Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

mshana eeh,hii kitu naikubali sana,ila sijui ulaji wake wa wese na upatikanaji wa spea zake na bei zake ukoje??

Ulaji wa mafuta bodaboda cha mtoto spare zipo wala usihofu
 
Last edited by a moderator:
Naomba uzoef wako juu ya mark2 blit, hasa ubora na udhaifu wake mbali na kuwa chini
 
Naomba uzoef wako juu ya mark2 blit, hasa ubora na udhaifu wake mbali na kuwa chini

Naona ni gari ngumu lakini zilizokosa umaarufu nafikiri kutokana na ukubwa wa engine na shape yake
 
3000km kwa hydrolic ya gearbox mkuu?

Hata mimi nimeshangaa kidogo. Ninavyojua ile sio ya kubadilinkila service hasa kama unaweka za kiwango cha ubora wa hali ya juu. Muhimu ni kuangalia ubora wake mara kwa mara.
 
Nashukuru kukuta hii thread. Wakuu nlitaka kubadili plug za Toyota opa inatumia plug za sindano lakini fundi anasema tunaeza funga za kawaida tuu. Je hakuna madhara yoyote tukibadili hii aina ya plug.
Asante
 
Hapana usifanye modification, kuna madhara kama gari kutetema na fuel consumption kupanda
 
Hata mimi nimeshangaa kidogo. Ninavyojua ile sio ya kubadilinkila service hasa kama unaweka za kiwango cha ubora wa hali ya juu. Muhimu ni kuangalia ubora wake mara kwa mara.

Basi nafikiri mimi nafanya tofauti kwakuwa kila service normally km 6000 mabadiliko vyote
Na kwakweli imenisaidia sana kutunza gearbox
 
Kwa matumizi ya oil katika engine za magari huwa hatujitungii kichwani kuwa ni aina ipi ya oil utumie eti kwakua kwenye gari ya fulani kaona inamfaa zaidi, hapana,
Huwa tunafuata Manual Instruction book, kitabu cha kwenye gari ambacho kinakuelekeza jinsi ya kutumia na kulifanyia matengenezo gari hilo.
Kwa aina nyingine za magari mf. Benz,Range Lover,Aud na mengineyo huwa yameandikwa Recommend oil katika cover's za engine ama bonet ya gari hiyo.
Ushauri wangu Tusome Manual Instructions Book ili kutoyaharibu magari yetu.
 
Watengeneza magari wanaingia contract na watengeneza oil. Mfano Bmw au MB wao wana contract na CASTROL ndio maana wameandika tumia Castrol,Peugeot wao wanashauri Total kwasababu wana contract nao.

Kwa faida yako muhimu ni namba ya engine oil either 5w40/10w50/10w60/0w40 ndio unayotakiwa kuzingatia na sio brand ya oil.
 
kwa kuongezea, magari mengi tunanunua used huwa yanakuja na mannual za kijapani, na hakuna tafsiri so we go by the rule of the thumb
 
Finally nimepata toyota duet,suzuki swift na vits zote fundi wangu amezikagua amesema ziko vizuri na price tofauti sio kubwa. naombeni comment za mwisho nsije jutia ndio gari ya kwanza, so which one i should go for.thanks in advance great thinkers.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…