Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Matumizi ya M kwenye na botton za power ect snow pia kwenye stering kwa chini kuna botton ukiweka grar leaver kwenye M zinakua active mean akibonyeza zina toa mlio gari ni Alteza RS200 3s1998 cc
 
gari yangu ni automatic nikibadilisha gear kutoka P kwenda R au D inakuwa inashtuka, kwenye dashboard hamna taa yoyote ya hatari inayowaka, je tatizo itakuwa ni nini?

Nenda kwa Fundi mwambie aangalie Engine mounting kama ziko poa. Nahisi hilo linaweza kuwa tatizo,
 
gari kuwa na RPM kubwa at silence zaidi ya 1.5 , je ni dalili ya tatizo au ni kawaida?

Normally rpm haitakiwi kuzidi 1000, inatakiwa iwe chini ya hapo. Though mi kila siku asubuhi nikiwasha rpm inasoma 1200-1300 lakini baada ya kupata moto engine rpm inashuka hadi 800.
 
unaishi kijiji gani boss?? kwa nissan mkuu ushauri wangu mkubwa ili uendelee kuipenda gari yako na usiiharibu tafuta mashine uipime na nenda kwa fundi ambaye anaweza kurekebisha maana now watu wengi wamenunua mashine kwa lengo la kupima tuu wanakutoa pesa zako wanakwambia tushakupimia na kuclear fault code unawapa pesa yao wanasepa.

mashine ni kama pen kwa karani ndio kifaa chake cha kazi.

hivyo anakupimia na kukurekebishia pia.

nakingine watanzania tuache kuwa nyuma kwa kila jambo suala kama lako hilo ni jepesi sana mbona.
unamiliki gari ya milion zaidi ya tano unashindwa kununua code reader ya $50 kwaajili ya kuchekia matatizo yako kwenye gari??

unamiliki smart phone ya laki 5 or 4 au hata laki na nusu unashindwa kununua obd 2 socket ya blue tooth unakuwa unachomeka kwenye gari na kufiagnosis gari yako kwa kutumia simu yako?? wakati garama ya hizo blue tooth soketi za obd 2 ni kama $9 or 10 nakitu tuu??

ilipaswa mnapokuja humu muwe mnasema jamani mwenzenu nime pima gari yangu na nimepata fault code hii example P0135 CKP circuirt malfunctio
je inamaana gani?? au hiyo ckp kwenye nissan x trail inakaa wapi?? ndio unapewa msaada stahiki.

now unauliza swali ambalo ni rahisi sana harafu ni gumu.kwa mm binafsi lipo ndani ya uwexo wangu lkn kwa style yako lipo nje ya uwezo wangu.

ungekuwa upo dar ningekwambia nitafute mm nitakupimia bure kabisa ki JF lakini spea juu yako kama itahitajika.

au kama unaweza fika dar poa.

magari mengi yanakufa na kuharibika zaidi kwajili ya nyie wamiliki kutokuyapa tiba stahiki.

na kwanisani ilivyo ukiitengeneza kienyeji utajuta na huto kaa uje uzipende tena gari za nissan

Mkuu LEGE nielekeze wapi pa kununua hizo vitu??
 
habari wakuu, asante kwa mada hii ni msaada sana kwetu sisi tusio na utaalamu wa magari, naomba kujuzwa kuhusu engine ya toyota caldina new model ambayo ni 4wd uimara wake,consuption ya mafuta spare parts na service na kama zinavumilia njia za vumbi nipo kwenye mchakato wa kuagiza. with regard.
 
Wakuu naombeni msaada! Gari yangu inawasha taa ambayo inafanana na ile ya temperature ila inarangi ya kijani, eti wakuu inaashiria nini.
Hapo hakuna tatizo lolote,inamaanisha ingine ni ya baridi sana unashauliwa uache gari silencer mpaka izimike ndio uondoe gari,,na wala haichukui mda kama gari iko byee
 
wana JF nipendezwa na hii new model ya Escudo. Nataka kujua kwa ambayo wanaitumia. Vipi uimara wake? matumiz ya mafuta. upatikanikaji wa spare? na gharama za spare zake uki compare na toyota
thanks
 
Less cc, less ugumu wa gari (kuepuka uzito), less usalama, less life span ya engine! So gari ya cc 650 ikiwa na kilometa 50,000 unaweza kuta ni sawa na gari ya cc 2700 yenye km 200,000
Hii point ni ya muhimu sana hasa kwa watu wanaodhania kuwa kununua magari ya cc ndogo wameepuka gharama,ukweli ni kuwa hizi gari zenye cc ndogo engine life span yake ni ndogo sana,mfano mzuri ni Toyota Vitz,Toyota Duet nk nyingi zimekufa mapema kabla hata ya kufikisha km 150,000,wakati magari mengi yenye cc kubwa,eg cc 2000 and above kwenye km 150,000 bado zinakuwa vizuri sana.
 
Gari yangu inaonesha kuwa handbreak iko on ilihali haijawekwa ,tatizo laweza kuwa NI nini ?
 
Naomba kujuzwa kuhusu toyota alphard kwa wenye kujua au waliotumia. Naopenda space na comfort ndani ila sijui uimara wa injini na maintenance yake.... Vipuri n.k

Asanteni
Kama utaweza kuimudu harrier V6 basi na alphard utaiweza tu maana engine moja......kwenye accessories zingine alphard ni habari nyingine very comfortable car.
 
Habari Wakuu
Naomba kueleimishwa tofauti kati ya Toyota Grand Mark 2 na Toyota Mark X katika mambo haya
1. Ubora/uimara
2. Ukubwa wa injini
3. Gharama za service
4. Mifumo ya kiumeme
5. Mengineyo mnayojua zaidi
Matumizi yake ni pamoja na safari ndefu kama za Dar to Tunduma na kuna wakati ntahitaji kupita barabara za vumbi
Nawasilisha

1. Ubora / uimara
Mark X ni bora na imara zaidi kuliko gx110 especially kwenye swala la usalama

2. Ukubwa wa engine
Hizi gari zote mbili engine yake kubwa sana ni 2.5L, japo kwa gx110 zipo za chini mpaka cc1990 but kwa mark X ni 2.5L

3. Gharama za service
Hapa naona wote wanaringana tu lazima 60,000 mpaka 80,000 ikutoke pamoja na gharama za fundi. Kama ukianza kununua parts hapo sasa mark X inaweza kwenda mbali maana kama mark x control box yake tu haiwezi fanana bei na ya gx110.

4. Mfumo wa umeme
Mark X inatumia umeme mwingi coz ni gari ya kisasa hata hivyo, wazungu wamejitahidi kupunguza consumption ya mafuta kwakuongeza matumizi ya umeme.

5. mengineyo
Kwenye barabara za vumbi hizi zote mbili zinafaa coz zinatumia wishbone mbele na nyuma inamaana hata kuhama njia hilo halipo, japo mark x itakua stable zaidi kutokana na kuwa nzito zaidi maana gx110 inakua na kg1350 mpaka kg1450, hila mark X inacheza kg1525 nyingi.

Na pia mark x imewezeshwa Traction Control hii inafanya gari inakua stable zaidi hata kwenye corner za iyovu unalala tu bila gari kuyumba.

My take:
Mark X inatosha
 
Safi kabisa. Kumalizia Mark X ni ghali zaidi kuliko Gx 110 kutokana na sababu zote hizo hapo
 
Gari yangu inaonesha kuwa handbreak iko on ilihali haijawekwa ,tatizo laweza kuwa NI nini ?
Ni gari ya aina gani?? inawasha taa ya hand brake peke yake?? au inawasha pamoja na taa ya ABS?? Kama zitakuwa zinawaka zote 2 basi kunatatizo au kama ni ist au gari yenye mfumo wa ABS basi control ya ABS itakuwa na shida kuna errors kidogo
 
ahsante kiongozi, ni noah aina ya voxy
 
Back
Top Bottom