Kuhusu FreeLander na Landrover zote kwa ujumla, yaani Defender,Freelander,Discovery na Range rover mnaweza kuniuliza maswali mengi muwezavyo hapa,
Nikianzia na FreeLander kwenye swami lako la msingi:
Matoleo ya mwanzo kabisa ya FreeLander yalipewa Polisi, baada ya warrant Kwisha FreeLander hizo zilipelekwa kwa mafundi wa mtaani kwa matengenezo nadhani kwa kuwa CMC, ambao ni wakala gharama zao za matengenezo ziko juu sana,kwa bahati mbaya sana magari nayo yanatumia Umeme mwingi sana wa ki-electroniki( electronic control systems) na pia yana complicated security system, na yakishakua na security issue ufumbuzi pekee kwa wakati huo ni CMC, ugumu huo ukapelekea mafundi kushawishi suluhisho pekee ni kubadilisha injini, ( weka injini ya RAV4, crazy!), dhana hiyo ikaacha kovu kwamba FreeLander hazitengenezeki, ila FreeLander ni magari mazuri sana tu, very comfortable, 4WD, n.k.