twafa-kali
JF-Expert Member
- Dec 15, 2012
- 251
- 211
Asante kamanda ubarikiweHili tumeshalizungumza hapa mara nyingi tu mkuu lakini
D=normal drive, hapa fari inashift gear hadi gear za mwisho za gari kulingana na model (kuna 4 speed, 5 speed na siku hizi 6 speed). Hapa wengi ndio huwa wanaendesha kwa kawaida
D2=hii mara nyingi huwa inatumika kuzuia mzunguko wa gear (gear ratio) usizidi gear namba mbili, ukiiweka hii maana yake gari inaweza kuondokea kwenye gear namba mbili (hasa kwenye mazingira ya barafu) lakini pia inaizuir isiende gear za juu ili kuruhusu nguvu zaidi kwa engine...unapopanda mlima mkali au kushuka, na pia kama unavuta trela
L (Low) ni kama D1 (First) na yenyewe maelezo yake kama hapo juu ila inazuia (limit) mzunguko wa gear (gear ratio) kwenye namba moja tu. kwa magari ya kisasa, bado automatically itashift kwa gear ratio za juu kama gari ikifikia RPM ya kiasi fulani kuzuia uharibifu wa engine na gear box.
Karibu kama kuna swali zaidi
Maelezo yako yamejitosheleza