Mada Maalum ya Madereva: Changamoto, Uzoefu, Vituko na Connections

Mada Maalum ya Madereva: Changamoto, Uzoefu, Vituko na Connections

Nakumbuka siku nilipata ajali ambayo hata sielewi ilikuwaaje ghafla tu najikuta nipo kwenye mashamba ya mpunga tena kwenye mkondo wa maji,ile nashtuka nasikia watu wakisema kaua kaua kwa wenge nililopata nikatokea kwenye dirisha nikajitosa kwenye maji dahh!! hii siku siwezi isahau
Vp ni kweli uliuwa na wapita njia wanasema ilikuwaje?
 
Ukiona unataka kuingia barabara nyingine na kuna gari hata liwe mbali kidogo halijawasha taa kukuruhusu uingie, tafadhali usiingie maana huwezi jua halijawasha taa kwasababu breki zimefeli au ni mbovu hivyo jamaa kaona hata akiwasha taa atakuvamia tu maana gari yake haisimami, Juzi nmeipata hii mi sikuingia ila kibajaji flani kiliingia na kuzua taharuki.
 
Hapa uje ulete mrejesho
Mrejesho

Ningumu kupata hiyo deal ya IT kama hauna Agent au mtu yoyote unaemjua anaetoa magari bandari. Nimejaribu kwa muda wa siku 5 mchana na usiku, maana pale magari yanatoka 24/7 hakuna sikukukuu lakini ni patupu. Kuna madereva zaidi ya 200 unakuta wamekaa tu wanangojea chance itokee wapate kibarua hicho. Kweli hali ya madereva ni ngumu ngumu ngumu. Bila connection hupati kitu.
 
Madereva wa mabasi wanamakusudi.
anakupigia honi kwa karaha anaomba njia umpe gepu mahala pasipo wezekana.alafu unakuta yupo mafuta na keshafika nyuma yako,ukimcheki kwenye side mira unamaona kama kagusa kabisa buti ya gari yako.
Madereva wa mabasi mkiwa barabarani mpunguze haraka.
 
Madereva wa mabasi wanamakusudi.
anakupigia honi kwa karaha anaomba njia umpe gepu mahala pasipo wezekana.alafu unakuta yupo mafuta na keshafika nyuma yako,ukimcheki kwenye side mira unamaonakama kagusa kabisa buti ya gari yako.
Madereva wa mabasi makiwa barabarani mpunguze haraka.
Sauli
 
Back
Top Bottom