Mada maalum kwa wanandoa

Mada maalum kwa wanandoa

............Mwaka wa saba huu naishi ndani ya ndoa with two kids,namshukuru Mungu sana tena sana sijawahi kupata jaribu kubwa japo changamoto za hapa na pale zipo,naposema jaribu namaanisha majaribu kama ambayo huwa nayasoma humu wakati mwengine hujikuta nalengwa lengwa machozi kwa vitu ambavyo hata havinihusu.

Huyu mke wangu nilianza naye kipindi hiko watoto,nikiwa aged 18 akiwa 15 yupo form 3 tukakaa kwenye uchumba au sijui niite mapenzi kwa miaka nane tukafunga ndoa.nilichojifunza kwenye haya mambo ni uchumba wa muda mrefu husaidia sana ku-stabilize maisha ya ndoa,niulize kwa nini?

Unapata wasaa wa kumjenga kiakili jinsi wewe unavyotaka muishi,hawezi act kwamba amekuelewa coz hata aki act kuna vitu utakuwa unaona anavifanya ambavyo havipo kwenye uhalisia uliomueleza na utamkanya mapema naye atakuwa na muda wa kubadilika tofauti na uchumba wa mwaka mmoja ambapo ata-act anaweza ila ukimuingiza Kanisani au Msikitini ndani ya miezi miwili ya ndoa anaanza kubadilika na ukisema umkanye ndo anazidi kuzingua,ndo vurugu tunazoziona humu mitaani.

Pia ikiwezekana umpate anayetokana na asili yako,vijana wengi siku hizi wanaowana na wapenzi wao waliokutana mavyuoni kila mtu ana tabia zake,hii itakufanya umsome zaidi adui yako kwa sababu unakuwa upo na mtu mnaejuana madhaifu yenu na jinsi ya kuvumiliana na kurekebishana.

Ushauri kwa mnaotafuta wake tafuteni mmoja permanently muwaandae mapema haya mambo ya kutafuta mke haraka haraka ukiwa na miaka 29/30 utakuja kuokota visivyookoteka chagua mmoja awe ndiye target yako.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk

So unamaanisha watarget mmoja kama vile simba akiwa anawinda swala mmoja kwenye kundi la swala?[emoji16][emoji16][emoji16]


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hakuna kitu kibaya kama watoto kuona baba na mama wanishi kwa ugomvi
Wakati mwingine inawasaidia watoto kukua wakijifunza tabia mbaya na nzuri kwa wazazi. Mf mm baba yangu alikuwa mkorofi sana kwa mama na hata watoto, sikuhiz na uzee wake hataki hata kusikia mkimkumbusha ubabe wake na hapendi kukumbuka. Ila sisi watoto wake tumejifunza sana kwa yale maisha ndo maana hata wake zetu watuwapigi ingawa wanatuogopa kwa kusikiliza historia ya mzee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom