Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mnyama huyo usimwache tatizo lake ambalo laweza kuwa sio tatizo iko chini sana kwahiyo rough road inabidi kuwa mpole otherwise ni gari ya kijamaaa sehemu kubwa na ubepari kidogo yaani 75/25%

Thanks,je TI carina?looking for gari ngumu na imara had toyota passo ni majanga
 

MshanaJr ubarikiwe kwa taarifa hii,
Jamaa yangu kapigwa kwa utaratibu huu ulioleza ,yeye ndio anaonekana mwizi baada ya TRA kumkamata kumbe mchongo wote umefanywa na muuzaji feki (ambaye ndiye mwizi)aliyeaminiwa na mmiliki halali wa gari,
Na epuka sana kununua gari ambayo bei yake ni rahisi sana tofauti na bei ya soko ya wakati huo, jamaa yangu aliponunua gari hiyo niliona kapatia kweli, kumbe kapatikana mazima
Asante mshana
 
Habari za asubuhi wanaJF,
Naomba nielekezwe utaratibu wa kufuata baada ya kudilisha mashine ya gari.
Mathalani baada ya kufunga mashine ya Toyota katika Escudo nawajibika chochote labda TRA?polisi? au ni mwendo mdundo?
 
Habari za asubuhi wanaJF,
Naomba nielekezwe utaratibu wa kufuata baada ya kudilisha mashine ya gari.
Mathalani baada ya kufunga mashine ya Toyota katika Escudo nawajibika chochote labda TRA?polisi? au ni mwendo mdundo?

Kapate kibali polisi kisha nenda TRA
 
Duu umeponea tundu LA sindano kupigwa hizo case zipo nyingi sana pale TRA makao makuu ghorofa ya nne chumba cha kwanza kushoto ukitoka kwenye lift, pameandikwa Investigation, kwenye post za mwanzo angalia nimeizungumzia hiyo kitu kwa undani

Nakubaliana sana na wewe broo... Ukitaka kununua gari kwa mtu hakikisha mnaenda TRA kwanza la sivyo kuna kulia. Mi niliwahi kununua gari mwaka 2012 nikapewa kadi na document zote muhim , tatizo likaja wakato road licence imeisha nataka kulipia tena nikakuta kumbe aliyekuwa na gari alienda sijui wap akachukua Road lisence fake na stika kabisa ikawa inaonyesha haijalipiwa muda mrefu. Kwanza ikabidi nilipe karibu laki tisa pamoja na faini. Pili TRA wakataka niwapeleke kwa aliyeniuzia gari ili wamkamate kwa kosa la kufoji. Nilivyoenda kwa aliyeniuzia akaniambia huo ni msala wako ukinisanua nakumaliza(machalii wa Arusha tena) nikawahonga TRA laki tatu wapotezee. Kwa kweli sishauri mtu atoe hela mfukoni kununua gari bila kupita TRA na pale TRA hawatakuchaji kitu.

Mghosi
 
Mshana jr mimi nataka kununua gx 100 cresta wiki tatu zijazo,hilo nalo vp?

Mnyama huyo usimwache tatizo lake ambalo laweza kuwa sio tatizo iko chini sana kwahiyo rough road inabidi kuwa mpole otherwise ni gari ya kijamaaa sehemu kubwa na ubepari kidogo yaani 75/25%

Kweli hiyo gariGX 100 ni mnyama hatari sana. Tatizo ni kuwa ipo chini,so inasumbua kunako rough road. Ila hiyo isikutishe mkuu,run for it.
 

Jaribu hii technique! Taa ikiwaka tu nenda station jaza full tank (hata km ni town trips). Tumia mpk iwake tena weka full tank, hiyo mm inanisaidia sana kuepuka kuua pump

Wandungu ahsanteni kwa maelezo mazuri yaliyonyooka. Basi mimi hapo nilikuwa najuaga labda kuna some general formula kuwa some % ya tank huwa reserved kwa magari yote. Ila nimefurahi kuwa whatever taa itakavyowaka una uwezo wa kuchanja mbuga for 30km ahead mpk gari kuzima. Mana mm kichwa huwaga kinapata moto pale taa ya mafuta inapoanza kuwaka,kublink. Ila cjawahi iacha ing'ang'anie kuwaka.
 

asante sana kwa taarifa hio nzuri
 

Thanks
 
Nimesoma kitu hapa nadhani sijaelewa vizuri, ina maana mtu akibadilisha engine ya gari akaweka ya aina ya gari ile ile anatakiwa kutoa ripoti polisi na TRA?
 
Nimesoma kitu hapa nadhani sijaelewa vizuri, ina maana mtu akibadilisha engine ya gari akaweka ya aina ya gari ile ile anatakiwa kutoa ripoti polisi na TRA?

Ndio kwakuwa makadirio ya road licence hutumia vigezo vya ukubwa/ uwezo wa engine, lakini pia hata unapobadili rangi ya gari inabidi TRA na JESHI LA POLISI wajulishwe, update ruhusa/kibali cha kubadili rangi na nafikiri na kadi mpya
 
Wakuu naomba kujulishwa hivi ile hydraulic ya kwenye gear box za automatic huwa inabadilishwa baada ya muda gani au baada ya kms ngapi?Mm nimetumia gari yangu sasa ni miezi 7 tokea nitoe bandarini nimekuwa nabadilisha engene oil peke yake.Nimeshatemebea kama 10,000kms kwa huo muda.Ila nikiicheki hiyo hydraulic ya gear box naona bado ipo poa tuu na gear zinabadilika bila shida yoyote.Gari yangu ni premio new model ya 2003.
 
Ndio kwakuwa makadirio ya road licence hutumia vigezo vya ukubwa/ uwezo wa engine, lakini pia hata unapobadili rangi ya gari inabidi TRA na JESHI LA POLISI wajulishwe, update ruhusa/kibali cha kubadili rangi na nafikiri na kadi mpya

Kabisa mkuu...lazima afanye ivo
 

Ile haiishi bali huchafuka na kupoteza ubora, unatakiwa ubadili haraka unaua gearbox
 
MANI ebu msikilize huyu jamaa aseee, DAH.

Aged 11 years and more
Current Retail Selling Price 30,975
Depreciation 80%
Freight
Customs value 3,200
FOB Value 3,200
Import Duty 25% 800
Excise Base for vehicle aged more than 10 years 1,200
Excise Base 4,000
Excise Duty 5% 200
VAT Base 5,400
VAT 18% 972
Total Taxes 3,172
Total Taxes in TSHs 5,395,572

Mkuu asikutie presha hesabu ni hiyo hapo juu ukiongeza na usajili na cpf haitazidi 6ml kwa hiyo ukiwa na 7 ml gari liko nje all inclusive.
 
Last edited by a moderator:
Mmmh!kuna fundi nilishamskia akisema gearbox oil huwa haibadilishwi coz ipo unique na ukibadili hupati iliyo bora kama hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…