Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Hivi bei ya registration TRA ktk card ya gari imeshuka maana kuna kadi nimeona bei ni sh 50,000 lkn ya kwangu bei yake ni 150,000?????
 
Naitwa, ELLY BASHIRI

shukrani kwa utaalamu na ujuzi wenu wanajamvi wa JF hususani ktk taaluma ya magari. Binafsi naomba ufafanuzi kidogo na ushauri kwenu. (1) Je ni vyema kuwa unaitumia O/D OFF per 80 speed above or O/D ON as usually kwenye safari ndefu..? eg; Mwanza to Dar (1,500 km).

(2). Je, na kama utatumia O/D OFF katika safari ndefu, (Mwanza to Dar ) consumption ya mafuta itaongezeka zaidi kutoka ktk normal consumption...?

Please, Ndugu MSHANA JR na waungwana wengine wenye taaluma hii naomba msaada wa Elimu hapa.

Aina ya Gari ni CRESTA GX-100, engine type ni VVT-i.
 
Over drive inaanzia speed 80, hivyo ni vema ukaicha On O/D always..
Consumption ya mafuta inaletwa na wrong driving kwamba unapanda speed na kushuka bila mpangilio
 
Okay, shukrani kiongozi kwa ushauri na ufafanuzi @ Mshana Jr.

Lakini naomba ni rudi tena kwako kiongozi MSHANA JR,
Niumeuliza hivyo kwasababu jana nilipanda gari moja aina ya Toyota PASSO nilikuwa natokea Mwanza kuja Shinyanga umbali ni Km 165, dereva alikuwa anatumia sana O/D OFF kila alipo fikia speed 80 na gari inakuwa nyepesi sana, nami nikafanya utafiti kidogo na kujiuliza maswali mengi kwa nini anaitumia sana O/D OFF, kwasababu ktk gari yangu sijawahi kutumia O/D OFF hata kama natoka Mwanza nakuja Dar.
Sasa kiongozi MSHANA jr, jamaa alivyokuwa anatumia hiyo O/D OFF muda mwingi je hakuna madhara yeyote yangeweza kutokea au kuna problem effect gani ya Technical utaipata kama utakapo tumia O/D OFF kwa muda mrefu.....?

Please ndugu Mashana jr na wengine Elimu tena kidogo.
 
Kwa uzoefu wangu kama unasafiri safari ndefu ni vizur over drive kuwa On hii itakusaidia gari kukimbia zaidi kwani ikiwa Off halaf unasafir safari ndefu utaichosha injini kwani itakuwa inadai gear nyingne wakati gearbox haijapewa nafasi ya kubadili, pia hiyo itachangia gari kutumia mafuta mengi lakn ikiwa On itarahisisha gari kukimbia zaidi na kubadili. Kumbuka unashauriwa kabla ya kuo-overtake gari unatakiwa kuiweka Off ili kuipa gari nguvu zaidi.
 
Wengi hatuelewi hizi gari za automatic. hupaswi kuhangaika na O/D, wengi wanafanya shifting kufidia mafuta lakini haina maana yoyote
 
Wanajamvi kazi na dawa ziko sokoni hizi milioni 27
milioni 12
 
Wakuu tafadhalini naomba mnisaidie hapa,hivi Tairi recommended kwa gari aina ya GX110 ni size ipi.
 
Nina swali kwenye kutumia kimiminika as coolant kwenye gari, wengine hutumia maji wengine hutumia kimiminika vinavyo uzwa madukani zenye rangi mbalimbali kama green, pink ili kupoza na kuzuia engine kupata kuta,

Swali ni je kipi ni kipi kati ya maji ama hivyo vimiminika vingine ushauri plzzz
 
Vimimika/coolant vimetiwa dawa na kuondolewa chemicals zinazoweza kuwa na madhara kwenye mfumo wa kupoza engine wakati maji ya kawaida hayajatibiwa
Lakini maji safi ya kunywa hayana shida, mabaya ni yale maji ya visima na kwenye vyanzo ambayo hayajatibiwa bado
 
Wataalam wa Diesel Engine...,naomba kuuliza Diesel Nok ni nini..?
 
Wataalam wa Diesel Engine...,naomba kuuliza Diesel Nok ni nini..?
Ni sauti mbaya ambayo huwa inatoka kwenye injini na husababishwa na injini kushindwa kuchoma dizeli vizuri inayomwagwa kwenye chemba. Hii husababishwa na nozeli kumwaga mafuta mengi au kuwa imestiki hivyo kusababisha injini kutoa mlio mbaya na pia hupelekea gari kula sana mafuta na kutoa moshi mwingi.
 
Asante mkuu.,Hapo nn kifanyike @ Itagata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…