Mada Maalum ya Madereva: Changamoto, Uzoefu, Vituko na Connections

Mada Maalum ya Madereva: Changamoto, Uzoefu, Vituko na Connections

IMG-20221101-WA0113.jpg
 
Kaka habar mm ni dreva wa Lori na hata gari ndogo nilikuwa naomba connection hata za IT napambana sana ila shida connection hata leo nilitoka uko uko....nafasi yeyote hile ya udreva napambana nao hata iwe pikipiki ama bajaji....kama unaconection namba yangu ni hi 0687354161
 
TAHADHARI KWA ABIRIA WAISHIO DAR ES SALAAM
Ikifika jioni maeneo ya Mnazi Mmoja kwa sababu ya shida ya usafiri wa kutoka katikati ya jiji kwenda maeneo mbalimbali pembezoni mwa mji, kuna wapiga debe hutangaza usafiri kwa nauli ya shs Elfu Mbili, kwenye moja ya Magari Madogo na Noah. Hususani maeneo ya karibu na Benki ya CRDB Tawi la Lumumba.
Majuzi jamaa Mmoja alipanda hizo gari akiwa na wenzake ikidaiwa inaelekea Gongo la Mboto. Matokeo yake walitekwa na watu wenye silaha ambao awali walijifanya nao ni wasafiri na kuporwa kila kitu baada ya kupelekwa Pugu Mnadani Wakasachiwa huku wakitishiwa kupigwa risasi na kuchinjwa kwa visu walivyokuwa wamebeba.
"Ukiweza wajulishe wengine ili wapande usafiri huo kwa tahadhari au wakiweza waachane nao"
Ahsante Sana kwa UKUMBUSHO huu ni HATARI SANA hasa ukiwa PEKE yako.
 
WAENDESHA BAISKELI WAUAWE TU! [emoji706][emoji706]
Baiskeli zina ua polepole uchumi wa Dunia.
Mfanyakazi mmoja wa benki aliwafanya wanauchumi wafikirie aliposema maneno haya:
"Waendesha baiskeli ni janga kwa uchumi wa nchi: hawanunui magari na wala hawakopi pesa kununua, hakuna anayelipa bima.Hawanunui mafuta, Hawalipii huduma za gari, na hakuna matengenezo yanayohitajika. Hawalipii maegesho. Hawasababishi ajali kubwa. Uwepo wao unafanya kusiwepo haja ya barabara nyingi.
Na hawanenepi hawa watu [emoji706][emoji706].
Watu wenye afya bora kama hawa, hawafai kwenye uchumi.Hawanunui dawa. Hawaendi hospitalini wala kuonana na madaktari.
Hawaongezi chochote katika Pato la Taifa.Hebu fikiri tu, Kila mgahawa mpya wa KFC unazalisha ajira 30 zaidi, madaktari wa moyo 10, madaktari wa meno 10, wataalam wa lishe na chakula 10 - achilia mbali watu wanaofanya kazi katika mgahawa wenyewe."
Kipi muhimu: baiskeli au KFC?.Na hawa watembea kwa miguu ndio hawafai kabisa. Yani hawanunui hata baiskeli![emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom