Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Utavihitaji vitu hivi wakati utakapotakiwa kusafiri zaidi ya km 500,,,Hakikisha unavyo garini wakati unapoanza safari:-
1.Tochi
2.Kisu
3.Waya mita mbili.
4.Tools kit
5.Jeki
6. Jerry can 5lts
7.Kamba
8.Adhesive glue
9.Mwamvuli
10. Silaha eg kisu,bunduki,jambia,...UNAWEZA KUONGEZA VINGINE...
Ni aina moja ila wametofautisha majina tu,kwamba moja ni Terrios Kid nyingine Terrios Cami ila ziko sawa na spare zake zipo but bei zake ni kubwa kiasi chake,yaani tuseme service atakayofanya mtu mwenye Terrios kwa ajili ya mizunguko ya kawaida mjini cost yake inalingana(inaweza kupita) na service atakayofanya mtu mwenye Spacio au Corona Premio kwa ajili ya long safari. the boss
Viashiria ni vingi kuchoka kwa break pads, ball joints lakini pia kuna wakati ni tatizo la alignment na balancing ya front tyres(I may be corrected)
kwa misele ya mjini ni gari nzuri ingawa nafasi kwa ndani ni ndogo.Parking mjini haikutesi..pia kwa upande wa barabara za kitanganyika spidi isizidi 20km/h otherwise itakutoa barabarani haina uwezo wa kuhimili bararbara zenye mashimo mashimo.Upande wa fuel consumption ni mzuri hasa kwa barabara za mjini nafikiri ni 1lt/20 km plus.Kama kwa kupigia lesi mjini si tatizo lakini kama ni gari ya kazi nasema hapo bado.Mie nipo kanda ya ziwa spare za suzuki bado ni changamoto lazima utembee na kipuri kilichopata shida madukani .Sasa weka nia kuu ya kuitumia gari yako ni ipi?
pamoja mkuuBarikiwa sana kiongozi nashkuru mno kwa mchango wako mkuu.
Hii tabia ya kuzima na kuwasha gari pindi uwapo ktk foleni " hasa hizi za jijini Dar" kwa minajiri ya kuokoa mafuta ya gari. Je ni kweli inasaidia kuokoa mafuta km inavyodhaniwa.?!
Ndio inasaidia na ndio maana magari mengi ya kuanzia 2012 yana kitu wanaita stop start system kama sijakosea
Ahsante mkuu. Je na hiko kitendo cha washa zima washa zima ya mara kwa mara kwa magari ambayo hayana huo mfumo wa stop start,haiwezi kuleta matatizo ktk starter ya gari.?!
Hii tabia ya kuzima na kuwasha gari pindi uwapo ktk foleni " hasa hizi za jijini Dar" kwa minajiri ya kuokoa mafuta ya gari. Je ni kweli inasaidia kuokoa mafuta km inavyodhaniwa.?!
Ndio inasaidia na ndio maana magari mengi ya kuanzia 2012 yana kitu wanaita stop start system kama sijakosea
Hapo itategemea na ubora wa injin kama injin hairespond haraka yaan inacherewa kuwaka mpk ushikilie switch kwa mda mrefu ndio iwake sikushauri
Hii zima washa si kitu cha kitaalam hata kidogo na sidhani kama hata hiyo spot starter hayo ndio malengo yake
Kuna mifumo mingi kwenye gari inayofanya kazi tofauti, hivyo tabia ya washa zima huathiri hii mifumo kwa njia moja au nyingine
Mfano uko kwenye foleni umewasha A/C, huu ni mfumo unaojitegemea kwahiyo ile zima washa zima washa huathiri sana compressor, evaporator na gas bottle, mfumo wa AC ya gari unafanana na friji, compressor ina intervals za kuwaka na kuzima hivyo unapoikatisha kila mara hufupisha lifespan ya mfumo mzima wa AC kama si kuuharibu
Kuna mfumo wa radio na mziki nao unaweza kuathirika kutokana na ile zima washa, kuna mfumo wa taa, fuses, na sensors mbalimbali...!
Binafsi siafiki na sishauri jamani, starter si kitu cha mchezo umeme unaotoka pale ukikupiga short unapoteza maisha, sasa kila mara kurestart current kubwa kama ile iingie kwenye mzunguko na kabla haijatulia unarudia tena ni hatari hata kwa maisha ya battery
Kwahiyo kuna madhara mengi kwenye zima washa kuliko faida, na ndio maana hushauri kuzima mifumo yote kwenye gari kabla hujastart
Duh. Kwa huu ufafanuzi kuanzia leo naacha kabisa hii tabia ya zima washa nikiwa ktk foleni yoyote ile.
hapa nahusika sana hapa.....
Makosa yanayostahili faini ya moja kwa moja ni pamoja na kuendesha mwendo kupita spidi iliyowekwa, kuendesha gari bila leseni, gari kukosa break fire extinguisher, bima, indicators, triangles, ulevi nk nk! makosa yapaswayo kuonywa kutofunga mkanda,kuwa na shida na matatizo madogomadogo kwenye gari kama bulb kuungua vioo kupasuka nk nk
Hapo kwenye kuonywa, uonywe mara ngapi ili ustahili kipigwa faini?
Kwa nchi yetu hatuna utaratibu wa kutunza kumbukumbu za makosa ya mtu, lakini hivi trafiki akikukamata mara ya pili kwa kosa lilelile, atakuonya tena kweli?
South zipo za kumwaga utagharamia uchakavu lakini