Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

wakuu naomba nielimishwe zaidi kuhusu izi gauge kama zinavyonekana kwenye hio picha.najua zinaongeza speed na nguvu tu ila naomba kujuzwa ni magari ya aina gani inakubali or ni any car??
 

Attachments

  • 1435598916363.jpg
    23.8 KB · Views: 373
msaada jmn uzuri na ubaya wa nissan march

Shida ya Nissan march iko kwenye gear box kuna wakati ukiwa unapanda mlima hata mtembea kwa miguu anakuwacha apo ujue imeanza kuzingua. faida kidogo fuel consumption inachukua nafasi
 
Jamani Toyota fortuner mwaka 2005 inaweza ikawa shillings ngapi mpya kutoka Japan mpaka kuitoa bandarini
 



Asanteni sana kwa elimu safi kuhusu magari yetu. Ifahamike pia kwamba gari ambayo upepo wake wa matairi hauko sawa ( yaani "unbalanced tyre pressure"), mfumo chakavu wa bushi (hasa za chini) na matairi ambayo hayako katika mstari mnyoofu (nonaligned tyres), huwa inachakaa haraka kuliko unavyofikiri. Watu wengi hawalijuwi hili. Wao wanaangalia na kuitunza injini tu na usafi wa gari, huku wakisahau kuwa ingini inatwishwa mzigo mzito wa kuisukuma gari tajwa. matokeo yake gari inalamba mafuta mengi na taratibu ingini inachoka na hatimaye kufa kabisa.

Shime ewe mwenye gari, tunza chombo chako kama vile hutanunua kingine. Kagua mara kwa mara gari yako. Ukiwa kwenye barabara iliyonyooka, lenga vimistari- - - -( au mstari mweupe) achia usukani kidogo. Je, tairi za kulia zinafuata mstari huo? Gari ambayo iko sawa, tairi zitafuata na kukanyaga vimista/mstari wa katikati ya barabara bila ya wewe kushika usukani. Je, inavuta kulia au kushoto? kama ndiyo, basi ipeleke gari kwa gereji ikarekebishwe.

Nakutakia uendeshaji mwema!!!
 
Wakuu naomba kuelewesha madhara ya silencer kuwa juu ktk gari hasa hizo ndogo/saloon car. Na ni nini sababu ya hiyo silencer kuwa juu.?!
 

Siku nyingine ukienda, atachomoa cable ya odo, atapiga misele ya kutosha kisha akirudi anarudishia cable, ukija unakuta zero yako uliyo-reset
 
Mkuu hivi Passo ina uwezo wa kusafiri toka Dar hadi Mwanza non stop?

kwanini isiweze? unahofia udogo wa injini? kama udogo wa injini mimi nina pajero mini cc 660 ya mwaka 1995 huwa nasafiri kilometa zaidi ya elfu moja kwa siku moja, kwa udogo wake huwa naenda reasonable speed isiyozidi 90. naiwasha mwanzo wa safari saa 12 asb siizimi hadi nafika saa 6 -7 usiku. sijafanya mara moja, nishafanya safari hizo za kati ya km 1100 hadi 1200 zaidi ya 8 kwa umbali huo bila matatizo.
 
Kwa ufupi big up sana kwa mleta uzi huu, binafsi nimejifunza mambo mengi sana ambayo sikuwa nayajua juu ya magari. sikutaka kuwa mvivu au kudandia gari kwa mbele, nimeanza nao mwanzo hadi mwisho, japo imenichukua siku kadhaa za kutosha lakini nimejifunza mengi.

big up kwa mshana jr na wachangiaji wote, kwa kweli tunahitaji jukwaa kwa ajili ya mambo ya magari, manake si rahisi mtu kwa sasa anauliza kitu, anaambiwa soma post zilizotangulia, hajui wapi, kama hajapata muda wa kupitia uzi mzima, inakuwa balaa. duh!!!!!!!!!!!!!!!!
 
kuna mdau aliuliza kuhusu harrier kuwa anapenda kuibadilisha rav 4 yake, comment zilikuja aachane na harrier maana ina shida ya gear box,
binafsi namshauri aende kwa anayo vutiwa nao, wengi wameeleza uzoefu wa jamaa zao, haya magari used sijui niseme bahati au nini. maana unaweza kukuta gari aina moja, mwaka na mwezi wa kutengenezwa mmoja, ila moja inashida hii nyingine mwendo mdundo. kuna wenye harrier wala hawajui hilo tatizo la gear box, kuna jamaa yangu ana Rav 4 gear box ilimsumbua hadi hataki kusikia kitu Rav 4.

kuna watu humu wametaja Toyota Cami kama the best, lakini kuna wengine wamezilalamikia pia, kuna watu wamesiku passo, kuna waliozilalamikia pia, cha msingi kile unachokipenda chukua, gari yoyote ni utunzaji na service, cha zaidi ulizia pa kupata spea ili ununue ukijua spea utapata wapi, utaagiza Nairobi, japan au kwa madiba.
 

Mi mwenyewe nilimshauri hivyo hivyo mkuu
 
Fuel consuption inakuwa juu

Alaaaaa kumbe. Ahsante sana bwana Mshana jr. Pia nilikuwa nasikia engine inatoa mlio flani hivi wa kucheketa km mashine ya kusaga aiseee. Ndio jamaa angu akamniambia kuwa kaka gari yako silence ipo juu.
 
Alaaaaa kumbe. Ahsante sana bwana Mshana jr. Pia nilikuwa nasikia engine inatoa mlio flani hivi wa kucheketa km mashine ya kusaga aiseee. Ndio jamaa angu akamniambia kuwa kaka gari yako silence ipo juu.

Yeah lakini pia hebu check na engine oil kama haijapungua kwakuwa ikipungua hutoa huo mlio
 
Yeah lakini pia hebu check na engine oil kama haijapungua kwakuwa ikipungua hutoa huo mlio

Yap nikaipeleka fasta kwa fundi wangu. Akaifanyia service ya kuishusha hiyo silence na pia akabadili hiyo engine & gearbox oil.
 
Wadau kwa wenye uzoefu na magari nisaidieni ushauri. Nimelipenda gari aina ya toyota volts. Nataka kununua. Mnanishaurije?
 
Habari za humu jamii forum naombeni msaada ya kuijua kiundani gari aina hii ya bighon seat capacity ukubwa wa engine bei yake yard kwa sasa inasifa gani kwa ujumla yaani positive na negative effects natanguliza shukurani zangu asanteni
 
gari ya ukweli mwaka wa 2 nipo nayo haijawah nisumbua kubadilisha vitu vidogo vidogo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…