Inategemea gari na gari na ukubwa wa tank! Kwa mfano reserve ya Duet haiwezi kuwa reserve ya Mark X au Brevis! Magari yenye engine kubwa huwa na tank kubwa na automatically reserve pia huwa kubwa
Vyovyote viwavyo taa ikishawaka moja kwa moja bila kuzima una uwezo wa kwenda km 30 ndio izime kabisa, kwahiyo hapo unaweza kufanya mahesabu kulingana na ulaji wa mafuta wa gari lako
MADHARA YA KUTEMBELEA EMPTY TANK/MAFUTA KIDOGO
kwenye tank la gari kuna pump inayochuja na kusukukuma mafuta yaende kwenye mfumo wa engine, ile pump hulala kwenye sakafu ya tank na huinuka kadiri mafuta yanavyokuwa mengi (ina boya)
Mafuta ambayo hayajadhibitiwa vema huingia na chembechembe za michanga, ambazo hutuwama chini ya tank, hivyo ukitembea mafuta kidogo kila wakati pump badala ya kuvuta mafuta inavuta uchafu na hatimaye kuziba na kushindwa kupeleka kiwango cha kutosha kwenye mfumo wa engine
Haya madhara si kitu cha maramoja bali huja taratibu mno, kwahiyo kwa USHAURI
-Epuka mafuta ya videbe/drip
-Epuka kuendesha gari mara kwa mara likiwa halina mafuta ya kutosha
-Epuka kuweka mafuta kwenye vituo vya kienyeji