Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Hapo nimekusoma jr.ila ni kwann haifanyi kazi vzr kwenye barabara ya vumbi? na hasa ukikanyaga brake ya ghafla.
 
Umetudanganya maana ya ABS na wewe.
ABS (Anti lock brake system)

Hapa hatubishani bali tunashare maarifa! Nimeongea ninachokifahamu ukitumia neno kudanganya si sahihi! Nidanganye ili iweje Habdavi?
Unaweza kuelezea zaidi kuhusu hiyo Anti lock break system kwa manufaa ya wote
 
Last edited by a moderator:
Hapo nimekusoma jr.ila ni kwann haifanyi kazi vzr kwenye barabara ya vumbi? na hasa ukikanyaga brake ya ghafla.

ABS inapokuwa katika ubora wake hufanya kazi popote! Lakini hilo la barabara ya vumbi kutofanya Nazi vizuri linahitaji utafiti zaidi kuliko majibu ya kubahatisha
 
Thanx @----- for ur efforts...! Many can learn from ur post n benefit
NB: badili username best

Nafikiri liko kwenye kati ya yale maneno ambayo yamewekwa kwenye auto ignore
 
Vipi kuhusu gari aina ya Dahatsu Terrios au Toyota CAMI
kwenye Bei, vipuri, imara, utumiaji mafuta nk.

Ninavutiwa nayo kwa sababu natafuta gari ndogo kwa mizunguko ya mjini lakini yenye uvungu mkubwa chini kwa kuwa ninapita pia kwenye rough road zenye mashimo mashimo.

Mkuu Zanzibar Asp ..mimi ninavyosikia kutoka kwa wataalamu wa magari ..wanasema gari zuri kati ya hizo gari ndogo za juu ulizotaja ni Toyota Cami..ila ununue engine K3 ndio inakula mafuta kidogo sawa na passo.. mm binafsi natumia Toyota Cami ila bado sijaichunguza vizuri maana bado iko ktk hali zuri nilinunua kutoka yard miezi 6 iliyopita..binafsi nimefurahia hizi gari kutokana na kuhimili maeneo ninayoishi .maana barabara ni mbovu na wakati wa mvua inakuwa mbaya zaidi..ila baadaya kununua hii gari ninapita sehemu yoyote bila shida ..hata kwenye vilima mitelezo mm naswagatu kwa kwenda mbele..nakumbuka siku moja nilipitia njia ya vingunguti kutokea Tabata Barakuda..kama unalifahamu eneo lile kukiwa na mvua kunakuwa na matope pamoja na utelezi pia kuna kamlima flani hivi kanasumbua sana..nikakuta Rav 4 new model imekwama na inateleza ikijaribu kupanda kimlina..ila mimi na Cami yangu nilipapita kama mchezo wa kuigiza vile..kwa hiyo hivi vigari vina nguvu na ni imara kiasi flani.

Ila Mkuu kama mfuko unarusu nunua new model ya hizi Cami ..yaani Toyota Rush..ni vigari vizuri mno ila bei yake kidogo ina range kwenye M 20 na ushee hivi...kwa Toyota Cami ktk Mayard hapo Dar bei yake ni kati ya M 10 na 12...au Hata mpaka M 15...
 
Nimeona gari imeandikwa maneno haya kwenye batoni karibu na gear lever ECT PWR na ECT SNOW na ukibonyeza yanaonekana kwenye dash board ni maana na kazi yake?
 
Nimeona gari imeandikwa maneno haya kwenye batoni karibu na gear lever ECT PWR na ECT SNOW na ukibonyeza yanaonekana kwenye dash board ni maana na kazi yake?
Kwanza nianze na hiyo ECT kirefu chake ni Electronically Controlled Transmission, kwa urahisi ni batani inayokuwezesha kulipa gari udhibiti binafsi wakati linapopita maeneo yenye changamoto kwake Mf.mlima, mteremko, barafu, tope zito nk ECT kile inafanya ni kupunguza mabadiliko ya Mara kwa Mara ya gia kwa mfano ukiibonyeza hiyo batani ktk PWR mode wakati unapanda mlima automatically gia za kupanda mlima aghlabu 1,2au3 zitakuwa zikijiseti kulingana na ukubwa wa mlima ukiweka batani ktk PWR mafuta zaidi yanatumika Ila injini nguvu yake inaongezeka,haishauriwi uiweke on kwenye normal town cruises, wenzetu kwenye barafu Kama huko Ulaya wanatumia hiyo batani Kama special effect kuwezesha gari kuhimili uterezi kwa sababu ECT huwezesha ongezeko la nguvu ya injini kwa kushabihisha na mzunguko wa injini kwa dkk-rpm, hapa Tanzania hiyo special effect inapatikana zaidi ktk Lexus,Escudos,baadhi ya corolla na mengineyo.

Kwa mukhtasari ECT batani husaidia gari kutumia low gear kwa muda mrefu.
 
Lakini pia Kama breki zako wasiwasi ECT itakusaidia Kama engine stopper ingawa haifanyi kwa ufanisi sana Kama gia halisi kwenye manual ikitumiwa kulipa uzito gari lenye ukimeo linaloshuka mlima kitonga au kawetere😀
 
Vipi kuhusu hizi probox jamani, naziona tu barabarani na watu wanazisifia kuwa ni nzuri. Vipi zinahimili barabara zetu hizi rough na fuel consumption ikoje?
 
Wakuu napenda kufaham hiv ac kwenye magari nikweli zinaongeza fuel cunsuption?
 
wakuu mimi swala langu ni kuhusu rotary engines. Hasa kwenye gari aina ya mazda rx8 inatumia mfumo huu wa engine.. Ni engine isiyotumia pistons ila inatumia rotors.

Kwa mwenye uzoefu wa aina hii ya engines, spare zake upatikanaji wake ukoje, matatizo ya engines hizi ni yapi

kaka hizo engine ni bomba sana.. Nikama za ndege. Engene ya ndege hai2mii piston hasa hizi kubwa..kitaalamu hiz za rotor ni nzuri motion haupotei,even gearbox unatumia botorn.
 
Back
Top Bottom