Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Habari wanajamii? mi nina cresta Gx 100 juzi juzi imeanza tatizo nikipak juani sana nikija kuwasha nakuta pale panapoonyesha kilometre panafuta na pia gari inakuwa nzito ghafla kwenye daahboard kuna leta alama ile ya on/off mfululizo ila nikiendesha mwendo mrefu gari inarudi ktk hali ya kawaida. Tatizo laweza kuwa nini?
 
Polen kwa ujenzi wa Taifa,jamani naomba msaada wa kuelimishwa kuhusu gari zinazotokana na brand ya Audi,Audi A4 avante au Audi allroad moja kati ya matoleo haya hunivutia sana.Na hasa matumizi yangu nataka iwe ni ktk barabara ya lami na vumbi.Wataalamu nomba mnisaidie kusu ubora na udhaifu wa hizi gari na hasa matoleo ya 2002 na 2003.Natanguliza shukrani
 
Aksante sana nimejifunza jambo hapo, nilitaka kukurupuka nitafute kigari chenye CC 650 kisa mafuta kumbe ingekula kwangu
 
Last edited:
Wapendwa habari za usiku kuna siku nilileta swali hapa jinsi ya kubadili plug kwenye ford escape yangu..nilifanikiwa kufanya hilo zoezi sasa hivi majuz nimeunguza head gascate..nimepeleka gari cmc arusha lakin mpaka sasa hawajapata spare..naomba kuuliza pakupata spare hii..ni ford escape limited V6 2005.natanguliza shukrani.
 
wana JF nipendezwa na hii new model ya Escudo. Nataka kujua kwa ambayo wanaitumia. Vipi uimara wake? matumiz ya mafuta. upatikanikaji wa spare? na gharama za spare zake uki compare na toyota
thanks
Chukua kitu, mm nina V6 yake powa sana fully Ac na sijawahi juta. Spare zipo ila c sana
 
Wala husijisumbue we ingia ebay andika spare unayotaka na aina ya gari or model then ikija pale angalia kama seller can ship to Tanzania.....baada ya hapo buy it.

Mimi ninayo ford exploler eddie Bauer V8 hila sipati shida ya spare. Lakini make sure card yako ya bank imewezeshwa kufanya manunuzi online, na pia huwe na account ebay na sehemu kama PayPal pia.....ukiagiza spare mara nyingi ni siku kama 7 - 10.

Ukishindwa basi nenda pale tabata matumbi kwa yule mama anayeuza vifaa vya mazda na ford
 
Ushauri mzuri sana mkuu, lkn hawa DHL na companies nyingine za shipping hua wana charge vifurushi kulingana na uzito wa mzigo. swali langu, kwa uzito wa spea jamaa si watakua wana charge pesa nyingi sana mkuu
 
Bado ni gari mpya hazijakaa sana Tanzania na zinamilikiwa na wachache, ambao kati yao wamezisifia lakini fuel consumption iko juu
mkuu mshana naomba kufahamu kuhusu hizi caldina new model, je ni full time 4wd(zenye 4wd),na vip kuhusu uimara wake and maintenance.
 
Ushauri mzuri sana mkuu, lkn hawa DHL na companies nyingine za shipping hua wana charge vifurushi kulingana na uzito wa mzigo. swali langu, kwa uzito wa spea jamaa si watakua wana charge pesa nyingi sana mkuu
Mie niliagiza rejeta na oil cooler walinicharge $80 kwa usafiri na kodi yake, na bidhaa zote mbili walinichaji $250.....DHL au FEDEX wote wazuri hao mzigo unafika kwa wakati na unapewa tracking codes
 
mkuu mshana naomba kufahamu kuhusu hizi caldina new model, je ni full time 4wd(zenye 4wd),na vip kuhusu uimara wake and maintenance.
Tulikuwa nayo moja mwaka jana ila jamaa akafika bei faster ni mtu wa kahama mpaka leo hajutii Kama umeipenda chukua tu
 
asante mkuu.. na mafundi wapo wengi wa suziki?
Duh sijawah peleka kwa fundi so far, lkn hizi gari zinapendwa sana. Naziona nyingi nyingi tu za namba D... Unajua zamani zilikua ni DFP na STJ na wahindi kdg ndio waliweza kununua. Ila ushuru wake kaka jipange, andaa 10m ya TRA
 
Kuna gari mpaka USD 50 na ziko vizuri tu shida ni usafiri na kodi zetu unaweza kujikuta unatumia si chini ya ten million kwa gari ulilonunua laki moja
Hiyo bei ni CIF........?........

Mafundi kuna kagari nataka kukanunua ni Subaru GT 4 cylinder ndio nlivyoambiwa na muuzaji, hivyo ningependa kujua weakness and strength ya gari hii wakuu.
 
Mafundi kuna kagari nataka kukanunua ni Subaru GT 4 cylinder ndio nlivyoambiwa na muuzaji, hivyo ningependa kujua weakness and strength ya gari hii wakuu.
Subaru ni gari nzuri ila spare parts ziko juu kidogo , ichukue zingazia kanuni za kumiliki gari hutojuta
 
Mafundi kuna kagari nataka kukanunua ni Subaru GT 4 cylinder ndio nlivyoambiwa na muuzaji, hivyo ningependa kujua weakness and strength ya gari hii wakuu.
Subaru sawa na Nissan tu hakuna spare fake kama toyota zetu.....lakini ni gari nzuri na zinadumu sana na spea zinapatikana, jipange tu kwenye bei ya spea
 
Subaru ni gari nzuri ila spare parts ziko juu kidogo , ichukue zingazia kanuni za kumiliki gari hutojuta
Subaru sawa na Nissan tu hakuna spare fake kama toyota zetu.....lakini ni gari nzuri na zinadumu sana na spea zinapatikana, jipange tu kwenye bei ya spea

Wakuu vipi fuel efficiency ya gari ya aina hii! Subaru Gt 4cylinder? Ni ya kuridhisha au insane? Karibuni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…