyo mke mwenye maneno mengi kwa mtu mtulivu. 21Usinaswe na uzuri wa mwanamke, wala usimtamani mwanamke kwa ajili ya mali yake. 22Kuna utumwa mzito, na fedheha, iwapo mwanamke humlisha mumewe. 23Mwanamke mbaya ni unyong'onyevu wa roho, na huzuni ya uso, na kujeruhi moyoni. Mwanamke asiyetaka kumfurahisha mumewe amefanana na mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza. 24Mwanzo wa dhambi ulitoka katika mwanamke, na kwa sababu yake sisi sote tunakufa. 25Usiyapatie maji mahali pa kutoka, wala usimpe mwanamke mbaya nafasi ya kusema kwa ujasiri. 26Tena iwapo haendi kama wewe utakavyo, mpe hati ya talaka.
 
 
Kutana na kabila la Dani huko Papua Guinea, Indonesia[emoji1169]

Katika ndoa, mwanamume lazima akate kidole cha mkono wake wa kulia na kumpa bibi arusi kama mahari yake.

.na akitaka kumpa talaka hukatwa vidole viwili vya mkono wake wa kushoto, lakini akifa mkewe hukatwa vidole kumi vya mikono yake ikiwa ni ishara ya uaminifu kwake na kwamba hataolewa na mwanamume baada ya yeye.

Ukioa, ukiachana au ufe... kuna vidole vinapaswa kukatwa.

#Moyowangu
FB_IMG_1654954508006.jpg
 
Kiwanja Cha mke nyumba ya mume, mke kaomba talaka mahakamani na mahakama ikaamuru mke abaki na kiwanja chake na mume ahamishe nyumba yake,mke kwa uzuzu akashangilia.Mume akaja na huo mtambo kuhamisha nyumba yake,mke abaki na kiwanja chake.

#glorysiahrimoy
 
Huu uzi haukupita machoni mwanagu nijifunze maana mambo ya ndoa ni ya kurudi darasani kila siku.
 
Mdogo wangu Hujambo..!?

Nimesikia leo umeamka Vema kabisa Mdogo wangu..!

KUNA SAFARI NA GAZETI..! Leo wacha nikuambie Kuhusu GAZETI najua unajua kwamba Bibi zetu kule wanaita GARAZETI lakini yoote maana yake moja tu isikuchanganye

Kuna kijana anaitwa joseph kayombo]] alinigusia Ununuzi wa MAGAZETI kwa siri sana Mdogo wangu KONDEBOY] nakusema kwamba niliwai kutamka kwenye Waraka wa NABIIMSWAHILI ibara ya 10 Kwamba

" UKIOA MWANAMKE ALIEKUZIDI UMRI NI SAWA SAWA NA KUNUNUA GAZETI JIONI"

sasa zipo Waraka nyingi za @nabiimswahili zinaweza kunukuliwa tofauti

Mimi nikutie nguvu na moyo [emoji3590] katika safari yako ya mapenzi na umedhihirisha kwenye Umma kwamba upo na huyo nikwambie hapa kuwa nae tu huyo ndio umemchagua ni wako Kula unachopenda usile UNACHOKUTA

Kila la Kheri mdogo wangu achana na hao watani wetu joseph kayombo]]

...!

KONDEBOY] joseph kayombo]] @nabiimswahili
FB_IMG_1656337644993.jpg
 
Heart breaking [emoji174]

"I married my wife 25 years ago. She came with two boys from her previous marriage.
I really loved them and adopted the kids since I I'm not medically fit to have a child of my own.

We stayed peacefully in rented houses. I was working back then and made sure to take my adopted kids to the best schools, their father never came to claim them or even support them.
The boys were very bright in school and as I write this, one is a doctor who got scholarship to finish his studies in USA.
He is back and already employed, the second boy is a pilot whom I used all my savings to pay for his course in South Africa, he is also back and employed too.

My happiness is that my boys are successful and have bought big houses, my problem is that my wife and the two boys have reunited with their dad and now living happily together as a family.

They seem to have abandoned me here, i can't even pay my rent anymore, I retired long ago, i have been moving from one relative to another for a place to sleep, they don't even pick my phone calls anymore. Please what do I do now? my life is so miserable" - Man narrates."
Happyhomebreed
Screenshot_20220627-165847.jpg
 
Update: Pichani wanandoa hao ambao mume amepitwa miaka 37 na mke wake huyo wametangaza kutaka kupata mtoto ambapo watatumia shilingi milioni 333.7 na tayari wamempata mwanamke wa kumuajiri awabebee mimba

Mke huyo anaitwa Cheryl ana miaka si chini ya 61 wakati mume wake huyo anaitwa Quran McCain(24) ambapo kwasasa wanaishi Rome, Italia baada ya kufunga ndoa mwaka 2021

Cheryl tayari alishazaa watoto 7 na ana wajukuu 17 katika mahusiano yake ya mwanzo, lakini Quran yeye bado hana mtoto kwahiyo wameamua ili kulinogesha zaidi penzi na ndoa yao basi wapate mtoto ambapo mbegu tayari wameshapata mwanamke wa kumuajiri awabebee hiyo mimba na watatumia jumla ya gharama £120,000 ambazo si chini ya milioni 333.7 za Kitanzania

Wamesema wanapendana sana kila mmoja anamfurahia mwenzie ambapo penzi lao lilianza kipindi cha nyuma baada ya mwanamama huyo kuachia video mtandaoni akicheza muziki kisha watu kuanza kumchamba na kukosa furaha ambapo Quran alianza kumfariji na baadaye penzi kuchanua na hatimaye kufunga ndoa
FB_IMG_1657171028780.jpg
 
Back
Top Bottom