Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Wakuu, Toyota IST ikifika speed kuanzia 80 RPM haishuki chini ya 3000RPM. Unavyozidisha speed kwenda 100kph ndivyo RPM inavyozidi kupanda. Kitaalamu ningeweza kuhisi haibadili gia zaidi ya gear no.4 . Je hii inaweza kuwa tatizo gani. Gearbox oil ishabadilishwa na service ya gearbox ilishafanyika. Gari ina nguvu ya kutosha tu ila ndiyo ikishafika hapo inakuwa kama inadai gia zaidi lakini inavuta vizuri
 
Mkuu speed 80 unatembea na RPM 3? Mbona rpm ipo juu sana kwa speed hyo?
 
Mkuu speed 80 unatembea na RPM 3? Mbona rpm ipo juu sana kwa speed hyo?
Ndio tatizo lenyewe. Ukivuka 80 lazima rpm ianze kupanda na speed. Mafundi watatu washalishika gari wanasema liko sawa. Mi sio fundi ila nasema haliko sawa. Simply ni kwamba haibadilishi gia kwenda 5. Sijawahi kuendesha IST nyingine ila sidhani kama hii ni sawa hata chembe
 
Wabobezi wa mambo ya mjini ....nawasalimu....! Naomba kufahamishwa maduka ambayo naweza kupata spare parts za hyundai tafadhalini...pia mafundi wa aina hizi za gari.

Asanteni wabobezi!!
 
Fuse kazi yake ni kulinda,(protection device) ukiunga moja kwa moja ikitokea shoti unaweza kuunguza Gari zima usikubali kaunga temporary wewe tafuta fuse urudishie kwa usalama wa Gari yako.
 
Fuse kazi yake ni kulinda,(protection device) ukiunga moja kwa moja ikitokea shoti unaweza kuunguza Gari zima usikubali kaunga temporary wewe tafuta fuse urudishie kwa usalama wa Gari yako.
Nashukuru mkuu. Ngoja nifanyie kazi ushauri wako mapema kabisa
 
Fielder ni gari ngumu na kwakuwa tayari unatumia corrola van basi fielder itakufaa sana kwa kila kitu
kaka mshana jr mambo vp kaka,naomba msaada wako ndugu, nimenunua garitoyota raum ambayo odometer inasoma 150000km kuna tatizo hapo?vipi ninaweza kwenda nayo kwa safari za mikoani?
 
kaka mshana jr mambo vp kaka,naomba msaada wako ndugu, nimenunua garitoyota raum ambayo odometer inasoma 150000km kuna tatizo hapo?vipi ninaweza kwenda nayo kwa safari za mikoani?
Sidhan kama nitatizo..ishu ni uzima wa gari....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…