Mada Maalum ya Madereva: Changamoto, Uzoefu, Vituko na Connections

IMG-20230428-WA0150.jpg
 
Cha kushangaza zaidi bara bara zetu ni ndogo au nyembamba sana .Wabunge wetu bungeni ni watu hovyo hovyo sana hakuna mtu anaeyazungumzia haya mambo .Burget ya mambo mengiii hakuna hata moja linalokuwa kama mimi Raisi nahakikisha kila mwaka nafanya kitu kimoja tu Kama ni UMEME natia Burget ya umeme 2023 Nahakikisha umeme kwa muda wa miaka 50 inayokuja sio tatizo tena , na hizo wizara nyengine ni burget ya mishahara yao tu na mwaka mwengine ni burget ya maji hali kadhalika barara na vitu vyengine kila mwaka kitu kimoja tu
 
Anaandika mzee Joseph Magee Jandwa
__
Leo imetimia miaka 25 tangu ajali ya basi iliyosababisha vifo vya abiria 96 na majeruhi 9, ilipotokea jioni ya tar 3/5/1998. Kihistoria haijawahi kutokea ajali mbaya ya basi iliyoua watu wengi kama hiyo.

Mimi ni miongoni mwa wale 9 tulionusurika kwa neema ya Mungu. Ajali hii ilihusisha basi la kampuni ya NO CHALLENGE ambayo baada ya ajali ilibadili jina na kujiita TASHRIF. Ajali ilitokea Mkoani Tanga, Wilaya Muheza, kijiji cha Kibanda. Bus lenye namba za Usajili TZK 960 lilikuwa likitoka Tanga kuelekea DSM.

Kipindi hicho kulikuwa na mvua nyingi zilizobatizwa jina Mvua za El-Nino. Tulipofika kijijini hapo tulikuta mabasi mengi yamesimama kutokana na kujaa maji kwenye mto. Kuanzia mabasi makubwa hadi madogo kama Coaster, Hiace na gari binafsi.

Kijiji cha Kibanda kuna mto uitwao Msangazi. Ulikua umejaa maji. Basi letu lilijaribu kuvuka ng'ambo ya pili ili kuendelea na safari. Baadhi ya abiria wa mabasi mengine walidandia basi letu ili wavuke kuendelea na ratiba zao. Lakini halikuweza kufika ng'ambo. Lilisombwa na maji. Likasukumwa mtoni na kuzama kabisa.

Watu 96 wakapoteza maisha, wakiwemo wale waliodandia. Sehemu kubwa ya abiria walifia ndani ya basi kwa kushindwa kutoka. Wachache waliotokea madirishani walikufa kwa kusombwa na maji yenye kasi ya mto huo. Ilikua simanzi kubwa.

Pamejengwa mnara wa kumbukumbu ya wafu na majina yao. Lakini naambiwa vijana wa vyuma chakavu wamekwanyua kibao kilichokuwa kimeorodhesha majina ya wafu 72 waliotambulika na wengine 24 ambao hawakutambuliwa.

Katika wale 9 tuliosalimika, alikuwepo Mzee Ramadhani Kimbunga Dereva wa basi hilo. Bahati mbaya pamoja na kuokoka kwenye ajali hiyo alikuja kufa miezi michache baadae kwa kifo cha kawaida. Manusura wengine wawili nao walishafariki kwa nyakati tofauti, na tuliosalia hai mpaka sasa ni 6 tu.

Baada ya ajali hiyo kampuni ya NO CHALLENGE ikabadili jina kuwa TASHRIF. Ikumbukwe kabla ya hapo ilikua ikiitwa AIR SHENGENA. Ilipopata ajali ya kugonga treni Korogwe mwaka 1996 ikaitwa NO CHALLENGE. Na baada ya ajali ya maji Muheza ikaitwa TASHRIF. Nimeona niwakumbushe maana wengi wamesahau. Tujifunze kupitia kisa hiki ili kuepusha ajali nyingine za aina hii.!
 
Kama kuna wenye ndugu zao waliosafiri na bus la KIDINILO leo wapige simu waulizie huko au hao waliokuwa kwenye gari ndogo kama ni ndugu zao[emoji33][emoji33][emoji33]
 
Mkuu na ile Ajali ilotokea pale singida nasikia nayo ni kubwa mno watu wakazikwa pale pale
 
Air shengena nilikuwa naisikia japo kipindi iko nilikua mdogo bado
 
Back
Top Bottom