Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Ok nimeku-PM in Box
mwaka huu mzuri mafuta yanashuka bei na vispea vya gari za kijapani navyo vinashuka
sasa bei za magari ndio zinaFlactuate nasubiria Noah zishuke hata zikaribie 5.5m sio Noah VOXY natafuta Town ace au Liteace (Limo) Lyimo
nilifika huko Lumumba nikaenda Ilala wnanikodolea macho tu wanataka 10m niakimbia Mlimani kuDeposit vihela vyangu wenyewe nikawapa wanywe supu maana walishanizunguka wakijua nimeuza ng'ombe huku Bara,
Mungu mkubwa nikaambiwa unabahati ukiDraw Mlimani city wanachukua lkn si kuweka aaa salama tu

Mkuu Ukwaju,
Kwa nini siyo VOXY..? Plz niweke sawa vile mie nataka kuvuta hiyo kitu.. Thanx
 
Mkuu Ukwaju,
Kwa nini siyo VOXY..? Plz niweke sawa vile mie nataka kuvuta hiyo kitu.. Thanx
Mwaka 2012 nlinunua voxy T ... CEK nikaitumia mpk 2014 nikauza. Ilikua poa tu kwa matumiz ya home-town! Nijuavyo Noah Ace zenye diff ni bora sana kulinganisha na dizain km hiyo ya magari
 
Habari wakuu, mi nauliza je hapa Tanzania upatikanaji wa vipuri vya Toyota Delta ukoje?
 
Hiyo engine inaitwa D4 sometimes......ki ukweli wengi tunazikimbia ....sio mbaya ukipata Fundi mzuri incase of emergency.......lakini nakushauri chukua 3S......hiyo engine imeshajadiliwa sana humu ndani tena uzi huu huu.......

Uwiiiiiiiii....kurasa ni nyingi mno kusoma, shida yake ni nini hasa??
 
Wakuu radio ya gari module frequency zake ni kati ya 76.6mHz na 89.9 MHz, hivi kuna uwezekano Wa kuongeza maana kuna redio stations nyingi sizipati na ningependa niwe na wide range.
 
Wakuu radio ya gari module frequency zake ni kati ya 76.6mHz na 89.9 MHz, hivi kuna uwezekano Wa kuongeza maana kuna redio stations nyingi sizipati na ningependa niwe na wide range.

Hapo hakuna addition ya frequency cha msingi badilisha redio ziko dukani kama Sony zinamaliza frequency
 
Wakuu radio ya gari module frequency zake ni kati ya 76.6mHz na 89.9 MHz, hivi kuna uwezekano Wa kuongeza maana kuna redio stations nyingi sizipati na ningependa niwe na wide range.
Kuna kitu kinaitwa frequency converter wakikufungia burdan mitaa ya ilala huko
 
Overhaul haina guarantee hasa kwa spare zetu za bongo
Sio kweli mkuu sema labda ufundi ndio tatizo.ukifunga spare original na kwa uhakika gari inakuwa kama mpyaaa.

Uwoga na ubovu wa mafundi now ndio wanakimbilia kununua engine used
 
Wakuu radio ya gari module frequency zake ni kati ya 76.6mHz na 89.9 MHz, hivi kuna uwezekano Wa kuongeza maana kuna redio stations nyingi sizipati na ningependa niwe na wide range.

Inawezekana kuongeza mkuu kwani upo wapi ww?? kuna kitu unafunga hapo mambo yanakuwa powa kinaongeza station nyingine
 
Sio kweli mkuu sema labda ufundi ndio tatizo.ukifunga spare original na kwa uhakika gari inakuwa kama mpyaaa.

Uwoga na ubovu wa mafundi now ndio wanakimbilia kununua engine used
Nilikuwa na maana hiyo hiyo ya spare
 
UFAHAMU KWA WENYE MAGARI;
Matairi ya gari muda wake rasmi wa matumizi ni miaka minne (4) tu toka yatengenezwe (sio toka uyafunge kwenye gari yako).
Ikishapita miaka minne toka tairi litengenezwe linaweza kupasuka wakati wowote. Jinsi ya kutambua tairi lilitengenezwa lini tafuta alama kwenye tairi iliyoandikwa kwa mfumo huu (*2603*) kuna kuwa na alama ya nyota mwanzo na mwisho wa hizo namba nne.
Namba mbili za kwanza zinaonyesha tairi lilitengenezwa wiki ya ngapi katika wiki 52 za mwaka na namba mbili za mwisho zinaonyesha mwaka tairi lilipo tengenezwa. kwa mfano *2603* inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 2003 au *2699* inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 1999.
KAGUA MATAIRI YAKO USITUMIE TAIRI LILILO PITA ZAIDI YA MIAKA MINNE KWANI LINAWEZA PASUKA WAKATI WOWOTE.
Pia kila tairi limeandikwa uwezo wa spidi yake ukikimbiza zaidi ya uwezo wake itapasuka na hizo spidi zimeandikwa kwa herufi kama ifuatavyo
CODE SPIDI
F=============80
G=============90
J==============100
K==============110
L==============120
M==============130
N==============140
P==============150
Q==============160
R==============170
S==============180
T==============190
H==============200
Huandikwa hivi
280/R/70/13/150/S

View attachment 317580

Ndiyo maana nimejiunga na "Wanajamii" kwa ajili ya kupata elimu kama hii toka kwa akina Mshana jr. Ahsante sana.
 
Back
Top Bottom