Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
msaada jmn uzuri na ubaya wa nissan march
Kumekuwa na mada nyingi kuhusu mambo yote yahusuyo magari, nikaona basi na sisi tuwe na Uzi huu ambapo habari zote zihusuzo magari kuanzia kuchagua, kuagiza, kuuza, kubadili nyaraka, matengenezo utunzaji na kadhalika.
Watu wengi wametapeliwa kwenye mauzo na manunuzi, kwenye nyaraka, kwenye vipuri kwenye matengenezo na hata matumizi.
Kwa Uzi huu basi kila mwenye ujuzi, uzoefu, ushauri au mwenye maswali na tatizo lolote linalohusiana na magari hapa ndio pawe uwanja wake
Karibuni sana
Ushauri: Jinsi ya kununua gari iliotumika ndani ya Tanzania
View attachment 225786
Mbona hazionekani vizuri?
Hasa hasa kujua umbali wa gari iliyotembea hasa ukireset zero
Kuna siku niliacha gari kwa fundi halafu ONDO nikareset 0 ilikuwa ijumaa, tulikubaliana niichukue gari jumanne iliyofuata yani siku nne baadae!siku ananikabidhi gari ilikuwa imetembea km 68 nilimweleza kuhusu hilo na nikamkata hela
Mkuu hivi Passo ina uwezo wa kusafiri toka Dar hadi Mwanza non stop?
kuna mdau aliuliza kuhusu harrier kuwa anapenda kuibadilisha rav 4 yake, comment zilikuja aachane na harrier maana ina shida ya gear box,
binafsi namshauri aende kwa anayo vutiwa nao, wengi wameeleza uzoefu wa jamaa zao, haya magari used sijui niseme bahati au nini. maana unaweza kukuta gari aina moja, mwaka na mwezi wa kutengenezwa mmoja, ila moja inashida hii nyingine mwendo mdundo. kuna wenye harrier wala hawajui hilo tatizo la gear box, kuna jamaa yangu ana Rav 4 gear box ilimsumbua hadi hataki kusikia kitu Rav 4.
kuna watu humu wametaja Toyota Cami kama the best, lakini kuna wengine wamezilalamikia pia, kuna watu wamesiku passo, kuna waliozilalamikia pia, cha msingi kile unachokipenda chukua, gari yoyote ni utunzaji na service, cha zaidi ulizia pa kupata spea ili ununue ukijua spea utapata wapi, utaagiza Nairobi, japan au kwa madiba.
Fuel consuption inakuwa juu
Alaaaaa kumbe. Ahsante sana bwana Mshana jr. Pia nilikuwa nasikia engine inatoa mlio flani hivi wa kucheketa km mashine ya kusaga aiseee. Ndio jamaa angu akamniambia kuwa kaka gari yako silence ipo juu.
Yeah lakini pia hebu check na engine oil kama haijapungua kwakuwa ikipungua hutoa huo mlio