Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Salama wandugu!!
Ni muda sasa nimejichanga changa na nimefikia uamuzi wa kutaka kumiliki gari! Aina ya gari ninayo wiwa kumiliki ni "Nissan Dualis" shida inakuja sina taarifa za kutosha kuhusu hii gari hususan ni uimara wake, ulaji wa mafuta lakini pia vipuri vyake!!!

Mwenye uzoefu tadadhali naomba kung'amuliwa!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kuuliza.
Hivi naweza kuweka engine ya 1G-FE kweny brevis kwa gear box ile ile ya 1jz
 
Kwa ushauri wangu tafuta Toyota ila kama umeipenda hiyo fuata sana kanuni za kumiliki chombo cha moto... Ukijisomea humu utafaidika na mengi

Jr[emoji769]
 
Nataka hiyo garii niiongezee bampa Kama hiyo picha namba mojaa katika kila upandee huku moshi wanachonga za batii ambae amewai kufanya hivo anipe changamoto alio wai kutana nayo pia Kama unawajua Wana wanao weza fanya hiyo kazi kwa umakiniii nijuze hapaaa...

Sent from my Mi A2 Lite using JamiiForums mobile app
 
Nenda Instagram kuna jamaa anajiita "riderkingofsound" anatengeneza bampa za chuma vizuri kabisa inakuwa swafi sana!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa kwenye Mitsubishi mirage umedanganya aiseeee labda kama ulikua unazungumzia zile za 2010 kurudi nyuma
 
Wadau naomba msaada, nina gari aina ya Toyota Vanguard 2008, ilichemsha, nikaipeleka kwa fundi Engine akagundua Gasket ilikuwa imeisha (inachanganya maji na Oil), akabadilisha, baada ya kurudishia vifaa vyote na kuiwasha Dashboard ikawasha taa ya Check engine na 4WD, akanishauri niende nikafute kumbukumbu kwa Computer, fund akafuta taa ya Check engine tu hiyo taa ya 4WD bado inawaka,nifanyaje ili niweze kuifuta maana mwanzo ilikuwa haiwaki( nadhan inajiengage Automatic),nisamehewe kwa kutotumia maneno sahihi (sio Expert)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado kuna defect kwenye system.. Pata machine inayoweza kusoma defects zote kwa usahihi

Jr[emoji769]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…