Mada Maalum ya Madereva: Changamoto, Uzoefu, Vituko na Connections

Mada Maalum ya Madereva: Changamoto, Uzoefu, Vituko na Connections

IMG-20220605-WA0368.jpg
 
Watu watatu wamefariki dunia huku saba wakijeruhiwa baada ya Basi la Zuberi linalofanya safari za Mwanza - Kahama kugonga kingo za daraja na kupinduka katika eneo la Mwigumbi Mkoani Shinyanga.



Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo Jumatano Juni 15, 2022 majira ya saa nane mchana katika barabara ya Mwanza Shinyanga ambapo basi hilo lenye namba za usajili T435 DJS SCANIA liligonga ukingo wa daraja la Mwigumbi na kutumbukia bondeni.


Kamanda Kyando ametaja mmoja wa waliofariki dunia kuwa ni dereva wa basi hilo aliyefahamika kwa jina la Hamza Haule.


Amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva alipata tatizo la kiafya akiwa safarini.


 
Weka maelezo kidogo kama unayo
Watu watatu wamefariki dunia huku saba wakijeruhiwa baada ya Basi la Zuberi linalofanya safari za Mwanza - Kahama kugonga kingo za daraja na kupinduka katika eneo la Mwigumbi Mkoani Shinyanga
 
Basi la Kampuni ya Mohammed Clasic lililokuwa likitoka Mkoani Arusha kuelekea Kigoma limegongana uso kwa uso na fuso katika kijiji cha Ming'enyi Wilaya ya Hanang' Mkoa wa Manyara na kusababisha vifo vya Watu watatu na majeruhi 26.

RPC Manyara, Benjamin Kuzaga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema fuso lilikuwa limetoka mkoani Tabora kuelekea Kilimanjaro likiwa limebeba mchele "Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi kutokuzingatia alama za barabarani"

"Waliofariki ni Msaidizi wa dereva wa fuso, Msaidizi wa dereva wa basi pamoja na utingo wake, dereva wa basi ametoroka kusikojulikana tunaendelea kumtafuta kwa kusababisha ajali na kugharimu maisha ya Watu na majeruhi na hatua kali zitachukuliwa"

"Majeruhi ni Wanaume 14, Wanawake 10 na Watoto wawili ambao wote wapo katika Hospitali ya Tumaini Kateshi"

#ajali_sasa_basiView attachment 2237783
Huyu alikuwa kaiva haswaaa
 
Back
Top Bottom