Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Plug unaaza kuhisi tatizo kwenye silence mode lakini pia zikague na ukibadili hakikisha unaweka genuine...
NB: hakikisha hivi vitu Unanunua mwenyeji na kusimamia ufungaji
Unanunua mwenyeji × = Unanunua mwenyewe √ nahisi ulimaanisha hivi?
 
Hebu cheki breezer tafadhali
 
Useful Thread... Naombeni msaada, nimejaribu kutafuta majawabu kwenye hii thread sijayapata bado, gari yangu nikifika speed 100kph usukani unaanza kutetemeka, ikipungua kuja 80 hivi inatulia..., nahitaji kufanya kitu gani hapo? Aina ya gari ni carina si
 
Check wheel alignment, steering rack huenda vikawa na tatizo
 
Mkuu chek gearbox yako iyo itakuwa inatatizo mfno ingekuwa kwa gar ya manual huwa iv ukiingiaza gear na unaanza kuondoka gar huanza.kutetemeka mpk itakapoondoka huwa ni clutch plate huwa imeeisha so hupata shida kuanzisha mwendo ktk uso flywheel cz ya kuisha kwa clutch plate lkn kwa gearbox za auto jpo sina uzoefu nazo itakuwa ni gearbox..ndan kuna driven plate huwa vikipat shida huleta ttz hasa kwa upande wa gear
 
Nashukuru kwa msaada wako mshana nitafanyia kazi hilo na vipi kuhusu plag! Maana yupo jamaa yangu mmoja aliwai nieleza inawezekana pia ikawa inachangiwa na plug. Kwa engine hizi za 4E au kwa udhaefu wenu inaweza kuwa nayo ni chanzo
Mkuu chek gearbox tu..plug na gear wap na wap..
 

Check wheel alignment, steering rack huenda vikawa na tatizo
Ball joints na stabilizer links ni za kubadili
 
Nina Passo piston 3 hivi oil filter zinaingiliana na zile za piston 4
 
Sawa mkuu nitafuatilia pia na hilo.
 
Kwa automatic wanaita torque convertor, ingawa najua inafanya kazi almost the same kama clutch plates kwenye manual transmission. Mafundi wanashauri saana kuepuka kubadilisha ATF yote kama imechafuka saana, as gearbox itaanza kuleta shida, sababu ile old ATF inakua na vipande vya vyuma vinavyosaidia hiyo touque convertor kufanya kazi. Inawezekana bwana Wa nyamadyaki alibadilisha ATF pia.
 
Air clearner iko safi mkuu, alafu ATF sijabadilisha mkuu
 
Air clearner iko safi mkuu, alafu ATF sijabadilisha mkuu
Okay. Basi hapo lazima utafute fundi mzuri. Fundi wa ajabu ajabu atakuongezea tatizo, wakati kiuhalisia utakuta ni shida ndogo saana. Ukienda kwa fundi mwelezee tatizo na jaribu kumdadishi uwezo wake wa kukuelezea tatizo, kabla hajaanza kufunguafungua vitu ovyo.
 
Actually, hapo inahitaji wheel balancing as opposed to wheel alignment. Ila pia inawezekana ni dalili ya moja kati ya components za suspension zimeanza kuisha, au zimeisha. Ila wheel balancing mara nyingi inatatua hilo tatizo.
 
Yeah nitafanyia kazi ushauri wako mkuu asante sana!!
 
Huu uzi ni mrefu sana inawezekana ninalotaka kuuliza limezungumuzwa kwenye uzi huu mniwie radhi ninataka kununua injini kwa ajili ya kagari kangu kutoka kwa wauzaji wa injini zilizotumika jee ni utaratibu gani unaotumika kubadili kadi ya gari na nitajuaje kama injini hiyo haitokani na gari la wizi au gari lisilolipiwa ushuru wakati likiingizwa nchini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…