Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Sawa mkuu ila ww huwezi kuchangia kwa ufahamu wako mkuu. Paso unazionaje mkuu?

Nisingependa kuonekana nakandia aina fulanj ya gari na kuisifu nyingine lakini kama hutajali sana achana nazo upate IST au Duet
 
Shukran mkuu kwa ist sawa ila Duet kimuonekano tu ndio inanichosha imekaa kizamani hivi. Poa ngoja nisimame hapo kwenye IST.
 
Wakuu nataka kununua Paso kwa mizunguko ya mjini tu. Je inafaa? vp uimara wake na ulaji wa mafuta?
Au ni gari ipi ndogo ambayo ni bora zaidi.
Nb. Bei iwe kama ya Paso au ikizidi basi isizidi mil 8.

Paso ni nzuri mkuu injini yake iko bye ila ukipata toleo la kwanza umeula ni imara zaidi upande wa enjini tofauti na Haya matoleo ya sasa yana shida kwenye mfumo wa umeme, kwa m 8 utapata iliyo fresh sana,go mkuu
 
Nasikia hizi GARI hazimudu safari za DSM Mbeya n kweli?
 
Labda kwakuwa engine yake ni ndogo kwa maana ya horsepower, vigari vidogo nilivyovipa salute kwa safari ndefu no Duet na IST
 
Sio kweli juzi January nimemsogezea mshkaji wangu Conwell Naweya ya mke wake Songwe border nikaiexperience ni gari imara kabisa ila sisitiza toleo la kwanza hata hapa kesi za passo sio kubwa ukilinganisha na vits au mini nyingine kama ist
 
Duh mkuu unaisifia Sana IST ngoja nijitahidi niijaribu...

Ila mda mwingine woga tu kuna jamaa kanisimulia alitoka na vits iringa mpaka DSM bila kupumzika na aliyapita mpaka mabasi
 
Ngoja nisimame kwenye ist kama anavyosema mdau ila naipenda sana paso aisee kimuonekano ipo kisasa zaidi kuliko duet.
 
Kuna mwananchi anataka kuniuzia NISSAN ELGRAND ya mwaka 2000, nipen ushauri
 
Elgrand ni gari nzuri ila huwa usipoifanyia checkup timely Huwaga inapoteza miendo kutokana na tatizo la MAF sensors kuchoka lakini vinginevyo iko bye,sema kama ni mpenzi wa hizi all purpose vans tafuta Noah au voxy zipo nyingi hapa Dar usumbufu wa Nissan ni vipuri hizo sensor zikifaga hapo kko kuzipata sometime inakuwaga issue,ila kama utaichukua karibu kwa matengenezo
 
Sio kweli juzi January nimemsogezea mshkaji wangu Conwell Naweya ya mke wake Songwe border nikaiexperience ni gari imara kabisa ila sisitiza toleo la kwanza hata hapa kesi za passo sio kubwa ukilinganisha na vits au mini nyingine kama ist

Mkuu Paso toleo la kwanza ndo ipoje hiyo?

Mkuu mfano MTU akikuwekea rav4 old model na Escudo old model uta prefer IPI? na kwanini?
 
Elgrand ni gari nzuri ila huwa usipoifanyia checkup timely Huwaga inapoteza miendo kutokana na tatizo la MAF sensors kuchoka lakini vinginevyo iko bye,sema kama ni mpenzi wa hizi all purpose vans tafuta Noah au voxy zipo nyingi hapa Dar usumbufu wa Nissan ni vipuri hizo sensor zikifaga hapo kko kuzipata sometime inakuwaga issue,ila kama utaichukua karibu kwa matengenezo

permanent solution ya hizo MAF SENSORS ni nini ?
 
Duh mkuu unaisifia Sana IST ngoja nijitahidi niijaribu...

Ila mda mwingine woga tu kuna jamaa kanisimulia alitoka na vits iringa mpaka DSM bila kupumzika na aliyapita mpaka mabasi

yes!,kama ulivyosema,mimi nina VITZ 2002 cc 1290,huwa natoka nayo Dar to Mbeya,sisimami sehemu no kuchemsha wala nn,so uoga ndio tatizo!
 
Wakuu niko na Brevis nikiwa naendesha nasikia harufu ya petrol ndani ya gari? Nini tatizo?
 
Wanandugu habari zenu,Naomba kujua Ubora na udhaifu wa Toyota Wish ya 2003?.
 
Unahitaji gari kwa ajili ya mikutano ya maalumu, kupokea wageni airport, safari za kitalii au mafunzo, harusi, misiba...... Wasiliana nami John Amon 0712999090/0763999090 (Junior de Transporter)
 
Attachments

  • 1426917954848.jpg
    1426917954848.jpg
    55.7 KB · Views: 354
Habari ndugu zangu...
Nawpongeza sana wana jf kwani huwa najifunza mengi kwenye hili jamvi. leo ningependa ushauri kuhusu gari ile niweze kufanya maamuzi sahihi. ninahitaji toyota saloon na kwa mapenzi yangu mimi ningepenga gari ambayo inastahimili barabara ya vumbi na ulaji wa mafuta mzuri , pia iwe ya bei nafuu ya kuagiza kutoka nje. binafsi ningependa CORONA PREMIO 2000, COROLLA 2000.

Naomba ushauri
1.nichukue ipi? au nichukue tofauti na aina hizo za gari?
2.pia ningependa kujua ni aina gani ya ingini ni bora kwa mazingira niliyotaja??.........
3.pia kwa wazoefu wa kuagiza magari kuagiza aina hizi za gari za mwaka 2000 inaweza kugharimu sh. ngapi mpaka gari inaingia barabarani???

Asante sana..
 
Back
Top Bottom