Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Kwa case ya ⛽ consumption basi chukua toyota spacio /wish...but Noah voxy imekaa kifamilia zaidi and comfortable japo ni cc1990 sio Huo Ndio ungekuwa uchaguzi wangu

Asante sana mkuu kwa ushauri.
 
SU- Shirika la Umma
DFP- Donor(s) Funded Project. Siku hizi wameboresha na kuwa DFPA kwa maana ni DFP tolea A
ST- Serikali ya Tanzania(toleo hukaa mbele kama STK ni Serikali ya Tanzania toleo series za herufi K)
JW- Jeshi la Wananchi( mbele yake huwekwa namba ya gari kwa idadi tangu linanunuliwa na kwa chini limeingizwa mwaka gani
SM- Serikali za Mitaa( haya hayamilikiwi na Serikali kuu kama zile STK, bali ni za TAMISEMI
MG- Magereza Tanzania
PT- Polisi Tanzania
AG- Attorney General
ST...A. Gari za Mjengoni japo sina hakika.
S- Speaker
KUB- Kiongozi wa Upinzani Bungeni
RAC- Gari za Shirika la Reli
T....CD ni gari za Mabalozi na mashirika ya Kimataifa. Rangi hutofautiana kati ya Blue na Kijani ili kutofautisha kati ya Mabalozi na Mashirika ya Kimataifa/UNO!
Mkuu ni MT
 
Wapendwa wana JF
Nimekuwa Napata shida barabarani kutoka kwa washirika wenzangu wa barabara hivyo naomba kukumbusha mambo yafuatayo

1. Washa indiketa unapotaka kutoka barabarani au kuruhusu gari lipite angalau meta 50 kabla ya kutoka.

2. Ukiona mwenzako ana ovateki, usimfuate/ kuunganisha hadi ujiridhishe kuwa ni salama.

3. Kuwasha indiketa sio kibali cha kukuruhusu upite/ kupinda kulia, ila ni ishara kuwa unataka kupinda, hivyo ukishawasha, sharti uangalie nyuma (side mirror) na mbele, kujiridhisha kuwa ni salama kabla ya kupinda.

4. Usikimbize gari mahali ambako huoni umbali mrefu/ kwenye Bonde au Kona, kwani huwezi jua nini unaweza kukutana nacho huko (wanyama, gari imeharibika nk)

5. Mkiwa mnafuatana (magari mawili) mwenzako akasimama, usipite kabla ya kujua kwa nini amesimama.

6. Kuendesha chini ya KM 50 kwa saa highway, haikuepushii ajali bali ni kuwapa usumbufu watumia barabara wenzako; cha msingi ni kufuata taratibu za barabarani.

7. Kumbuka; kumbiza gari sio chanzo cha msingi cha kuleta ajali; Kinacholeta ajali ni kutokujua sheria au kutozifuata sheria na alama za barabarani zinazokuruhusu wapi ukimbize na wapi uende polepole.

8. Usiongee na simu lakini pia usipige sana stori au Kusikiliza radio/mahubiri kwenye radio wakati hujazoea kwani ukinogewa unaweza kujisahau na kukwangua/kukwanguliwa

9. Jitahidi kujua ukubwa wa gari lako, hasa kama unarudi nyuma au unapita sehemu nyembamba; omba msaada wa kuelekezwa.

10. Ukipaki gari barabarani, hakikisha ni salama kabla ya kufungua Mlango. Hii ni jukumu lako kuangalia usalama wako na uliowapakia hasa kama mlango unafungukia kulia (upande wa barabarani).
Kumbuka kuna bodaboda zinazoweza kugonga mtu anayeshuka kwa urahisi

Nawasilisha!!!
Nami naongezea hapa, kila mara angalia na kumruhusu aliye upande wako wa kulia apite kwanza kwenye mzunguko (keep left/ round about) maana hili limekuwa tatizo sugu hasa kwa madereva wa Dar.
Usipige honi ukiwa unaendesha kwenye service road, hospitali au mahakamani.
Usiendeshe mwendo kasi ukiwa kwenye barabara za mitaani kwakuwa unachangia hizo barabara na watumiaji wengine
 
Mshana umetupa elimu nzur sanaa labda niulize kidogo me kwasasa natumia vits old model kwanini hizi Gari bampa lake halikazi na kwenye bonet kama kuna uwazi na ntalitatua vipi tatzo hilo?
 
Mshana umetupa elimu nzur sanaa labda niulize kidogo me kwasasa natumia vits old model kwanini hizi Gari bampa lake halikazi na kwenye bonet kama kuna uwazi na ntalitatua vipi tatzo hilo?

Kwenye bonet huwa kuna laba zina tred jaribu kuzipunguzia kimo kwa kuzifunga
 
Zile adjuster za bonnet haziko imara ndio maana baada ya muda hutokea shida kama hiyo na hata kwenye bumper pia vile vishikio vyake
 
Habarini jamani! Naomba kuuliza hivi rangi ya gari zaidi ya color preference kuna technical explanation inayoweza niguide kuchagua rangi ya gari!? Nauliza hivyo sababu nimechagua sehemu subaru forester nyekundu jamaa yangu kaniambia siyo rangi nzuri.
 
Kitu black ndio nzuri mkuu! Au kitu yenye dark colour...! Dark Blue au Dark Green mkuu! Silver colour au white colour zipo nyingi kitaa
 
Angalia post za juu utapata majibu yote! Hizo ni gari nzuri ngumu zinazohimili all weather
Mshana, naomba unijuze kwenye Toyota cam kwenye gear kuna herufi P R N D 2 na L, je hii L ina maana au kazi gan? Naomba msaada plz
 
Kaka mshana mi MSANGI aisee sasa Nina tumilion 5 naweza pata kagar kazur ka familia ILS nafsi inapendelea Subaru forests,passo,mak 11 new model,pia kasiwe mkebe na niweze kukamudu
 
wadau kufanya overhaul ya engine ya Alteza 1G six cylinders yaweza kufika sh ngp?
 
Mshana, naomba unijuze kwenye Toyota cam kwenye gear kuna herufi P R N D 2 na L, je hii L ina maana au kazi gan? Naomba msaada plz

L-low gear gari inakuwa kwenye mwendo mdogo lakini wenye nguvu nyingi mara nyingi hutumika kwenye miinuko utelezi barafu na mikwamo
 
Kaka mshana mi MSANGI aisee sasa Nina tumilion 5 naweza pata kagar kazur ka familia ILS nafsi inapendelea Subaru forests,passo,mak 11 new model,pia kasiwe mkebe na niweze kukamudu

Unaweza lakini ya mkononi nafikiri tuna wadau humu wanaweza kukusaidia katika hilo naamini watakuja
 
Wakubwa nahtaj kununua Toyota wish hvyo naomba pro na cons zake maana kuna jamaa kaanza kunirudisha nyuma an anasema engine take sio vvti,nawasilisha
 
Wakubwa nahtaj kununua Toyota wish hvyo naomba pro na cons zake maana kuna jamaa kaanza kunirudisha nyuma an anasema engine take sio vvti,nawasilisha

Naomba niwe mkweli na usikereke hizo gari kama zilivyo nyingi za kisasa huko chini kwenye links tyrod ends shock ups na ball joints ni majanga hasa kama utakuwa unaishi rough road
 
Kaka mshana VP kuhusu injini yake?in aina gani na hasara zake?kuhusu ishu uliyoshaur awali c tatzo maana barabara ya vumbi ni ka mita mia 3 baada ya hapo lami hadi kazn ,nakaa chanika VP kuhusu wese kwa umbali ule ?I hope wadau mnapajua chanika
 
Vingine viko sawa engine ni ya kawaida kabisa hata fuel consumption pia
 
Back
Top Bottom