Mada Maalum ya Madereva: Changamoto, Uzoefu, Vituko na Connections

Mada Maalum ya Madereva: Changamoto, Uzoefu, Vituko na Connections

Nakumbuka mwaka jana naendesha gari toka babati-Arusha ilikuwa usiku wa manane kuna eneo wanapaita mbuyu wa mjerumani nikaona mbele kama mita 100 watu kama wamama wamevaa kama mashuka na wamefunga vitambaa vyeupe kichwani nikaongeza taa full na kupunguza mwendo,,pale kuna kama konaa hivi gafla naifikia ile kona sioni chochote pale wala wale watu siwaoni,,aseh alafu kwenye gari nilikuwa peke ya ngu,,sikuelewa lile tukio kabisa
Hapo ni kilingeni...una bahati hujapata madhara

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
 
Habarini wana jumuiya kubwa ya JamiiForums,

Ni wakati sasa wa kuwa na mada yetu maalum kwa kaliba hii kubwa na pana yenye dhamana adhimu ya kuhakikisha tunasafiri na kufika tuendako salama iwe:
  • Makazini
  • Kwenye starehe
  • Kwenye dharura
  • Kutembeleana nknk
Ni kaliba hii adhimu pia yenye dhamana kubwa ya kufikisha salama mizigo na vifurushi vyetu vyote vya kibiashara, kikazi nknk

Mada hii maalum ni jumuishi ya:
  • Madereva wa magari makubwa na madogo ya mizigo
  • Madereva wa boda to boda
  • Madereva wa magari yote ya abiria
  • Madereva wa viongozi, matajiri na watu maarufu
  • Madereva wa mitambo
  • Madereva bajaj bodaboda wote kwa ujumla wao
  • Na mwisho kabisa madereva wa magari binafsi
Mada hii ni maalum pia ya kusimuliana changamoto mbalimbali za barabarani kuanzia vibali, uendeshaji mbovu, ushirikina, maafisa usalama, mamlaka zenye dhima na usafiri nk.

Kuna ishu ya uzoefu pia ambayo tunaweza kushirikishana hapa ili kupata uzoefu incase likitokea la kutokea ujue jinsi ya kukabiliana nalo

Hakuna mahali hapakosi vituko na vibweka. Kwenye hii kaliba pana ya usafiri vipo vya kutosha. Je, una kituko chochote? Huu ni uwanja wako sasa.

La mwisho lakini ambalo si la mwisho kabisa ni swala zima la kupeana connection. Madereva wazoefu na wazuri ni wengi mno lakini shida inakuja kwenye ajira. Kupitia mada hii nina HAKIKA TUNAWEZA KUPEANA SHAVU LA AJIRA

Ni mada pana na yenye ulingo mpana sana. Kuna mengi ambayo sijaandika hapa. Naomba ushiriki wenu kwa yale niliyosahau.

Dondoo baadhi za uzoefu wangu kwenye udereva
  • Nidhamu barabarani huepusha ajali nyingi
  • Barabarani derava hapaswi kuwa na maamuzi mawili kwa wakati mmoja
  • Muda wote ni dereva anapokuwa kwenye usukani ni lazima macho yake yaone sekunde 15 mbele toka alipo
  • Inapotokea dharura ya pancha si vema kufunga breki ghafla
  • Muhimu muda wote kusoma taa za tahadhari kwenye dashboard
Tutazidi kushirikina mengi kadiri mada itakavyokuwa inaendeleea, na hata kama kuna links za kazi za udereva tutapeana hapa
Nitangulie kuwatakia maandalizi mema ya sikukuu za mwisho wa mwaka.

Kwa madereva wenzangu tuna DHIMA kubwa ya kuzivusha salama mwaka huu roho za mamilioni ambazo ni ndugu jamaa marafiki na wanadamu wenzetu.

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
Hello Madereva,

Kuna hizi nafasi za kazi za madereva wa magari na madereva wa bodaboda zimetangazwa na shirika la MDH... Ni kazi za temporary (January-Septemba 2021). Jaribuni bahati yenu, deadline imekaribia sana (ni keshokutwa tarehe 10)-Ila mnaweza kui meet maana hawahitaji vitu vingi sana. Sana sana ni vyeti vyako, picha ya passport size na barua ya wadhamini wawili na mwenyekiti serikali za mitaa. Penye nia pana njia.
Nimepost hapa baada ya Mshana Jr kuniomba nifanye hivyo. See the links below

[emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545] Thanks Dr..!!

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
 
Mshana Jr we acha tu.
Dereva anakupa helmet ukiiangalia humu pembeni kwa ndani kuna uchafu wa kutosha.
Ndio maana watu wengi wanasita kuvaa helmet japo ni nzuri kwa usalama wa abiria.
Pamoja na baadhi ya wadau kuwagaia madereva wa bodaboda helmet mbilimbili tena bure kabisa bila malipo, ila suala la usafi wa hizo helmet hawalizingatii kabisa.
Unashika kuivaa unakuta inanuka jasho, mafuta ya nywele au ina weusi...ndii maana vichwa vyetu vinawaka mashetani kila siku kutokana na kuvaa magundu na mabalaa ya wengine.
Tunavagaa mikosi ya wengine.

Mada nzuri sana hii Mshana Jr
Nunueni kofia zenu sasa
 
nadhani humu na askari wa barabarani watoe koment zao sio kusoma tuu na kubadili mbinu zenu.wengi wenu ni washenzi sana tukiwapa ata leseni zetu mkague tuu mnatuchorea mkeka bila kosa lolote!!matokeo yake deni linabet bila dereva kujua.ukishtuka iko elf60
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
 
Asante kwa uzi mzuri.
Mm naomba mwenye connection au kujuana na wale ma agent au makampuni yanayotoa magari ya IT pale bandarini. Jana ni siku ya 3 naenda pale kwanzia asubuhi mpaka sita usiku bila mafanikio. Mm nidereva mwenye uzoefu wa miaka 10 kwa safari ndefu na fupi. Kazi yangu ya mwisho kufanya ni ya uber baada ya korona kuingia mwenye gari ali park gari yake na sasa kaitoa uber kabisa. Nategemea baada ya Noel kupita nirudi tena pale bandarini kujaribu tena. Asnte
Ndugu kazi za it ni tofauti Sana na jinsi unavyofikiri.jambo la Kwanza ukitaka kupata hizo gari ujuane na clearing agent au ujuane na dereva mwenzako ambae atakuunganisha na hao mawakala wa forodha ndipo unaweza pata kazi vinginevyo utakuwa unapoteza muda bure tu
 
Kuendesha gari ni suala linalohitaji umakini na utulivu mkubwa, hasa pale unapoendesha gari umbali mrefu. Mara kwa mara kumeshuhudiwa ajali mbalimbali ambazo kimsingi zinatokana na madereva kutokuzingatia kanuni muhimu katika utumiaji wa vyombo vya usafiri.

Ili kuhakikisha usalama wako pamoja na watumiaji wengine wa barabara, yapo mambo kadhaa unayopaswa kuyazingatia kabla na wakati wa kuendesha gari umbali mrefu.

1. Kagua na andaa gari
Kabla ya safari yoyote gari linahitaji kukaguliwa na kuandaliwa, hasa kabla ya safari ndefu. Kuna mambo kadhaa unayohitaji kuyakagua kwenye gari lako:

Kagua hali na ubora wa magurudumu. Hakikisha magurudumu yamejaa vizuri na hayajazeeka. Kagua mafuta lainishi (oil). Hakikisha gari yako ina mafuta lainishi ya kutosha tena ya ubora unaotakiwa.

Kagua kiasi cha maji. Maji? Ndiyo maji ni muhimu sana kwenye gari kwa ajili ya kupooza injini ya gari pamoja na kusafishia vioo.Kagua utendajikazi wa injini. Hakikisha injini yako inafanya kazi vizuri.

Kagua sehemu nyingine za gari kama vile breki, kiongeza mwendo (accelerator), usukani, taa, honi, viashiria (indicators), n.k. Usibebe mizigo isiyokuwa ya lazima kwenye gari. Hii itakupotezea mafuta na nafasi bila sababu.

Hakikisha unalikagua gari lako vyema na kuliandaa kwa ajili ya safari. Unaweza pia kumtumia mtaalamu wa magari ili akusaidie kulikagua na kuliandaa kwa safari yako.

2. Pumzika
Ili uweze kuendesha gari vyema wakati wa safari ndefu ni muhimu kupumzika kwa kiasi cha kutosha kabla na wakati wa safari.

Hakikisha kabla ya safari unapata muda wa kutosha wa kulala ili kuepusha kusinzia barabarani kunakoweza kusababisha ajali.

Unapokuwa barabarani unaweza pia kupumzika baada ya umbali fulani ili usichoke sana.
Kumbuka! Kupumzika uwapo safarini kutakuwezesha kupata nguvu zaidi na kutoa nafasi ya gari lako kupoa ili kuepusha ajali ya gari kuwaka moto.

3. Fahamu sheria na kanuni
Kuna kanuni zinazotawala matumizi ya barabara pamoja na vyombo vya usafiri. Ili kuepuka kuingia kwenye matatizo, hakikisha unafahamu vyema sheria za barabarani za eneo unalokwenda.

Unaweza kuzingatia haya:
Beba vibali na nyaraka muhimu za dereva na gari Mf. leseni, bima, n.k.
Kama utavuka mipaka ya nchi beba pasi ya kusafiria pamoja na Visa kama inahitajika.

4. Beba vitu muhimu
Kama ilivyo ada, safari inahitaji maandalizi. Hakikisha unabeba vitu muhimu unavyoweza kuvitumia kwenye safari yako kama hivi vifuatavyo:

Chakula na vinywaji. Ikiwa hutonunua chakula au kupata mahali pa uhakika pa kununua chakula na vinywaji, basi beba chakula chako utakachokula mara uwapo safarini.

Beba kisanduku cha huduma ya kwanza. Ni muhimu kuwa na kisanduku cha huduma ya kwanza kwenye gari ili upatapo tatizo la kiafya kikusaidie.
Beba vifaa vya msingi vya matengenezo ya gari. Vifaa kama vile jeki, spana, tochi, n.k. ni muhimu sana.

5. Tumia mafuta vizuri
Hakikisha unatumia mafuta vizuri mara uendeshapo gari umbali mrefu ili kuhakikisha unapunguza gharama zisizokuwa za lazima.

Hakikisha pia huachi kiwango cha mafuta kipungue sana ili usije ukaishiwa mafuta kwenye eneo ambalo liko mbali na kituo cha mafuta.

6. Usitumie kilevi
Chanzo kikubwa cha ajali ni ulevi au matumizi ya pombe kwa madereva. Pombe hukufanya ushindwe kumudu gari vyema, hivyo usitumie kilevi kabla na wakati wa safari.

7. Fahamu kuhusu hali ya hewa
Safari yako inaweza kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na hali ya hewa. Hivyo ni vyema ukahakikisha unafahamu hali ya hewa ya eneo unalokwenda ili ujiandae mapema.

Kwa mfano kama kunatarajiwa kunyesha mvua, ni vyema ukachunguza kama barabara utakayoitumia kama huwa inapitika wakati wa mvua ili usije ukakwama.

8. Endesha kwa mwendo wa wastani
Mwendokasi ni chanzo kikubwa cha ajali na matatizo mengi barabarani. Ni muhimu kuendesha gari kwa mwendo wa wastani ili kuepusha matatizo yasiyokuwa na ulazima.
Kumbuka! Unapoendesha gari kwa mwendo wa wastani ni rahisi kujihami mara kunapotokea tatizo barabarani.

9. Zingatia burudani
Burudani tena? Ndiyo, unaweza kubeba miziki ambayo itakuburudisha wewe pamoja na wale unaosafiri nao ili msichoke muwapo safarini. Kusikiliza mziki wakati wa kuendesha gari kutakuweka katika hali (mood) nzuri sana.

10. Fahamu vyema eneo unalokwenda
Je unafahamu vyema barabara utakayoitumia kufika kwenye eneo unalokwenda? Ili kuepuka kupotea au kukwama kwenye safari yako, ni muhimu ukafahamu vyema eneo unalokwenda. Unaweza kuwauliza watu wanaofahamu eneo hilo au kutumia ramani mbalimbali kama vile Ramani za Google.

C&P

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
Mkuu hongera Sana kwa mada uliyoanzisha bila kusahau elimu unayotoa.nakupongeza Sana kwa sbb hii taasisi ya udereva ni kubwa Sana lkn ni moja ya kazi ambazo naweza kusema serikali imeisahau .yaani umekuwa Kama mtoto yatima.ni moja kati ya kazi iliyoajiri watanzania wengi Sana.shida labda ninayoiona ni kwakua ni kati ya kazi ambazo walio wengi sio wataaluma .mkuu Kama itakupendeza Mimi pia ni dereva sikubahatika kuwa na elimu ya secondary lkn nilimaliza darasa la saba.nina leseni ya udereva na pia nilipitia chuo Cha usafirishaji NIT nikapata cheti Cha PSV Nina majaraja yote yanayoniruhusu kuendesha magari ya abiria makubwa na madogo pia Nina leseni inayoniruhusu kuendesha magari makubwa ya mizigo na nimeenda masafa marefu katika nchi mbalimbali east Central and southern.kama utakuwa na connection usisite kunipa mkuu .nipo tayari kufanya kazi nchi yoyote kwa utii na kufuata taratibu zote zinazostahili.
 
Amina asante kwa pongezi nitafanya jitihada kukutafutia connection kwakuwa umekuwa muwazi na mkweli

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
 
Huyo wa Fuso wangemkamata wamfunge kamba kwenye Fuso yake KILA abiria amlambe bakora tatu tatu Ili iwe funzo siku nyingine awe na adabu.

Madereva wa malori waelewa wakishaliona Basi tu kwa nyuma anakupisha anajua unawahi. Basi haliwezi kwenda mwendo wa lori Basi linatembea mwendo wa biashara sasa kama Fuso alimbania overtake wa Basi atembee kama Fuso bakora ndo adhabu yake.
Husiongee kitu husichokijua....
 
Back
Top Bottom