Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Safi sana Mshana kwa huu uzi! Naombeni ushauri nataka kununua BMW 3 series ya mwaka 2000! naombeni ushauri wa kitaalam uimara wake na engine ipi nzuri ya hiyo gari maana nimepitia showroom mbalimbali nimeona zinatofautiana engine! Spear zake pia vipi hapa bongo? Ubaya wa hizo gari pia ukoje? Ulaji mafuta vipi?

Suzuki Aerio na Mazda demio station wagon nazo vipi?

Naomba kuwakilisha
 
cc: RRONDO, N'yadikwa na Kaizer
 
Last edited by a moderator:
Wakuu huu uzi mzr unatusaidia wengi sana. Tatizo langu ni kwamba kuna ndugu yangu amenunua NISSAN MURANO iko bomba sana sasa ina tatizo moja ambalo yeye hakuligundua nimekuja kung'amua mie the baada ya kuuzima gari kae niitest. Iko na tatizo ya front suspensions (shock-up) ameenda kuuliza Serengeti kariakoo kaambiwa 700,000 new brand. Ameona maji marefu akaenda used ilala kakosa aina ya gari lake. Sasa je anaweza pata wapi kene bei nafuu? Je huko Nairobi nilikosikia spare zipo anaweza pata new brand kwa bei gani? Halafu service special kwa Nissan ni garage gani kwa hapa Dar? Najua gari zingine zinahitaji matunzo mazuri ndo zinadumu otherwise unaweza kuichukia gari. Pia hata kubadili badili mafundi napo co vzr ko nataka ndg yangu nimuelekeze awe anaenda kufany service sehem moja kila wakat. Mkuu #Mshana_jr_na_wengineo okoeni jahazi!
 
Ingia anuani yoyote ya Nairobi utasaidika mfano www.nissannairobi.com nk, service nenda kwenye engen puma total nk wako byeee
 
Mkuu izo naona zipo poa tu watu kibao wanazo na spare zipo. Gari flan ya heshma nadhani RRONDO ananuzoefu nayo ashawahi kuimiliki.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu izo naona zipo poa tu watu kibao wanazo na spare zipo. Gari flan ya heshma nadhani RRONDO ananuzoefu nayo ashawahi kuimiliki.

Kuna mtu kaulizia hii gari juzi juzi,nimeelezea hadi bei ya filter. Ndio maana tukaomba jukwaa special ambamo kutakuwa na thread za individual cars! Sasa hivi watu hata kumi washaulizia hii gari na kupewa maelezo.
 
Halafu service special kwa Nissan ni garage gani kwa hapa Dar? Najua gari zingine zinahitaji matunzo mazuri ndo zinadumu otherwise unaweza kuichukia gari.

Kwa garage special kwa Nissan kwa hapa dar nenda maduka mawili kule chang'ombe temeke. Ipo eneo la viwanda chang'ombe.
 
RRONDO nisaidie best yangu kupata hiyo threat uliyoandika kama ulivyoeleza hadi bei ya filter au unitag niweze kuisoma msaada wako ni mkubwa sana kwangu!:confused2:
 
Kwa garage special kwa Nissan kwa hapa dar nenda maduka mawili kule chang'ombe temeke. Ipo eneo la viwanda chang'ombe.

#Ndesalee : nashukuru mkuu kwa msaada zaidi. Chang'ombe maduka mawili nakujua sema lada special area ndo itakuwa ngumu. Lakini kwa maelezo hayo najua nikifika huko nitajua zaidI kwa kuulizia hata watu wa area ile.
 
Kuna mtu kaulizia hii gari juzi juzi,nimeelezea hadi bei ya filter. Ndio maana tukaomba jukwaa special ambamo kutakuwa na thread za individual cars! Sasa hivi watu hata kumi washaulizia hii gari na kupewa maelezo.

Prondo tusaidie mkuu hizi info za bmw 3 series au kama vp tuwekee link tuweze kusoma maelezo yake sorry kwa kukuuliza kitu ulichokwisha jibu
 
Jamani naombeni kuuliza,kuna magari nmekutana vibao vyake vya namba vinasomeka kama: LORD MAYOR na nyingine: T JSB 108,zina maanisha nini?
 
Jamani naombeni kuuliza,kuna magari nmekutana vibao vyake vya namba vinasomeka kama: LORD MAYOR na nyingine: T JSB 108,zina maanisha nini?
Ukiwa na Millioni tano nafikiri unasajili na wewe gari lenye plate no.unayoitaka iwe jina lako au mtaa wako au mke wako yaani upendavyo
 
Ukiwa na Millioni tano nafikiri unasajili na wewe gari lenye plate no.unayoitaka iwe jina lako au mtaa wako au mke wako yaani upendavyo

Hayo ya m5 ni wale wanaoandika majina yao MBALAMWEZI,CHOGONDINGO halafu mara nyingi yanakuwa magari ya maana!sasa hayo nlotaja mfano T JSB ni toyota spacio
 
Hayo ya m5 ni wale wanaoandika majina yao MBALAMWEZI,CHOGONDINGO halafu mara nyingi yanakuwa magari ya maana!sasa hayo nlotaja mfano T JSB ni toyota spacio

Mkuu kwani Spacio sio gari ya maana?
 
Mkuu kwani Spacio sio gari ya maana?

Sorry mkuu kama nimekukwaza kwa kuongea tungo tata!!nlimaanisha magari ambayo bei ghali wengi hatuwezi kumudu kuyanunua na kuhakikisha tunayahudumia!
 
Mkuu kwani Spacio sio gari ya maana?
Huo ndo ukweli ingawa ni Mchungu. Watu wakisema jamani wenye magari ya maana wayatoe..na wewe utatoka na Spacio yako?
Na wenye Vogue, Mercedes and other relating brands wafanyaje?hauna gari una chombo cha usafiri kaka
 
Duh kumbe kuna vogue zimewekwa engine za toyota?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…