kiipwi cha ngoghwe sidhani kama zipo Altezza 4S na kama zipo ulaji wake waweza uwe hautofautiani sana na 6S
ANGALIZO:
Unaweza ukawa na gari 6S na ikatumia mafuta vizuri zaidi kuliko mwenye 4S! Hii ni kutokana na uendeshaji, kwa mfano unatoka shekilango kuelekea mjini unajua kabisa ukifika big brother lazima upunguze mwendo lakini mtu anaivuta mpaka spidi 80 halafu akifika big anapunguza mpaka spidi 30 then anavuta tena akifika tiptop anapunguza tena huo ni uharibifu was mafuta, kwa jinsi hiyo utakuwa unapoteza mafuta mengi bila sababu
Vilevile hata safari ndefu ongeza mafuta taratibu na jitahidi kucontrol spidi yani kama una hakika kipande fulani hakina kupunguza mwendo ongeza mwendo taratibu mpaka spidi uitakayo kisha nenda nayo hiyo mpaka utakapotaka kupunguza punguza taratibu pia
Ukiwa mtu wa kupanda na kushuka yani mara umevuta toka spidi 80 mpaka 120 mara ukashuka ghafla mpaka 70 kisha mara ukavuta tena mpaka 120, 30, 40 nk kisha ukashuka ghafla utaisoma
Mwisho uendeshaji wa mjini ni ghali mno kwa mafuta kwakuwa break ni kila dakika