Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Aisee N'yadikwa kuna kalamu, note book, kigogo maji safi, first aid kit kuna wakati vinahitajika katika mazingira usiyotegemea
 
Last edited by a moderator:

Mkuu nikuweke wazi kidogo,terios kid na daihatsu terios zote ni jamii ya Daihatsu ambayo iko chini ya toyota,terios kid ina cc 660 ilhali daihatsu terios ina cc 1300 toyota wana toleo lao linalofanana na daihatsu terios linaloenda kwa jina la Toyota Cami,tofauti ni majina tu ila cc ni sawa 1300,nawasilisha.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu mi ninayo hii gari,ni ngumu asikueleze mtu,nna mwaka wa nne sasa nimetumia ya kwanza nikavuliwa na mtu nikaorder nyingine japan,nimeenda nayo pasaka moshi km 500 kama kumsukuma mlevi ukiwa na buku 2 unaingia sheli,hutajuta nunua faster
 
Hii tabia ya kuzima na kuwasha gari pindi uwapo ktk foleni " hasa hizi za jijini Dar" kwa minajiri ya kuokoa mafuta ya gari. Je ni kweli inasaidia kuokoa mafuta km inavyodhaniwa.?!
 
Hii tabia ya kuzima na kuwasha gari pindi uwapo ktk foleni " hasa hizi za jijini Dar" kwa minajiri ya kuokoa mafuta ya gari. Je ni kweli inasaidia kuokoa mafuta km inavyodhaniwa.?!

Ndio inasaidia na ndio maana magari mengi ya kuanzia 2012 yana kitu wanaita stop start system kama sijakosea
 
Ndio inasaidia na ndio maana magari mengi ya kuanzia 2012 yana kitu wanaita stop start system kama sijakosea

Ahsante mkuu. Je na hiko kitendo cha washa zima washa zima ya mara kwa mara kwa magari ambayo hayana huo mfumo wa stop start,haiwezi kuleta matatizo ktk starter ya gari.?!
 
Ahsante mkuu. Je na hiko kitendo cha washa zima washa zima ya mara kwa mara kwa magari ambayo hayana huo mfumo wa stop start,haiwezi kuleta matatizo ktk starter ya gari.?!

Hapo itategemea na ubora wa injin kama injin hairespond haraka yaan inacherewa kuwaka mpk ushikilie switch kwa mda mrefu ndio iwake sikushauri
 
Ndio inasaidia na ndio maana magari mengi ya kuanzia 2012 yana kitu wanaita stop start system kama sijakosea

Hapo itategemea na ubora wa injin kama injin hairespond haraka yaan inacherewa kuwaka mpk ushikilie switch kwa mda mrefu ndio iwake sikushauri

Hii zima washa si kitu cha kitaalam hata kidogo na sidhani kama hata hiyo spot starter hayo ndio malengo yake
Kuna mifumo mingi kwenye gari inayofanya kazi tofauti, hivyo tabia ya washa zima huathiri hii mifumo kwa njia moja au nyingine
Mfano uko kwenye foleni umewasha A/C, huu ni mfumo unaojitegemea kwahiyo ile zima washa zima washa huathiri sana compressor, evaporator na gas bottle, mfumo wa AC ya gari unafanana na friji, compressor ina intervals za kuwaka na kuzima hivyo unapoikatisha kila mara hufupisha lifespan ya mfumo mzima wa AC kama si kuuharibu
Kuna mfumo wa radio na mziki nao unaweza kuathirika kutokana na ile zima washa, kuna mfumo wa taa, fuses, na sensors mbalimbali...!

Binafsi siafiki na sishauri jamani, starter si kitu cha mchezo umeme unaotoka pale ukikupiga short unapoteza maisha, sasa kila mara kurestart current kubwa kama ile iingie kwenye mzunguko na kabla haijatulia unarudia tena ni hatari hata kwa maisha ya battery
Kwahiyo kuna madhara mengi kwenye zima washa kuliko faida, na ndio maana hushauriwa kuzima mifumo yote kwenye gari kabla hujastart
 
Duh. Kwa huu ufafanuzi kuanzia leo naacha kabisa hii tabia ya zima washa nikiwa ktk foleni yoyote ile.
 
Duh. Kwa huu ufafanuzi kuanzia leo naacha kabisa hii tabia ya zima washa nikiwa ktk foleni yoyote ile.

Unajua pia inaathiri hata pump ya mafuta kwenye tank!? Gari inapokuwa silencer mtiririko wa mafuta unakuwa unaenda kwa utaratibu wake uliokubalika, sasa hii zima washa kila muda husababisha mafuta kurudi kwenye tank na kuingia kwenye mzunguko tena na kabla haijatulia, unazima mafuta yanarudi tena, mara unawasha aisee ni usumbufu wa hali ya juu
Lakini pia kuna kiwango cha mafuta kinapotea bila kujua kwenye hiyo zima washa...! Unapowasha gari silencer huwa juu na huendelea kushuka kadiri mafuta yanavyoingia kwenye mzunguko, na silencer ikiwa juu ulaji wa mafuta huongezeka hivyo hata huu utaratibu wa zima Sasha unakula mafuta
 
Unajua kupitia hii mada maalum ya magari humu Jf,nimeweza kujua mambo mapya kuhusiana na masuala mazima ya magari na kuboresha niliyokuwa nayajua awali. Bravo bravo Mshana Jr,N'yadikwa,dony2680 na wachangiaji wote kwa ujumla kwa kushare ideas kiroho safi kwa kadiri ya uelewa wao.
 
Hapo kwenye kuonywa, uonywe mara ngapi ili ustahili kipigwa faini?
 
Hapo kwenye kuonywa, uonywe mara ngapi ili ustahili kipigwa faini?

Kwa nchi yetu hatuna utaratibu wa kutunza kumbukumbu za makosa ya mtu, lakini hivi trafiki akikukamata mara ya pili kwa kosa lilelile, atakuonya tena kweli?
 
Kwa nchi yetu hatuna utaratibu wa kutunza kumbukumbu za makosa ya mtu, lakini hivi trafiki akikukamata mara ya pili kwa kosa lilelile, atakuonya tena kweli?

Uko sawa mkuu , kuna issue kama kioo cha mbele kuwa na ufa. Matrafiki hutoza faini, na hata kama wa kwanza akikuonya anayefuatia usipompa kitu kidogo, basi faini hukwepi.
You are very resourceful mkuu. Thanks!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…