Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Wakuu nataka kununua Paso kwa mizunguko ya mjini tu. Je inafaa? vp uimara wake na ulaji wa mafuta?
Au ni gari ipi ndogo ambayo ni bora zaidi.
Nb. Bei iwe kama ya Paso au ikizidi basi isizidi mil 8.
Naomba
Kwa gari ndogo na imara starlet iko pouwa na engine yake ni moja kati ya engine zinazovumilia tabu nyingi ni 4E za coil na distributor .Vipuri ni tele with resonable price...fuel consumption ni 1lt/14 km. Kwa passo ni gari ya kisasa kiasi ila body ni delicate na rough road haihimili.. vipuri bado ni changamoto kiasi, fuel consumption ni 1lt/21 km.
Fanya chaguo..wadau watapita kuongeza yaliyo ya kitaalamu zaidi
 
Habarini za asubuhi wadau. Samahani nina swali nahitaji msaada wa majibu. Nina landrover 110 nikitembea spidi zaidi ya 80 tairi za mbele pamoja na usukani vinacheza lakini nikitembea spidi chini ya hapo inatulia je hili tatizo linasababishwa na nini maana nimebadilisha drop arm na kuweka mpya lakini tatizo bado lipo.
 
Wadau naomba ushauri kuhusu hizi gari toyota brevis kwa anaezijua haswa ulaji wa mafuta nataka kumvua mtu @ Mshana

#pathfinder nilishalitolea maelezo humuhumu mkuu kama alivosema mshana ukirejea utaona...kwa ufupi brevis ni miongoni mwa salon cars poa ila kama una mawazo ya bajeti ya mafuta hii Gari achana nayo 'inakunywa' enjini yake ni 2.5 na 3.0 na zina undugu na tyt progress 'farasi' hizo mafuta usiweke ya kupima kwenye sadolin inataka kiwese
 
Habari ndugu zangu...
Nawpongeza sana wana jf kwani huwa najifunza mengi kwenye hili jamvi. leo ningependa ushauri kuhusu gari ile niweze kufanya maamuzi sahihi. ninahitaji toyota saloon na kwa mapenzi yangu mimi ningepenga gari ambayo inastahimili barabara ya vumbi na ulaji wa mafuta mzuri , pia iwe ya bei nafuu ya kuagiza kutoka nje. binafsi ningependa CORONA PREMIO 2000, COROLLA 2000.

Naomba ushauri
1.nichukue ipi? au nichukue tofauti na aina hizo za gari?
2.pia ningependa kujua ni aina gani ya ingini ni bora kwa mazingira niliyotaja??.........
3.pia kwa wazoefu wa kuagiza magari kuagiza aina hizi za gari za mwaka 2000 inaweza kugharimu sh. ngapi mpaka gari inaingia barabarani???

Asante sana..

kaka nichangie kipengele kimoja tu..Corona premio hujakose kabisa wala huta juta ni gari nzuri na vipuri vinapatikana...jamaa yangu anayo yenye engine ya 7A tunapiga safari za vijijini na hata Mwanza mpaka mtukula mashine iko poa..
 
Tatizo la hii gari yangu ni ac yake haitunzi gesi yan nimejaza gesi mwezi wa December lakn January imeisha nikaenda kujaza tena nimetumia week tu imeisha nimempelekea fundi kaangalia kasema hakuna leakage kwenye pipes zake akajaza gesi lkn nayo imekaa week imeisha yani majanga tu joto na vumbi ni kero sana
 
Kuna leakage fundi kashindwa kuigundua, hakuna mazingaombwe hapo
 
Habarini za asubuhi wadau. Samahani nina swali nahitaji msaada wa majibu. Nina landrover 110 nikitembea spidi zaidi ya 80 tairi za mbele pamoja na usukani vinacheza lakini nikitembea spidi chini ya hapo inatulia je hili tatizo linasababishwa na nini maana nimebadilisha drop arm na kuweka mpya lakini tatizo bado lipo.

Jaribu kufanya wheel balance
 
Thanx ndugu yangu mujemaso. Tena ngoja nikimbie gereji sasa hivi. Maana inanikosesha raha kweli.
 
Habarini za asubuhi wadau. Samahani nina swali nahitaji msaada wa majibu. Nina landrover 110 nikitembea spidi zaidi ya 80 tairi za mbele pamoja na usukani vinacheza lakini nikitembea spidi chini ya hapo inatulia je hili tatizo linasababishwa na nini maana nimebadilisha drop arm na kuweka mpya lakini tatizo bado lipo.

General information ya gari kuvibrate baada ya 80+ ni
-shock up kuchoka
-stabilizer link kuchoka
-ball joint kuchoka
- kuweka Spencer
- tyres kuchoka
- rack ends kuchoka nk nk
 
mkuu Mshana ubarikiwe sana kwa uzi wenye manufaa kama huu
Naomba kujuzwa nina jamaa angu tupo ofisi moja anataka agiza gari ,kati ya MAZDA TRIBUTE na SUBARU FORESTER unamshauri achukue ipi in terms of durability and availability of spare parts.
Mungu akubariki sana!
 
Natafuta wapi naweza kuservice gari langu aina ya Subaru. Nimekuwa nalo kwa mwaka sasa ila sijapata fundi mzuri na sehemu nzuri ya kununua spare hapa DAR.

Natanguliza shukrani
 
Nashukuru kaka kwa hizi za kisasa naomba N'yadikwa na Kaizer wakujibu tafadhali, nawachosha bandugu lakini tunawahitaji kila mara
 
Last edited by a moderator:
Natafuta wapi naweza kuservice gari langu aina ya Subaru. Nimekuwa nalo kwa mwaka sasa ila sijapata fundi mzuri na sehemu nzuri ya kununua spare hapa DAR.

Natanguliza shukrani

Kuna mafundi was subaru tabata dampo ni wa zamani sana miaka ile ya 2003--->>>walikuwa wazuri sana kwasasa sina hakika kama bado huduma ni ya kiwango kilekile
 
sorry for interruption. Nasikia gari la happy nation limetumbukia mlima kitonga leo 9/4/2015 majira ya saa kumi, je ni kweli? nina ndugu yangu humo ila yeye hapatikani kwenye simu, naombeni uthibitisho mwenye taarifa kamili.

Happy nation limepata ajali mikumi la kitonga ni lingine nenda jamii photos utaona kila kitu
 
Natafuta wapi naweza kuservice gari langu aina ya Subaru. Nimekuwa nalo kwa mwaka sasa ila sijapata fundi mzuri na sehemu nzuri ya kununua spare hapa DAR.

Natanguliza shukrani

Kuna fundi ana garage yake kinondoni, nyuma ya majengo ya iliyokua shule ya biafra, huyo fundi anatengeneza SUBARU tu, jina la garage ni 0-60, anaitwa God, ni maarufu sana mitaa ile.
 
Back
Top Bottom