Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Habari zenu wakuu.

Natumai mu-wazima kabisa wadau kama MADA inavyojieleza wakuu naomba msaada wa kujua ushuru wa hii gari kuitoa bandarini..................ipo njiani, tarehe 22 Apr inataraji kufika bandarini ningependa kujua mapema gharama ili nijue kipi cha kufanya wakuu,natanguliza shukran.

SPECS :

Make : Nissan X-trail

Engine Size :1,990cc

Registration
Year/month :
2002/3

Manufacture
Year/month :
2002/3

Price : U.S $ 3600

BF369773_1aea8d.jpg

BF369773_13e0d2.jpg

BF369773_a6e0ca.jpg

For more details visit here :

Nissan X-trail.Beforward

THANK YOU.

mkuu hiyo hapo;

Reference Number1415412147
Make:NISSAN
Model:X-TRAIL
Body Type:SUV
Year of Manufacture:2002
Fuel Type:PETROL
Engine Capacity:1001 - 2000 CC
Customs Value CIF (USD):3114.00
Import Duty (USD):778.50
Excise Duty (USD):194.63
Excise Duty due to Age (USD):1167.75
VAT (USD):945.88
Total Taxes (USD):3087
Total Taxes (TSHS):5541165
 
Hiyo calculator ya TRA ni ngumu.........mi hata siielewi........
nakuomba utukokotolee hii halafu utuwekee hapa Ili tuelewe vizuri.........

checki hapo chini:

Reference Number1415412147
Make:NISSAN
Model:X-TRAIL
Body Type:SUV
Year of Manufacture:2002
Fuel Type:PETROL
Engine Capacity:1001 - 2000 CC
Customs Value CIF (USD):3114.00
Import Duty (USD):778.50
Excise Duty (USD):194.63
Excise Duty due to Age (USD):1167.75
VAT (USD):945.88
Total Taxes (USD):3087
Total Taxes (TSHS):5541165
 
habari za muda huu wadau,leo kuna mtu alikua anataka kuniuzia gari bila card nayeye ni mmiliki wa pili lkn anatumia copy ya mmiliki wa kwanza,madai yake yuko busy hawezi fuatilia,nikamwambia twende tukaandikishiane police au TRA lkn kakataa nami nikashtuka.. kwa uzoefu wenu mlokua nao nini kingenitokea endapo ningeamua kuichukua kwa card ambayo ni copy?!
 
Duu umeponea tundu LA sindano kupigwa hizo case zipo nyingi sana pale TRA makao makuu ghorofa ya nne chumba cha kwanza kushoto ukitoka kwenye lift, pameandikwa Investigation, kwenye post za mwanzo angalia nimeizungumzia hiyo kitu kwa undani
 
duu!! namshukuru Mungu kwa kuponea tundu la sindano,naomba unijulishe kwa niaba ya wadau wote kwa haraka haraka ni vitu gani muuzaji anatakiwa akupatie kama mmiliki wa 3,ahsante
 
Total ni pamoja na uchakavu

Wakuu nawashkuru sana sana kwa michango yenu wandugu.

Nilitingwa sana leo sikupata nafasi ya kuingia hapa nilipata msiba na nashkuru kuwa tumezika salama.
 
Reference Number1415412147
Make:NISSAN
Model:X-TRAIL
Body Type:SUV
Year of Manufacture:2002
Fuel Type:PETROL
Engine Capacity:1001 - 2000 CC
Customs Value CIF (USD):3114.00
Import Duty (USD):778.50
Excise Duty (USD):194.63
Excise Duty due to Age (USD):1167.75
VAT (USD):945.88
Total Taxes (USD):3087
Total Taxes (TSHS):5541165
Mkuu unaongeza na usajili 150,000
Ada ya mwaka(motor vehicle 230,000
Kulingana na calculator ya TRA Bandalini
unaweza kuulizia wahusika Kiongozi

Mkuu nakushkuru sana sana kiongozi kwa msaada wako wa hali ya juu umenipa mwanga wa kutosha kwa jinsi ulivyopangilia kwa uzuri kiongozi MUNGU akubariki sana sana ndugu yangu.
 
Kuna mdau ameipost page yenye hesabu Total Custom Value (CIF) inatakiwa kuwa $3114 sasa unaweza kuwa na invoice Value yake ni zaidi ya hiyo kodi lazima itazidi 5.5

Ni kweli jcb nnavyoelewa ni kwamba custom value ikiwa juu ya CIF na kodi nayo haiwi kubwa kiongozi wangu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu umesahau kuna cpf charges ndio maana nikamweleza aandae 6.5 ml na hiyo calculator TRA saa nyingine haiwafuati ipasavyo.

cpf charges inakuwa ni nini MANI ?.
 
Last edited by a moderator:
duu!! namshukuru Mungu kwa kuponea tundu la sindano,naomba unijulishe kwa niaba ya wadau wote kwa haraka haraka ni vitu gani muuzaji anatakiwa akupatie kama mmiliki wa 3,ahsante

Njia rahisi kabisa ni kwenda naye hapo nilipokuelekeza kwakuwa siku hizi watu wanapigwa sana
Iko hivi ni nina gari anakuja mshkaji kuniazima let's say akimbie Tanga mara moja kumbe fix
Namkabidhi gari na vitu vyote muhimu ikiwemo copy certified ya gari, yeye anaenda kutengeneza kitambulisho bandia kwa jina langu anaenda polisi kuripoti wizi/upotevu wa kadi halisi ya gari,anapewa loss report
Akitoka hapa ni TRA, akifika anaonyesha police loss report anapewa kadi duplicate ya gari ikitoka siku ya pili anatengeneza mkabata wa mauziano ya gari, anajiuzia kwa jina lake halisi na kupata kadi duplicate yenye jina lake
Huku nikijua mshkaji yuko mkoa kumbe yupo TOWN anadalalia gari yangu, akifanikiwa kuiuza mimi nikaja kugundua nikifika TRA na kukuta hizo habari na kadi original wanaifungia gari kwenye system na kuanza kuitafuta
Ukikamatwa nayo wewe ndio mwizi
Na mara nyingi TRA hawahangaiki kutafuta gari wanakusubiri kwenye road licence ukishalipia unaenda dirishani kuchukua sticker yako....habari mbaya huanzia hapo
 
Back
Top Bottom