Mada maalum ya ndege toka FB

Mada maalum ya ndege toka FB

Michael Ngaleku Shirima (aliyezaliwa 1943) alikuwa ni Mtanzania mfanyabiashara, mjasiriamali, na mfadhili. Yeye ndiye mwanzilishi na mwenyekiti wa Precision Air, shirika kubwa la ndege linalomilikiwa na watu binafsi nchini Tanzania.
Michael Shirima alianzisha Precision Air imnamo mwaka 1993.
Ilianza kama kampuni ya kibinafsi ya kukodisha ndege inayoendesha ndege aina ya Piper Aztec yenye viti vitano.
Biashara yake ya awali ilihusu kutoa mawasiliano kwa watalii wanaotembelea vivutio vya asili vya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Kreta ya Ngorongoro, kaskazini mwa Tanzania, Kisiwa cha Zanzibar katika Bahari ya Hindi na maeneo mengine ya nchi kutoka Arusha mjini kama kitovu chake.

Kuongezeka kwa mahitaji ya huduma za usafiri wa anga wakati nchi ilipoanza uchumi wa soko huria kuliifanya Precision Air kufanya safari zake zilizopangwa na kudumisha Arusha kama kituo chake kikuu.
Safari za kwanza za ndege zilipangwa kwa kutumia ndege ya injini moja ya viti saba moja Cessna 207, Cessna 402 yenye viti saba, Cessna 404 ya watu kumi na moja na LET 410 ya watu kumi na tisa hadi katikati ya miaka ya 1990 wakati shirika la ndege lilianzisha ndege kubwa za ATR.

Mnamo 2003, Kenya Airways, shirika kubwa zaidi la ndege katika Afrika Mashariki, lilipata umiliki wa 49% katika Precision Air kwa pesa taslimu ya Dola za Marekani milioni 2.
Precision Air ina makao yake makuu jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania.
Mnamo Oktoba 2011, Precision Air ilimiliki hisa asilimia 30.35 katika hisa za shirika la ndege, katika toleo la awali la umma kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam.
Kufikia Juni 2012, ripoti za vyombo vya habari nchini Kenya zilionyesha kuwa Michael Shirima ndiye mwanahisa mkubwa zaidi katika hisa za shirika la ndege akiwa na asilimia 42.91 ya hisa.

Michael Ngaleku Shirima pia ni mwanzilishi na mmiliki wa Kituo cha watoto yatima cha Cornel Ngaleku, kilichopo kaskazini mwa Tanzania.

Pumzika kwa Amani #Michael #Ngaleku #Shirima

Chanzo:
@https://www.michael-shirima.com/
@ Wikipedia/shirima
Precisionair Tanzania
FB_IMG_1686456691992.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa majina inaitwa, Steering Hand Control au #Tiller. Hiki ni kifaa kinachotumika kukata kona kulia, kushoto na kunyoosha ndege pindi inapokua inatembea ardhini mithili ya gari.

Pindi ndege inapokua angani, huwa haitumii Tiller kukunja kona.
Kwenye baadhi ya ndege hivi vifaa huwa viwili na katika ndege nyengine huwa moja.
Ndege ambazo zina Steering Hand control mbili, Rubani kiongozi na rubani msaidizi wote wanaweza kuidhibiti ndege pindi inapokuwa ardhini.

Kwa ndege ambazo ipo moja, kifaa hiki huwekwa upande anaokaa rubani kiongozi tu na huwa ni yeye pekee mwenye uwezo wa kutumia kidhibiti ndege ardhini.

Mtaalamu wetu:
Maridadi Farid
FB_IMG_1686482629061.jpg
FB_IMG_1686482625570.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
After 45 years in the skies and 23,567 total flight hours, Captain Ernesto Carrilho of Mozambique Express has retired. AAG wishes him a happy retirement. #ProudlyAfrican
FB_IMG_1686759834127.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
𝗡𝗗𝗘𝗚𝗘 𝗛𝗨𝗞𝗔𝗧𝗔𝗝𝗘 𝗞𝗢𝗡𝗔 𝗔𝗡𝗚𝗔𝗡𝗜?

{Ufafanuzi mwepesi}

Ndege inakata kona kutumia pedeli mbili {kushoto na kulia} anazokanyaga rubani.

Pedeli hizo {#foot_pedal} ndiyo zinakata kona tairi ya mbele na kielekezi cha mkia uliosimama {#rudder}.

Rubani akikanyaga pedeli ya kushoto tairi itakata kushoto na kinyume chake.
Lakini pedeli hizo zimegawanyika mara mbili, endapo zikikanyangwa kwa upande wa juu unapata #brake za tairi.

Kwahiyo rubani anatumia upande wa visigino vyake kusukuma 'pedal' ili kukata kona au kukanyaga pedal hizo kwa upande wa vidole vya miguu kukamata 'brake'

Inapokuwa chini ndege inakata kona kwa kutumia tairi ya mbele (ukiacha ndege za #trail_dragger} na ikiwa angani tairi haina kazi tena na inatumika 'rudder' pekee kukata kona kwa kukinzana na upepo upande wa kushoto au kulia mkiani.

Kwa upande wa mbawa kuna vielekezi vilivyo karibu na ncha kulia na kushoto viitwavyo "#ailerons" ambavyo vinafanya kazi kwa kutumia usukani wa ndege {#steering_yoke/#flight_yoke} kukata kulia au kushoto.
Pia usukani huu ukivuta au kusukuma ndiyo unainamisha au kuinua pua ya ndege kwa kutumia kielekezi cha mkia uliolala {#elevator}

Vielekezi vya mbawa 'Ailerons' hutumika zaidi angani wakati ndege inahitaji kukata kona kwa kulala {#bank} na mara nyingi vinafanya kazi kinyume.

Ndege ikitaka kukata kona ya kulia basi kielekezi cha mbawa ya kulia 'Aileron' kitainuka juu kikinzana na hewa ipitayo na kulazimisha mbawa kwenda chini wakati huo kielekezi cha kushoto kitainama chini kukinzana na hewa ipitayo chini na kusukuma mbawa juu.
Hapo utaona ndege inalala upande wa kulia na kinyume chake.

Ndege huwa haikamiliki kukata kona kwa kulala kulia au kushoto, hapo itakuwa inateleza tu angani kuelekea mbele {#slipping} kama vile gari iliyokata kona ghafla kwenye utelezi.

Kwasababu hiyo rubani anakata kona yake vizuri kwa kujumuisha pamoja vielekezi vyote "Ailerons" kulaza ndege upande aliokusudia, atasukuma pedeli ya upande aliolazia ndege ili rudder mkiani ipeleke pua ndege alipokusudia.

Hapo utaona ndege inakata kona nzuri kwa kulala upande.

Uchambuzi ujao utakuwa kuhusu vifaa vinavyosaidia ndege kupaa na kutua kwa mwendo mdogo "#lifting devices"

{#Flaps & Slats} na brake za kukinzana na upepo {#speedbrake au #Spoilers}

Tafsiri kutoka:
#boldmethod
#Aerodynamics_syllabus

Picha kw hisani ya mtandao.
FB_IMG_1687440823292.jpg
FB_IMG_1687440826452.jpg
FB_IMG_1687440829276.jpg

Picha kw hisani ya mtandao.View attachment 2665463View attachment 2665464View attachment 2665465

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli lakini hii ni basics. Kwa ndege kubwa angani katika spidi kubwa ukitumia rudder itakupa deflection kubwa. Kwa lugha rahisi katika spidi kubwa angani, ndege hutumia ailrons na baadhi ya spoilers. Hivyo ndege hukata kona ilikoinamia.
 
"𝙉𝙙𝙚𝙜𝙚 𝙮𝙖 𝙞𝙣𝙟𝙞𝙣𝙞 𝙣𝙣𝙚 𝙮𝙖 𝙋-3 𝙊𝙧𝙞𝙤𝙣, 𝙖𝙢𝙗𝙖𝙮𝙤 𝙞𝙡𝙞𝙜𝙪𝙣𝙙𝙪𝙖 𝙠𝙚𝙡𝙚𝙡𝙚 𝙮𝙖 𝙠𝙞𝙨𝙝𝙞𝙣𝙙𝙤 𝙅𝙪𝙢𝙖𝙩𝙖𝙣𝙤, 𝙞𝙡𝙞𝙞𝙣𝙜𝙞𝙖 𝙠𝙬𝙖 𝙢𝙖𝙧𝙖 𝙮𝙖 𝙠𝙬𝙖𝙣𝙯𝙖 𝙢𝙣𝙖𝙢𝙤 1962 𝙣𝙖 𝙞𝙣𝙖𝙩𝙚𝙜𝙚𝙢𝙚𝙖 𝙣𝙙𝙚𝙜𝙚 𝙮𝙖 𝙇𝙤𝙘𝙠𝙝𝙚𝙚𝙙 𝙀𝙡𝙚𝙘𝙩𝙧𝙖.

𝙉𝙙𝙚𝙜𝙚 𝙞𝙡𝙞𝙜𝙪𝙣𝙙𝙪𝙖 𝙠𝙚𝙡𝙚𝙡𝙚 𝙗𝙖𝙖𝙙𝙖 𝙮𝙖 𝙠𝙪𝙖𝙣𝙜𝙪𝙨𝙝𝙖 𝙢𝙖𝙗𝙤𝙮𝙖 𝙮𝙖 𝙨𝙤𝙣𝙖𝙧, 𝙖𝙢𝙗𝙖𝙮𝙤 𝙮𝙖𝙡𝙞𝙩𝙚𝙡𝙚𝙯𝙖 𝙟𝙪𝙪 𝙮𝙖 𝙗𝙖𝙝𝙖𝙧𝙞, 𝙞𝙠𝙞𝙨𝙞𝙠𝙞𝙡𝙞𝙯𝙖 𝙨𝙖𝙪𝙩𝙞 𝙖𝙢𝙗𝙖𝙯𝙤 𝙖𝙨𝙞𝙡𝙞 𝙞𝙨𝙞𝙣𝙜𝙚𝙬𝙚𝙯𝙚𝙠𝙖𝙣𝙖 𝙠𝙪𝙩𝙤𝙖.

𝙄𝙡𝙞𝙥𝙤𝙠𝙚𝙖 𝙠𝙚𝙡𝙚𝙡𝙚 𝙯𝙖 𝙠𝙖𝙬𝙖𝙞𝙙𝙖 𝙯𝙖 𝙠𝙞𝙨𝙝𝙞𝙣𝙙𝙤 𝙠𝙬𝙖 𝙢𝙪𝙙𝙖 𝙬𝙖 𝙙𝙖𝙠𝙞𝙠𝙖 30, 𝙟𝙖𝙢𝙗𝙤 𝙖𝙢𝙗𝙖𝙡𝙤 𝙬𝙖𝙩𝙖𝙖𝙡𝙖𝙢𝙪 𝙬𝙖𝙣𝙖𝙥𝙚𝙣𝙙𝙚𝙠𝙚𝙯𝙖 𝙣𝙞 𝙞𝙨𝙝𝙖𝙧𝙖 𝙠𝙬𝙖𝙢𝙗𝙖 𝙬𝙖𝙣𝙖𝙛𝙖𝙣𝙮𝙬𝙖 𝙣𝙖 𝙬𝙖𝙣𝙖𝙙𝙖𝙢𝙪.

"𝙐𝙠𝙬𝙚𝙡𝙞 𝙠𝙬𝙖𝙢𝙗𝙖 𝙞𝙨𝙝𝙖𝙧𝙖 𝙮𝙖 𝙨𝙖𝙪𝙩𝙞 𝙯𝙞𝙢𝙚𝙩𝙤𝙛𝙖𝙪𝙩𝙞𝙖𝙣𝙖 𝙠𝙬𝙖 𝙙𝙖𝙠𝙞𝙠𝙖 30 𝙣𝙖 𝙣𝙞 𝙞𝙨𝙝𝙖𝙧𝙖 𝙣𝙯𝙪𝙧𝙞," 𝙖𝙣𝙖𝙨𝙚𝙢𝙖 𝙅𝙖𝙢𝙞𝙚 𝙋𝙧𝙞𝙣𝙜𝙡𝙚, 𝙢𝙨𝙤𝙢𝙖𝙟𝙞 𝙬𝙖 𝙨𝙖𝙮𝙖𝙣𝙨𝙞 𝙮𝙖 𝙠𝙞𝙟𝙞𝙤𝙜𝙧𝙖𝙛𝙞𝙖 𝙠𝙖𝙩𝙞𝙠𝙖 𝘾𝙝𝙪𝙤 𝙆𝙞𝙠𝙪𝙪 𝙘𝙝𝙖 𝙆𝙚𝙚𝙡𝙚 𝙣𝙘𝙝𝙞𝙣𝙞 𝙐𝙞𝙣𝙜𝙚𝙧𝙚𝙯𝙖.

"𝙋𝙧𝙤𝙥𝙚𝙡𝙖 𝙮𝙖 𝙢𝙚𝙡𝙞 𝙖𝙢𝙗𝙖𝙮𝙤 𝙞𝙣𝙖𝙬𝙚𝙯𝙖 𝙠𝙪𝙚𝙣𝙙𝙚𝙡𝙚𝙖. 𝙄𝙨𝙝𝙖𝙧𝙖 𝙮𝙖 𝙨𝙖𝙪𝙩𝙞 𝙞𝙣𝙖𝙨𝙖𝙛𝙞𝙧𝙞 𝙢𝙗𝙖𝙡𝙞 𝙨𝙖𝙣𝙖 𝙢𝙖𝙟𝙞𝙣𝙞, 𝙠𝙬𝙖 𝙝𝙞𝙫𝙮𝙤 𝙝𝙞𝙮𝙤 𝙣𝙞 𝙝𝙖𝙗𝙖𝙧𝙞 𝙣𝙟𝙚𝙢𝙖 𝙣𝙖 𝙢𝙗𝙖𝙮𝙖.

𝙐𝙩𝙖𝙝𝙞𝙩𝙖𝙟𝙞 𝙖𝙣𝙜𝙖𝙡𝙖𝙪 𝙢𝙖𝙗𝙤𝙮𝙖 𝙢𝙖𝙩𝙖𝙩𝙪 𝙠𝙖𝙩𝙞 𝙮𝙖 𝙝𝙖𝙮𝙤 𝙩𝙪𝙡𝙞 𝙞𝙡𝙞 𝙠𝙪𝙬𝙚𝙯𝙖 𝙠𝙪𝙜𝙚𝙪𝙯𝙖 𝙘𝙝𝙖𝙣𝙯𝙤 𝙘𝙝𝙖 𝙨𝙖𝙪𝙩𝙞 𝙠𝙪𝙬𝙖 𝙥𝙚𝙢𝙗𝙚 𝙩𝙖𝙩𝙪 𝙞𝙡𝙞 𝙠𝙪𝙥𝙖𝙩𝙖 𝙚𝙣𝙚𝙤."

BBC Swahili
FB_IMG_1687496269578.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Uasi wa Wagner wa Juni 23 - 24, ulileta uharibifu katika kikosi cha anga cha Urusi. Kwa mujibu wa chanzo huru, helikopta mbili za kivita aina ya Ka-52 na Mi-35, helikopta tatu aina ya Mi-8MTPR, na gari moja la kijeshi la Mi-8, ya ulinzi aina ya II-22M imedunguliwa.

Taarifa hizi ziliripotiwa na wandishi habari wa Urusi na wana bloga. Kwa mujibu wa timu ya migogoro na intelejinsia, inawezekana kwamba helikopta nyingine aina ya Mi-8MTPR ilidunguliwa karibu na Ligansk Juni 23, ingawa hakuna taarifa za kutosha kuhusu tukio hili. Pia, haikuwa wazi ni watu wangapi walifariki"

BBC Swahili
FB_IMG_1687965824139.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Breaking: Delta Flight Manages Successful Landing In Charlotte Without Nose Gear

FB_IMG_1688108769410.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika kipindi cha vita ya Pili ya Dunia Ujerumani alitengeneza uwanja cha ndege bandia (Fake Airport) zikiwemo Ndege bandia za mbao, Magari n.k ili kumchanganya adui yake (Uingereza na washirika) endapo watafanya mashambulizi kutoka angani.

Hata hivyo Uingereza illipata taarifa za kiintelijensia na kusubiri hadi walipomaliza ujenzi kisha ikatuma ndege kwenda kudondosha Bomu kubwa la bandia la mbao.

Ilichukuwa muda kiasi kwa wanajeshi wa Ujerumani kujikusanya tena upya kutafuta bomu ambalo halikulipuka na kugundua lilikuwa bandia.

Chanzo:
Soga maarufu za mtandaoni.
FB_IMG_1688278294463.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
𝗞𝗮𝗯𝗹𝗮 𝘆𝗮 𝗸𝘂𝗮𝗻𝗱𝗶𝗸𝗮 𝗵𝗶𝘇𝗶 𝘁𝗮𝗮𝗿𝗶𝗳𝗮 𝗹𝗮𝘇𝗶𝗺𝗮 𝘁𝘂𝗳𝗮𝗵𝗮𝗺𝘂 𝗸𝘄𝗮𝗻𝘇𝗮, 𝗸𝘄𝗮𝗺𝗯𝗮, 𝗡𝗱𝗲𝗴𝗲 𝗻𝗶 𝘁𝗼𝗳𝗮𝘂𝘁𝗶 𝗻𝗮 𝗕𝘂𝘀.
𝗟𝗶𝗻𝗮𝗽𝗼𝘁𝗼𝗸𝗲𝗮 𝘁𝗮𝘁𝗶𝘇𝗼 𝗹𝗮 𝗸𝗶𝘂𝗳𝘂𝗻𝗱𝗶 𝗵𝗮𝘁𝗮 𝗹𝗶𝘄𝗲 𝗱𝗼𝗴𝗼 𝗸𝗶𝗮𝘀𝗶 𝗴𝗮𝗻𝗶, 𝗸𝘄𝗮 𝘁𝗮𝗵𝗮𝗱𝗵𝗮𝗹𝗶 𝘇𝗮 𝗸𝗶𝘂𝘀𝗮𝗹𝗮𝗺𝗮 𝗻𝗶 𝗸𝗮𝘄𝗮𝗶𝗱𝗮 𝗻𝗱𝗲𝗴𝗲 𝗸𝘂𝘁𝘂𝗮 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝘂𝘄𝗮𝗻𝗷𝗮 𝘄𝗮 𝗻𝗱𝗲𝗴𝗲 𝘂𝗹𝗶𝗼 𝗸𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝗶𝗹𝗶 𝗸𝘂𝘁𝗮𝘁𝘂𝗮 𝘁𝗮𝘁𝗶𝘇𝗼 𝗹𝗶𝗹𝗶𝗷𝗶𝗶𝘁𝗼𝗸𝗲𝘇𝗮 𝗸𝗮𝗯𝗹𝗮 𝗵𝗮𝗹𝗶𝗷𝗮𝗹𝗲𝘁𝗮 𝘀𝗵𝗶𝗱𝗮 𝗻𝘆𝗶𝗻𝗴𝗶𝗻𝗲.

"Tahadhari za kiusalama ndiyo Tamaduni katika sekta ya usafiri wa anga"
FB_IMG_1688370041669.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cockpit au Flight deck ni eneo ambalo kwa kawaida mara nyingi huwa mbele au karibu na mbele ya ndege au chombo cha angani, ambapo rubani hutumia hudhibiti ndege.
Baadhi ya ndege za awali 'cockpit' unaweza kuikuta katikati ya ndege.
Je, unaweza kutambua pichani ni 'cockpit'ya ndege gani?
FB_IMG_1688631650915.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumezoea kuona Ndegevita nyingi za vyumba viwili vya marubani huwa za mafunzo (Combat Training Aircraft), ambapo huketi mwalimu na mwanafunzi wake.
Je, hii pia yaweza kuwa ya mafunzo?

Picha:
BBC Swahili
FB_IMG_1689917237485.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
#Beechcraft #Starship ni ndege ya injini mbili ya pangaboi 'turboprop' iliyoundwa na Beechcraft katika miaka ya 1980 na 90.
Ilikuwa mojawapo ya ndege za kwanza kutumia malighafi mchanganyiko na fremu yake yote iliyotengenezwa kwa nyuzi za kaboni.

Mbinu hii ya ujenzi iliruhusu muundo mzuri wa tabiahewa "aerodynamic" ambayo ilichangia Starship kuwa na kasi ya juu na ufanisi wa mafuta.
Hata hivyo, kutokana na gharama yake ya juu na mahitaji machache ya soko, uzalishaji wa Starship ulisitishwa baada ya ndege 53 pekee kujengwa.
Leo, Ndege nne zilizosalia na kukidhi vigezo vya kuruka 'airworthness' hutafutwa sana na wapenzi anga kote ulimwenguni na kila wakati hugeuza vichwa kuzitafuta.

Chanzo:
Dylan Phelps
FB_IMG_1690359387407.jpg
FB_IMG_1690359384798.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mashirika ya Ndege ya American Airlines, Delta Air Lines, na United Airlines zote zina magari wanayotumia kusaidia baadhi ya abiria wao wa ngazi ya juu kufanya miunganisho na kuwahi ndege kwenye viwanja vya ndege vikubwa.
Lakini, Delta pekee ndiyo inayotumia Porsche 918 Spyder Hypercar kwa kusafirisha.

Porsche 918 Hypercar ni Gari la kisasa zaidi la michezo linagharimu zaidi ya dola za kimarekani milioni moja.

FB_IMG_1690653832467.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom