Mada Maalum ya Madereva: Changamoto, Uzoefu, Vituko na Connections

Watu watatu wamefariki dunia huku saba wakijeruhiwa baada ya Basi la Zuberi linalofanya safari za Mwanza - Kahama kugonga kingo za daraja na kupinduka katika eneo la Mwigumbi Mkoani Shinyanga.



Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo Jumatano Juni 15, 2022 majira ya saa nane mchana katika barabara ya Mwanza Shinyanga ambapo basi hilo lenye namba za usajili T435 DJS SCANIA liligonga ukingo wa daraja la Mwigumbi na kutumbukia bondeni.


Kamanda Kyando ametaja mmoja wa waliofariki dunia kuwa ni dereva wa basi hilo aliyefahamika kwa jina la Hamza Haule.


Amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva alipata tatizo la kiafya akiwa safarini.


Your browser is not able to display this video.
 
Weka maelezo kidogo kama unayo
Watu watatu wamefariki dunia huku saba wakijeruhiwa baada ya Basi la Zuberi linalofanya safari za Mwanza - Kahama kugonga kingo za daraja na kupinduka katika eneo la Mwigumbi Mkoani Shinyanga
 
Huyu alikuwa kaiva haswaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…