Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Salama mkuu!
Long time no see🙉

Ist zimekua too much, its good to be a lito bit different. Chukua volvo, ford ama terios (kid)

Tupo kaka kwenye mfanano uko sahihi lakini wengi huogopa ishu za spare na matengenezo unapokuwa exclusive!
 
Mkuu hebu nipe ushauri kuhusu pajero mini yaani GDI uimara na udhaifu wake...

natanguliza shukran.

Niko njiani narudi Dar kaka ngoja kesho nikijaaliwa kufika salama takufanyia mchakato
 
Hapana mkuu.Alivyosema Richard ndio sahihi, Airbag ikishapachikwa kwenye sterling haiguswi wala sensor haiguswi, Airbag sio kama tunavyobadilisha Oil au spark Plug. Airbag sio hivyo, ikishafungwa pale inasubiri tu ajali itokee ikulinde si zaidi ya hilo.

Ni sahihi Kalamzuvendi lakini nilipoongelea service sikumaanisha kwamba lile boya/ yake maboya yafunguliwe au hizo sensors la hasha! Service/checking ya airbags inafanyika kwa mtambo maalum kuangalia pressure ya boya/maboya na defect yoyote kwenye sensors! Wenzetu wanafanya hivyo

Na bado nasimamia palepale kwamba lifespan ya airbag initially ilikuwa ni ten years sijui kwasasa pengine imeboreshwa zaidi kwakuwa tech inabadilika kila kukicha, baada ya miaka kumi chances za airbags kufanya kazi kwa kiwango kilichokusudiwa ni 75/100 ndio maana pamoja na hili la airbag nchi nyingi wameweka standard ya matumizi ya gari isizidi miaka kumi wajep kwa mfano wanazingatia sana hili

Hili la airbags kutofunguka wakati wa ajali linasababishwa pia na udanganyifu wa wauzaji hasa magari ya Dubai! Magari mengi ni yale rejects Japan jamaa wanayaokota wakifika Dubai wanabalidilisha spare parts mbovu zikiwemo airbag (kwa maana ya boya tu) zilizopasuka kupiga rangi upya na kusafirisha Afrika

Ukija unanunua gari bei poa kumbe lina matatizo yake yasiyoonekana, na mara nyingi gari zao sio kitu kigeni kukuta rangi zinatofautiana ama kwenye milango, bumpers au mudguards
 
Last edited by a moderator:
Jamaa yangu kanunua Suzuki Aerio, nikamuuliza iko poa akasema poa ila spea ni za shida kidogo. Sasa kama kuna anaejua tabia za hii gari atujuze maana mitandaoni naona hazina bei, je zina shida yoyote?
 
Jamaa yangu kanunua Suzuki Aerio, nikamuuliza iko poa akasema poa ila spea ni za shida kidogo. Sasa kama kuna anaejua tabia za hii gari atujuze maana mitandaoni naona hazina bei, je zina shida yoyote?

Ngoja zichanganye bei itashuti unakumbuka Suzuki carry ilikuwa m3 tuu?
 
a
Asante sana gear box ikifa si ninaweza weka ingine au nikaibadilisha ikawa automatic?

Inawezekana kabisa kubadili transmission toka Manual kwenda Automatic lakini, kufa kwa gearbox kwa gari inayotumika kwa matumizi personal huwa ni very rare kwahiyo usiogope uzuri hayo matatizo yote yanatengenezeka sababu spare za hiyo gari zipo.
 
Rufiji,

What is the point of having a balance government based on religion if it is not effective? why fear that if one group is majority then they have an advantage?

Bottom line we are repeating the same nonsense by bitching about religion the same way it done after independence and continued in the past 3 administrations.

It is time to move one and think progressivelly and ask if these apointees can deliver! The foundation of our success is based on efficiency and effectivenes of those who are empowered to run things and not political or religious affiliation.
lusungo kwanza niwie radhi kwa kuchelewa, binafsi sina uzoefu sana na hizo ila kwa utafiti niliofanya kwa watu 2,3 wanaozimiliki wameniambia kuwa ni gari very comfortable ila ni 'handle with care' hazitaki shida na vipuri kidogo bei imechangamka, na hata ulaji wa mafuta kidogo uko juu
 
Last edited by a moderator:
Habari wana jf! Nahitaji a serious clearing & forwarding agent. Ani pm namba yake please!
 
Nissan Fuga ndio mbadala wa brevis na mark x mjini saiv.......mwenye uzoefu na Nissan Fuga atupe characteristics zake basi maana naona zinamiminika sana mjini saiv, na uongo dhambi jinsi fuga lilivyokaa tu linatia hamasa sana kuliko hata mark x na brevis kwa maisha ya ujana
 
Kwa nini wabongo tunanunua migari ya kufanana wote? Rav 4 namba1, ist mmmh kero kila gari 5 basi 2ist. Tatizo ni nini?

Kasumba tu mi nasukuma escudo langu safi,ila pia nimegundua hiyo kasumba inasababishwa na kutishana lakini pia tabia ya watanzania wengi kuiga, ukiwa pale mbeya kwa mf. utagundua wenzetu wazambia wananunua varied brands,kv audi,Benz,saab,discovery,nk Sie hapa watu wamejaza mitoyota tuu! nahisi watz wanadanganyana kwamba rare brands hayana spares kirahisi eti,tena Dar ndo kabisaa bora hata arusha au mbeya wanachanganya kidogo hapa Dar ukipita foleni ni mjazano wa marav4 wee vi-ist,macarinaa agh
 
mkuu bado nasubir kwenye matumiz ya gear 1,2,3 baada ya D kwenye subaru forester
Kwa subaru ukihamisha gia liva toka d kwenda 3, 2, au 1 ni kuitoa kwenye mfumo wa full automatic kwenda semi manual. mfano kwa kuchagua 1 gari itatembelea gia no. moja pasipo kubadilisha gia. Huwa nyepesi na nguvu nyingi with high engine rev.

Ukichagua 2 itatembea kwa gia no. moja na mbili. Ni chaguo sahihi kwenye utelezi. Na ukichagua 3 itatembea kwa gia no moja, mbili na tatu. gari huwa nyepesi na huchanganya haraka.

Kama unashindana unaweza kuingiza gia kama manual kuanzia gia no. moja mpaka tatu kisha hamishia d kuiruhusu gari kuingia gia no 4, wakati wa kuhamisha gia ni lazima kubonyeza batani iliyo kwenye gia liva.

Pia down shifting yaani kutoka d kuja 3, 2 na 1 huweza kutumika kama breaking system wakati wa tyre bust.
 
Back
Top Bottom