Mada Maalum ya Madereva: Changamoto, Uzoefu, Vituko na Connections

Mada Maalum ya Madereva: Changamoto, Uzoefu, Vituko na Connections

Nilichogundua ni kwamba mamlaka hazijawa serious na usalamma wa abiroa na mali zao na kuna madai baadhi ya ma RPC kuwa kwenye payroll ya baadhi ya wamiliki wa nabus
True.
kipindi flani natoka Mwanza nakuja DSM na Princess Muro kabla aijakataa roho,dereva wa basi yupo mafuta trafik wa tochi wanampetete mikono atembee.
Ilibidi tulipofika mdaula kwenye kituo cha mafuta tuskilizie kwanza muda usogee,maana tungefika Ubungo saa nne,wangempiga faini pale Ubungo.
 
Kwahiyo ni wazi kabisa mamlaka zenye dhamana ni sehemu ya tatizo

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
 
Madereva wa mabasi wanamakusudi.
anakupigia honi kwa karaha anaomba njia umpe gepu mahala pasipo wezekana.alafu unakuta yupo mafuta na keshafika nyuma yako,ukimcheki kwenye side mira unamaonakama kagusa kabisa buti ya gari yako.
Madereva wa mabasi makiwa barabarani mpunguze haraka.
Daaah mie yalinikuta mabasi ya kaskazini , Asant Arab sio kwa honi zile alizo nipigia mpka nikapanic nimemwachia site apite ile narudi site yangu Kiazi Kitamu huyu hapa honi za laaan mpaka anagusa spare tire yalivyo nipita nilipark pembeni kwanza kunywa maji maana sio kwa kunijambisha hukooo[emoji4] abiria wa yale mabasi wanamoyo
 
Awajamaa wanafanya kusudi,kila muda wanaharaka,awataki waone mbeleyao kuna gari tofauti na basi.
 
Daaah mie yalinikuta mabasi ya kaskazini , Asant Arab sio kwa honi zile alizo nipigia mpka nikapanic nimemwachia site apite ile narudi site yangu Kiazi Kitamu huyu hapa honi za laaan mpaka anagusa spare tire yalivyo nipita nilipark pembeni kwanza kunywa maji maana sio kwa kunijambisha hukooo[emoji4] abiria wa yale mabasi wanamoyo
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]sorry imebidi nicheke

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
 
Binafsi nalia na hawa trafiki wanaotuandikia hata makosa ya onyo, kwakweli ipo siku watalipwa wanachostahili. Hizo elfu30 wanaona ni rahisi sana kuzipata. Nyie endeleeni tu na huo uonevu.

Sasa wadau hii ifuatayo ni CV yangu kwa ufupi, mwenye "connection" tafadhari usisite kunikonekti na mimi.

Leseni: class A A2 B C1 C2 C3 D
jinsia: mwanaume, 32.
Uzoefu: zaidi ya miaka 4 barabarani, masafa marefu na mafupi. Naendesha 'manual' na 'automatic'
Elimu: kidato cha sita, Kozi ya udereva NIT (advanced driving grade two-vip). Pamoja na kozi ya udereva wa awali.
Mawasiliano:0626 876 896
#Naishi Dar es salaam, nipo tayari kufanya kazi mkoa wowote ndani ya Tanzania.

[emoji1542]Tuinuane ndugu zangu.
 
Daaah mie yalinikuta mabasi ya kaskazini , Asant Arab sio kwa honi zile alizo nipigia mpka nikapanic nimemwachia site apite ile narudi site yangu Kiazi Kitamu huyu hapa honi za laaan mpaka anagusa spare tire yalivyo nipita nilipark pembeni kwanza kunywa maji maana sio kwa kunijambisha hukooo[emoji4] abiria wa yale mabasi wanamoyo
Hili kiazi kitamu ni balaaa Sana gari linakimbia kama halijabeba watu
 
Binafsi nalia na hawa trafiki wanaotuandikia hata makosa ya onyo, kwakweli ipo siku watalipwa wanachostahili. Hizo elfu30 wanaona ni rahisi sana kuzipata. Nyie endeleeni tu na huo uonevu.

Sasa wadau hii ifuatayo ni CV yangu kwa ufupi, mwenye "connection" tafadhari usisite kunikonekti na mimi.

Leseni: class A A2 B C1 C2 C3 D
jinsia: mwanaume, 32.
Uzoefu: zaidi ya miaka 4 barabarani, masafa marefu na mafupi. Naendesha 'manual' na 'automatic'
Elimu: kidato cha sita, Kozi ya udereva NIT (advanced driving grade two-vip). Pamoja na kozi ya udereva wa awali.
Mawasiliano:0626 876 896
#Naishi Dar es salaam, nipo tayari kufanya kazi mkoa wowote ndani ya Tanzania.

[emoji1542]Tuinuane ndugu zangu.
Nitakucheki

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
 
Kuendesha gari ni suala linalohitaji umakini na utulivu mkubwa, hasa pale unapoendesha gari umbali mrefu. Mara kwa mara kumeshuhudiwa ajali mbalimbali ambazo kimsingi zinatokana na madereva kutokuzingatia kanuni muhimu katika utumiaji wa vyombo vya usafiri.

Ili kuhakikisha usalama wako pamoja na watumiaji wengine wa barabara, yapo mambo kadhaa unayopaswa kuyazingatia kabla na wakati wa kuendesha gari umbali mrefu.

1. Kagua na andaa gari
Kabla ya safari yoyote gari linahitaji kukaguliwa na kuandaliwa, hasa kabla ya safari ndefu. Kuna mambo kadhaa unayohitaji kuyakagua kwenye gari lako:

Kagua hali na ubora wa magurudumu. Hakikisha magurudumu yamejaa vizuri na hayajazeeka. Kagua mafuta lainishi (oil). Hakikisha gari yako ina mafuta lainishi ya kutosha tena ya ubora unaotakiwa.

Kagua kiasi cha maji. Maji? Ndiyo maji ni muhimu sana kwenye gari kwa ajili ya kupooza injini ya gari pamoja na kusafishia vioo.Kagua utendajikazi wa injini. Hakikisha injini yako inafanya kazi vizuri.

Kagua sehemu nyingine za gari kama vile breki, kiongeza mwendo (accelerator), usukani, taa, honi, viashiria (indicators), n.k. Usibebe mizigo isiyokuwa ya lazima kwenye gari. Hii itakupotezea mafuta na nafasi bila sababu.

Hakikisha unalikagua gari lako vyema na kuliandaa kwa ajili ya safari. Unaweza pia kumtumia mtaalamu wa magari ili akusaidie kulikagua na kuliandaa kwa safari yako.

2. Pumzika
Ili uweze kuendesha gari vyema wakati wa safari ndefu ni muhimu kupumzika kwa kiasi cha kutosha kabla na wakati wa safari.

Hakikisha kabla ya safari unapata muda wa kutosha wa kulala ili kuepusha kusinzia barabarani kunakoweza kusababisha ajali.

Unapokuwa barabarani unaweza pia kupumzika baada ya umbali fulani ili usichoke sana.
Kumbuka! Kupumzika uwapo safarini kutakuwezesha kupata nguvu zaidi na kutoa nafasi ya gari lako kupoa ili kuepusha ajali ya gari kuwaka moto.

3. Fahamu sheria na kanuni
Kuna kanuni zinazotawala matumizi ya barabara pamoja na vyombo vya usafiri. Ili kuepuka kuingia kwenye matatizo, hakikisha unafahamu vyema sheria za barabarani za eneo unalokwenda.

Unaweza kuzingatia haya:
Beba vibali na nyaraka muhimu za dereva na gari Mf. leseni, bima, n.k.
Kama utavuka mipaka ya nchi beba pasi ya kusafiria pamoja na Visa kama inahitajika.

4. Beba vitu muhimu
Kama ilivyo ada, safari inahitaji maandalizi. Hakikisha unabeba vitu muhimu unavyoweza kuvitumia kwenye safari yako kama hivi vifuatavyo:

Chakula na vinywaji. Ikiwa hutonunua chakula au kupata mahali pa uhakika pa kununua chakula na vinywaji, basi beba chakula chako utakachokula mara uwapo safarini.

Beba kisanduku cha huduma ya kwanza. Ni muhimu kuwa na kisanduku cha huduma ya kwanza kwenye gari ili upatapo tatizo la kiafya kikusaidie.
Beba vifaa vya msingi vya matengenezo ya gari. Vifaa kama vile jeki, spana, tochi, n.k. ni muhimu sana.

5. Tumia mafuta vizuri
Hakikisha unatumia mafuta vizuri mara uendeshapo gari umbali mrefu ili kuhakikisha unapunguza gharama zisizokuwa za lazima.

Hakikisha pia huachi kiwango cha mafuta kipungue sana ili usije ukaishiwa mafuta kwenye eneo ambalo liko mbali na kituo cha mafuta.

6. Usitumie kilevi
Chanzo kikubwa cha ajali ni ulevi au matumizi ya pombe kwa madereva. Pombe hukufanya ushindwe kumudu gari vyema, hivyo usitumie kilevi kabla na wakati wa safari.

7. Fahamu kuhusu hali ya hewa
Safari yako inaweza kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na hali ya hewa. Hivyo ni vyema ukahakikisha unafahamu hali ya hewa ya eneo unalokwenda ili ujiandae mapema.

Kwa mfano kama kunatarajiwa kunyesha mvua, ni vyema ukachunguza kama barabara utakayoitumia kama huwa inapitika wakati wa mvua ili usije ukakwama.

8. Endesha kwa mwendo wa wastani
Mwendokasi ni chanzo kikubwa cha ajali na matatizo mengi barabarani. Ni muhimu kuendesha gari kwa mwendo wa wastani ili kuepusha matatizo yasiyokuwa na ulazima.
Kumbuka! Unapoendesha gari kwa mwendo wa wastani ni rahisi kujihami mara kunapotokea tatizo barabarani.

9. Zingatia burudani
Burudani tena? Ndiyo, unaweza kubeba miziki ambayo itakuburudisha wewe pamoja na wale unaosafiri nao ili msichoke muwapo safarini. Kusikiliza mziki wakati wa kuendesha gari kutakuweka katika hali (mood) nzuri sana.

10. Fahamu vyema eneo unalokwenda
Je unafahamu vyema barabara utakayoitumia kufika kwenye eneo unalokwenda? Ili kuepuka kupotea au kukwama kwenye safari yako, ni muhimu ukafahamu vyema eneo unalokwenda. Unaweza kuwauliza watu wanaofahamu eneo hilo au kutumia ramani mbalimbali kama vile Ramani za Google.

C&P

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
 
NAULI MPYA ZILIZOPANGWA NA SUMATRA ZA MABASI YA KWENDA MIKOANI KUTOKEA DAR: BEI ZOTE NI KWA SHILINGI YA TANZANIA.
DAR - ARUSHA = Basi la kawaida 22,700/=, Semi luxury bus 32,800/=, Luxury bus 36,000/=
DAR - BABATI via ARUSHA = Basi la kawaida 29,000/=, Semi luxury bus 41,800/=, Luxury bus 45,900/=
# DAR - BUKOBA via DODOMA = Basi la kawaida 55,100/=, Semi luxury bus 77,300/=, Luxury bus 85,000/=
DAR - DODOMA = Basi la kawaida 16,700, Semi luxury bus 24,100/=, Luxury bus 26,400/=
DAR - IRINGA = Basi la kawaida 18,300/=, Semi luxury bus 26,300/=, Luxury bus 28,900/=
DAR - KIGOMA = Basi la kawaida 58,800/= Semi luxury bus 80,900/=, Luxury bus 88,900/=
DAR - LINDI = Basi la kawaida 17,800/= Semi luxury bus 24,400/=, Luxury bus 26,800/=
DAR - MBEYA = Basi la kawaida Basi la kawaida 30,700/=, Semi luxury bus 44,300/=, Luxury bus 48,700/=
DAR - MOROGORO = Basi la kawaida 7,100/=, Semi luxury bus 10,300/=, Luxury bus 11,300/=
DAR - MOSHI = Basi la kawaida 19,800/=, Semi luxury bus 28,500/=, Luxury bus 31,300
DAR - MTWARA = Basi la kawaida 21,500/=, Semi luxury bus 29,700/=, Luxury bus 32,600/=
DAR - MUSOMA kupitia DODOMA = Basi la kawaida 50,800/=, Semi luxury bus 73,200/=, Luxury bus 80,500/=
DAR - MWANZA kupitia DODOMA = Basi la kawaida 42,600/=, Semi luxury bus 61,400/=, Luxury bus 67,500/=
DAR - SHINYANGA = Basi la kawaida 36,600/=, Semi luxury bus 52,700/= Luxury bus 57,900/=
DAR - SINGIDA kupitia DODOMA = Basi la kawaida 25,500/=, Semi luxury bus 36,800/=, Luxury bus 40,400/=
DAR - SONGEA = Basi la kawaida 35,000/=, Semi luxury bus 50,600/=, Luxury bus 55,500/=
DAR - SUMBAWANGA = Basi la kawaida 45,100/=, Semi luxury bus 62,100/=, Luxury bus 68,200/=
DAR - TABORA = Basi la kawaida 39,000/=, Semi luxury bus 54,700/=, Luxury bus 60,100/=
DAR - TANGA = Basi la kawaida 12,800/=, Semi luxury bus 18,500/=, Luxury bus 20,300/=
DAR - KIBAHA = Basi la kawaida 1000/=, Semi luxury bus 1,500, Luxury bus 1,600/=

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom