Sembeta jr
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 805
- 367
hapa nahusika sana hapa.....
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumekuwa na mada nyingi kuhusu mambo yote yahusuyo magari, nikaona basi na sisi tuwe na Uzi huu ambapo habari zote zihusuzo magari kuanzia kuchagua, kuagiza, kuuza, kubadili nyaraka, matengenezo utunzaji na kadhalika.
Watu wengi wametapeliwa kwenye mauzo na manunuzi, kwenye nyaraka, kwenye vipuri kwenye matengenezo na hata matumizi.
Kwa Uzi huu basi kila mwenye ujuzi, uzoefu, ushauri au mwenye maswali na tatizo lolote linalohusiana na magari hapa ndio pawe uwanja wake
Karibuni sana
View attachment 225786
Mkuu mshana jr nashukuru sana kwa thread yako hii, kuna vitu vimenisaidia. Mimi naomba tu kujua mafundi wazuri, kwa service ya gari hizi Raum new model na Toyota Voltz. Kwa Dar, fundi wa mwanzo niliyekuwa naye now hayupo.
Mkuu Mshana Jr gari yangu ni Nisan Xtrail inawaka taa ya check engine. Na wakati naendesha wakati mwingine inakosa nguvu kabisa na engine rotation kuwa kubwa. Baada ya diagnosis wanasema solenaid valve ya gear box imekufa. Hiki ni kitu gani na kinapatikana wapi kwa bei gani? Natanguliza shukrani
wakuu nielewesheni jinsi ya kutumia auto/manual transimission system kwenye Toyota Mark x, pia kwenye gear leaver kuna D na S + na - nini kazi zake, D ni drive ila S+ na S- sizielewi, nawasilisha.
Kwenye Mark X engage manual transmission then button zagear zipo chini ya steering, lakini tumia tu auto ndio kisasa S+ na S- nafikiri ni D1 na D2, D1 ya mwinuko na tifutifu D2 utelezi
Hapana mimi sio fundi, runx si ndio kizazi cha ist, Allex, duet nk? Ni gari ambazo hazitaki shida wala mikikimikiki, kwa ushauri nunua gari yeyote kizazi cha corolla100, 110 au hata GX 100 kavu! GX vvti itakutesa
HAKI ZA DEREVA ANAPOKAMATWA NA TRAFFIC
- Trafiki hana idhini ya kukulazimisha kumkabidhi leseni yako
-Akikukuta na kosa na kukuandikia notification na ukalipa ni lazima akupe risiti ya serikali
-Hana haki ya kukuulizia kuhusu road licence hiyo ni kazi ya TRA kwakuwa siku utakapoenda kulipa utalipia na faini
-kama huna leseni una haki kisheria kuipeleka kituoni ndani ya Massa 72 ya kazi tangu ulipotakiwa kufanya hivyo
-Akikusimamisha una haki ya kusimama sehemu ile ambayo utaona ni salama na si lazima usimame anapotaka yeye
- Sio kila kosa ni la kuadhibiwa, mengine ya kuonywa au kuelimishwa
Hapana mimi sio fundi, runx si ndio kizazi cha ist, Allex, duet nk? Ni gari ambazo hazitaki shida wala mikikimikiki, kwa ushauri nunua gari yeyote kizazi cha corolla100, 110 au hata GX 100 kavu! GX vvti itakutesa
Hivi kwa nini House Girl kuachiwa mtoto sio ishu lakini huwezi kusikia House girl kaachiwa gari?
Sehemu za uhakika za kufanyia service ni kwenye petrol station zinazotoa hiyo huduma, inaweza kuwa a bit expensive lakini ni afadhali kuliko
Mkuu mshana Jr kwanza nakupongeza kwa hii brilliant idea ya kuanzisha huu Uzi..! Sasa tafadhali tuelimishe kuhusu makosa yanayostahili faini na yale yanayostahili kuonywa au kuelimishwa, pia na vifungu vyake vya sheria.
Jamani namtafuta fundi wa Fuel System ya SUBARU FORESTER,nikikanyaga accelerator hadi mwisho kwennye Mwendo inaanza miss,inajivuta vuta.Ni plugs?na inawaka CHECK ENGINE.Nipo DAR