Mada maalum ya ndege toka FB

Mada maalum ya ndege toka FB

Cockpit au Flight deck ni eneo ambalo kwa kawaida mara nyingi huwa mbele au karibu na mbele ya ndege au chombo cha angani, ambapo rubani hutumia hudhibiti ndege.
Baadhi ya ndege za awali 'cockpit' unaweza kuikuta katikati ya ndege.
Je, unaweza kutambua pichani ni 'cockpit'ya ndege gani?View attachment 2679990

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawajakupa jibu tu pamoja na kuandikwa nyuma ya viti?
Lakini mimi nikiona tu hakuna control column, kuna control stick, moja kwa moja hiyo ni Airbus.
 
Ndege ya shirika la Ural Airlines aina ya Airbus320 ya nchini Urusi, yenye usajili namba RA-73805 itajaribu kuruka kutoka eneo ilipolazimika kutua baada ya kuisha mafuta na kutua kwa dharura kwenye uwanja wa nyasi mnamo tarehe 12 Septemba 2023.

Shirika hilo la ndege lilithibitisha uamuzi wa kuifanya Airbus A320 kupaa kutoka mahali ilipo sasa.
Shirika la ndege linasubiri kuletewa lifti ili kufanya majaribio mfumo wa matairi kama unafanya kazi.

Mpango huo pia unajumuisha kuondoa viti ili kuifanya ndege kuwa nyepesi zaidi kabla ya jaribio hilo.
Ural ilitua eneo hilo ikiwa na abiria 167, wakiwemo watoto 23 na wafanyakazi 6 ambapo wote walitoka salama.

Chanzo:
#airwaysmag
FB_IMG_1696425005442.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
𝙅𝙚, 𝙣𝙞 𝙠𝙞𝙩𝙪 𝙜𝙖𝙣𝙞 𝙪𝙣𝙖𝙙𝙝𝙖𝙣𝙞 𝙝𝙖𝙠𝙞𝙥𝙤 𝙨𝙖𝙝𝙞𝙝𝙞 𝙨𝙖𝙣𝙖 𝙠𝙖𝙩𝙞𝙠𝙖 𝙠𝙞𝙥𝙚𝙧𝙪𝙨𝙝𝙞 𝙝𝙞𝙠𝙞?
FB_IMG_1696440889009.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mujibu wa Air Tanzania, Rubani Kiongozi Murtaza Gulamhussein na Rubani Msaidizi Sweetbert Mtweve ndio wamepewa dhamana ya kuirusha BOEING 737-MAX 9 toka Seattle Marekani hadi Tanzania.
FB_IMG_1696441744003.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
𝗕𝗮𝗮𝗱𝗵𝗶 𝘆𝗮 𝗻𝗷𝗶𝗮 𝗶𝗻𝗮𝘆𝗼𝘁𝘂𝗺𝗶𝗸𝗮 𝗸𝘂𝗽𝗶𝗺𝗮 𝘂𝗶𝗺𝗮𝗿𝗮 𝘄𝗮 𝗺𝗮𝗯𝗮𝘄𝗮 𝘆𝗮 𝗻𝗱𝗲𝗴𝗲!
FB_IMG_1696581060930.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cockpit au Flight deck ni eneo ambalo kwa kawaida mara nyingi huwa mbele au karibu na mbele ya ndege au chombo cha angani, ambapo rubani hutumia hudhibiti ndege.
Baadhi ya ndege za awali 'cockpit' unaweza kuikuta katikati ya ndege.
Je, unaweza kutambua pichani ni 'cockpit'ya ndege gani?View attachment 2679990

Sent using Jamii Forums mobile app
Airbus A350
 
NDEGE YA KWANZA KUUNGANISHWA TANZANIA

(Oktoba 12, 2023)
Tanzania imeanza safari ya kuzindua ndege yake ya kwanza kabisa kutengenezwa nyumbani.
Kampuni ya "Airplanes Africa Limited" inazindua ndege ya kwanza kabisa Tanzania kuunganishwa nchini katika maenesho ya #TIMEXPO 2023.

Ndege aina ya #Skyleader600 imeundwa kwa ajili ya safari za kibiashara na uwezo wa kumudu gharama ya chini ya uendeshaji.

Poa kampuni ya #AAL inapanga kupanua #Skyleader500 kwaajili ya matumizi ya kilimo.

Kampuni hiyo iliyo #Morogoro, ilionesha ndege ya kwanza kabisa kuunganishwa nchini Tanzania siku ya Jumatano. Tamasha la Skyleader 600’s lilifanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee katika Maonesho ya Kimataifa ya Wazalishaji Tanzania (TIMEXPO), yaliyofanyika katika jiji kuu la Dar es Salaam.
Ndege hiyo imeundwa kupakia watu wawili akiwemo rubani.

David Grolic, mkurugenzi wa AAL alifichua kuwa shirika lake liliamua kuchukua fursa ya mazingira mazuri ya biashara ya Tanzania, na nia ya kutumia teknolojia mpya, kwa kuanzisha kuunganisha ndege nchini.

Chanzo:
FB_IMG_1697458155030.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Siku Marubani wa Ethiopia walichapa usingizi Angani"

Mnamo 18 Agosti 2022, Ndege ya Shirika la Ethiopia, Boeing 737-800, iliyosajiliwa ET-AOB ikifanya safari ya ET-343 kutoka Khartoum (Sudan) hadi Addis Ababa (Ethiopia), ambapo ilitokea marubani kulala usingizi ikiwa usawa wa futi 37,000.

Ndege hiyo iliendelea kupita usawa wa kuanza kuteremka ikidumisha usawa wa 37,000 na iliendelea kupita kituo cha kutua uwanjani wa ndege njia namba 25L bila kushuka.

Kituo cha kuongoza ndege (ATC) ilijaribu kuwasiliana na marubani mara kadhaa bila mafanikio.

Baada ya kupita nje ya uwanja wa ndege mfumo wa kujiendesha ndege (Autopilot) ulijizima ambapo kengele iliwaamsha marubani kisha waliongoza ndege ili kutua kwa usalama kwenye njia ya 25L kama dakika 25 baadae.

Ndege hiyo ilibaki ardhini kwa takriban saa 2.5 kabla ya kuondoka kwa safari yake inayofuata iliandika #AviationHerald.

Siku mbili mbele marubani hao walisitishwa majukumu kupisha uchunguzi.

Taarifa ya:
FB_IMG_1698316617773.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
JE, UNAIFAHAMU KAZI YA "WINDSOCK?"

#Windsock ni kifuata upepo au koni ya upepo.
Ni mfano wa mfuko duara uliotengenezwa kwa kitambaa maalum chenye umbile la mfano wa Soksi "Sock" kubwa.
Windsock inaweza kutumika kama mwongozo wa msingi kuhusu uelekeo wa upepo na kasi.

Marubani na waongoza Ndege hutumia kifaa hiki na vingine kama #windvane kufahamu taarifa za uelekeo na kasi ya upepo katika viwanja vya ndege ili kushauri upande ambao ndege inatakiwa kuruka au rubani kuchagua mbinu ya kupaa ili kukinzana na msukumo.
Mara nyingi ndege hupaa kufuata upepo unapotokea sio unapoelekea.

Katika viwanja vya ndege vingi windsock huwa ina angazwa na taa usiku iwe zilizoizunguka au iliyowekwa kwenye nguzo inayoangaza ndani yake.

Mara zote upepo unapotokea ni kinyume cha windsock inapoelekea.
kwa hivyo upepo unapotokea kaskazini windsock itaonyesha kuelekea/kupepea kusini.

Windsock huwa inanyanyuka pale upepo unapovuma na kuinama pale upepo unapokuwa mdogo au hakuna mvumo.

Mistari inayoonekana kwa rangi ya machungwa na nyeupe sio urembo bali hutumika kusaidia kukadiria kasi ya upepo.
Kila mstari unaashiria kasi ya mafundo 3 ya upepo au kilomita 5.5

Mfano:
Windsock ikinyanyuka mstari wa kwanza tu wenye rangi ya machungwa tambua upepo una kasi ya fundo 3 (3 knots) au kilomita 5.5 kwa saa.

Ikinyanyuka mstari unaofuata wa pili mweupe tambua upepo una kasi ya fundo 6 au kilomita 11 kwa saa.

Ikinyanyuka mstari wa tatu wenye rangi nyingine ya chungwa kasi ya upepo ni fundo 9 au kilomita 16 kwa saa.

Inaendelea hivyo hadi mstari wa nne mweupe au mstari wa mwisho wa tano wenye rangi ya chungwa ambao kasi ya upepo ni fundo 15 sawa na kilomita 28 kwa saa.

kumbuka Windsock haijawekwa tu kama bendera za mashabiki wa soka, bali imeainishwa katika kiambatisho cha 14 kwenye shirikisho la usafiri wa anga ulimwenguni #ICAO na katika kanuni, miongozo au sheria za wadhibiti kutoka nchi tofauti ulimwenguni.

Muongozo:
#skybrary

[emoji2398] Aviation Media Tz

Picha:
Mtandaoni
FB_IMG_1698744708936.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
𝗝𝗘, 𝗞𝗨𝗡𝗔 𝗨𝗛𝗨𝗦𝗜𝗔𝗡𝗢 𝗞𝗔𝗧𝗜 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗜𝗥𝗜 𝗭𝗔 𝗡𝗗𝗘𝗚𝗘 𝗡𝗔 𝗜𝗡𝗝𝗜𝗡𝗜?

Marudio.

Magurudumu (Tairi) za ndege hazina kiunganisho wala husiano na injini za ndege iwe Pangaboi au Jeti.
Gurudumu huzunguka huru kama toroli au au kiti cha kusukuma "wheel chair" isipokuwa tu zimefungwa mifumo ya breki, mifumo wa kona na mifumo ya 'hydraulic' ya kuvuta tairi ndani au kutoa nje kwa ndege zinazoingiza tairi.

Magurudumu ya ndege ni huru 'freewheel' ambayo hufuata ndege inaposukumwa injini hivyo hakuna 'propeller shaft, 'chain' wala 'belt' yeyote na haifanani na mifumo ya uendeshaji wa vyombo vingine vya moto kama magari.

Kazi ya injini za ndege kusukuma upepo nyuma kwa kasi kubwa ambayo hupelekea ndege kwenda mbele (action & reaction)
Unaweza sema injini za ndege za jeti ni mfano wa 'compressor' kubwa za kufua upepo, kukusanya na kusukuma nyuma kwa kuongezwa nguvu ya mafuta na viwashio, na kwa pangaboi pia hutumia panga zake kusukuma hewa nyuma.
Tafuta makala uchambuzi za nyuma inayosema 'aina ya injini za ndege'

Mara nyingine utaona trekta maalumu (tow truck/tug) hutumika kusukuma au kuvuta ndege kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Kama ilivyo panga za meli chini kusukuma maji kwenda nyuma kisha Chombo kuelekea mbele, pia hali ndivyo ilivyo kwa ndege kusukuma upepo nyuma ili ndege kuelekea mbele.

Kwa ngivu ya upepo unaovutwa, kufuliwa na kusukumwa nyuma ya ndege (Jet blast) mfano kwenye #Boeing777, Boeing787, #Boeing747, #Airbus380, #Airbus330 n.k unaweza kuangusha Gari la ukubwa wa 'Bus endapo likatiza nyuma ya ndege ikiwa imewasha injini katika nguvu ya mwisho (full power).
Kwa binaadamu ni sawa na mbu kukatiza mbele ya feni.

Kumbuka ndege inapopaa tairi hazina matumizi tena hadi wakati wa kutua.
Mfumo mzima wa tairi za ndege unaitwa 'Landing Gear'

#Admin,
[emoji2398]Aviation Media Tanzania

Picha kwa Hisani ya Mtandao.
FB_IMG_1699255653356.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mujibu wa mtandao wa simleflying.com, tovuti, majarida ya mashirika ya ndege, kuhusu usafirishaji wa shehena za mizigo, ndege aina ya Boeing B767-300F ndio chaguo la bei rahisi zaidi la U$220.3 milioni, ikifuatiwa na Boeing B777F (U$352.3mn).

Kwa sasa ndege ya injini Nne Boeing B747-8F ndiyo ndege ya bei ghali zaidi ya kubeba mizigo ya Boeing ya U$419.2 milioni lakini itapendeza kuona jinsi gharama ya 777XF (777-8F) inavyojipanga baadaye.
Katika kundi hilo, ndege za abiria ni nafuu kidogo kuliko za mizigo.

Baadhi ya ndege za mizigo kwa Mashirika ya ndege matatu ya Ethiopian Airlines, Kenya Airways na Air Tanzania;

Ethiopian Airlines
09 Boeing B777-200LRF (Tani 100 -105)
02 Boeing B767-300F (Tani 52)
04 Boeing B737-800F (Tani 23)

Air Tanzania
01 Boeing B767-300F (Tani 52)

Kenya Airways
02 Boeing 737-300SF (Tani 18)

Zaidi:
FB_IMG_1699263823706.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni siku Tisa tu zimebaki kuelekea Maonesho ya usafiri wa Anga ya Dubai, 13, Novemba 2023.

[emoji991]:
Saeed.h
@Aerosaeed
FB_IMG_1699280361207.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom