Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Ila kama kuna mtu anaweza kunisaidia naomba anipe majibu samahani kama nimemlenga yeye tu
 
Nimesoma kuanzia mwanzo mpka hapa ulipoiandika hii. Nilichojifunza ni kuwa gari likifikia km laki moja ni vzr kubadili timing belt, si busara kusubiri mpaka ikatike, madhara yake ndio kama haya, gharama zinaongezeka ktk utengenezaji as kuna hatari mifumo mingine ikaharibika.
 
Kwa diploma ya hapa hapa jukwaani ni vzr unaponunua gari kwa mtu akakupa service history yake ili kukusaidia kumaintain gari hilo. Ni vzr ikawa kwenye maandishi.

Pia wenye magari, ni vzr kuandika service history ili tunapoamua kuyauza tusiwape tabu kama hii wateja tarajali
 
habari zenu wakuu??
ipi ni gari nzuri kununua kati ya TOYOTA AURIS na TOYOTA VOLTZ?? interms of gharama ya spare na upatikanaji wake,,ubora wa gari,,fuel consumption pamoja na bei
pia naomba msaada kwa anayefahamu bei ya hizo gari hadi kufika tz pamoja na kuingia barabarani
 
Aisee nimesoma kuanzia mwanzo na sasa nimemaliza!

Nitarudia tena once my car reaches me from Japan.

Very educative! Asanteni sana wooote!!! Sijaacha comment ya mtu!

Barikiwa Mshana Jr kwa kuanzisha uzi huu murua!!
 
Wadau nina Passo piston 3 nataka kubadili engine kuweka ya piston 4. Naomba kujua gharama ya tukio zima kuanazia manunuzi kwa wanaoju. Thanks
 
Wadau nina Passo piston 3 nataka kubadili engine kuweka ya piston 4. Naomba kujua gharama ya tukio zima kuanazia manunuzi kwa wanaoju. Thanks
Is it possible kuswitch hiyo engine bila kuathiri vitu kama engine mountings? Wajuzi wa mambo njooni huku...
 
 
nina Gari aina ya Toyota spacio old model,Jana nimebadili oil ya gearbox nashangaa imebadili tabia,ili kuwa inabadili gear kwenye spidi ya 13km/h,baada ya kubadili mpka ifike 16km/hr je ni sahihi?nilistuka Na kumuuliza fundi ananambia itarudia hali yake oili bado inazunguka je ikoje Hapana Naomba msaada wenu
 
Mafundi wetu sio mahiri kabisa
 
Ilitakiwa uongeze oil na sio kubadili, mie ilinitokea kwenye prado sx, ilikuwa kubadili gear mtihani inabd ukanyage kwel, lakin baada ya kufanya safar ndef ikarudi kawaida, baada ya kuanza kudadisi shida ilikuwa kutoa oil yote. Hivyo vizur kuongeza na sio kubadiisha yote.
 
Habari za week end wandugu? Naomba kupata uzoefu kwa mwenye Nissan murano, Nimezifatilia hizi gar nimependa ukubwa wake na nafasi ilonayo ndani. Ila nilisoma uzi mmoja wa nje kuwa zina shida sana katika gear box na umeme yani haziko reliable kama prado au x trail. Mwenye uzoefu nazo tafadhali anijuze natanguliza asante, pia nasema asante kwa bwana lege alinisaidia baada ya brevis kunizimikia ghafla
 
Ziko vizuri sana kwa kila kitu ila zingatia masharti ya kuitunza... Hasa hiyo gearbox weka hydraulic stahiki usidanganywe na fundi ukaweka inayofanania utaumia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…