Mada maalum ya ndege toka FB

"FARASI ATOROKA NJE YA KIBANDA ANGANI"

Ndege inayoendeshwa na shirika maalum la ndege la Air Atlanta Icelandic, ilikuwa ikielekea Liege nchini Ubelgiji kabla ya kulazimika kurejea katika uwanja wake wa ndege ilipotoka huko New York baada ya farasi kutoroka nje ya kibanda chake katika sehemu ya kubebea mizigo na kuanza kukimbia ndani ya ndege.

Ndege hiyo aina ya Boeing 747 yenye usajili TF-AMM, ilikuwa ikisafiri kwa umbali wa futi 31,000 juu ya Boston wakati ambapo kwa ghafla farasi mmoja alitoka kwenye kontena lake.

Marubani walilazimika kumwaga tani 20 za mafuta ili kupunguza uzito wa ndege kabla ya kutua kwa usalama.

Picha ni kwa lengo la kufikisha ujumbe tu.

Chanzo:


Sent using Jamii Forums mobile app
 
"ETHIOPIA YAAGIZA ZAIDI YA NDEGE 30"

Siku ya pili katika Maonesho ya usafiri wa anga #DubaiAirshow2023,
Shirika la Ndege la Ethiopia limekubali kuagiza ndege 11 aina ya Boeing B787-9 Dreamliner na 20 aina ya Boeing B737 MAX 8 na fursa ya ndege nyingine kati ya 15 na 21 za ziada.

Mkataba huu unawakilisha ununuzi mkubwa zaidi kuwahi kutokea wa ndege za Boeing katika historia ya Afrika. Ethiopian huendesha idadi kubwa zaidi ya mchanganyiko wa ndege za Boeing 787-8 na B787-9 (Dreamliner) barani Afrika za Dreamliner.

Chanzo:
Aeronews
DubaiAirshow
#das2023 #das23

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukirudi nyuma kiasi tunaona jinsi Helikopta zilivyokuwa zinapitia majaribio ya uvumilivu katika hali ya hewa ya mvua na barafu.

@NASA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Timu ya watafiti katika Chuo Kikuu cha Washington State (WSU) imeunda nyuki wa roboti anayeweza kuruka kwa utulivu katika pande zote.

Mfano wa Nyuki++ ni wa kwanza kufikia digrii sita za harakati ambazo mdudu wa kawaida anayeruka huonyesha.

Nyuki++ imetengenezwa kwa nyuzinyuzi za kaboni na mylar, na ina mabawa manne ambayo yanadhibitiwa na vitendaji vinne vyepesi.
Watafiti walitengeneza kidhibiti kipya kinachoruhusu roboti kujipinda kwa njia iliyodhibitiwa, ambayo ni kazi ngumu kwa roboti zinazoruka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je, unajua kwamba injini namba 2 (ile unayoiona kwenye mkia) ya Boeing 727 na trijeti nyingi (isipokuwa DC-10) haipo kabisa juu ya fuselage?
Injini ziko ndani ya fuselage, na bomba la mfumo wa uvutaji hewa umetokea nje mfano wa herufu S (S-duct)

SOMA ZAIDI: The S-Duct Intake of the Lockheed Tristar and Boeing 727 [emoji328]: Aldo Bidini Katika picha: Dassault Falcon 900EX

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TAA ZA NDEGE

Mifumo yote ya taa za vyombo vya moto inakusudia kupunguza uwezekano wa kugongana/Usalama wa chombo na watu.

Taa za ndege pia ni hivyo, uifanya ionekane zaidi na ndege nyengine au vyombo vingine vya moto/watu, wakati ikiwa chini au kupaa angani.

TAA ZA URAMBAZAJI
(#Navigation_Lights)
Hizi zinajumuisha taa mbili hadi tatu, nyekundu kwenye ncha ya mbawa ya kushoto, taa ya kijani ncha ya mbawa ya kulia na nyengine taa nyeupe kwenye mkia wa ndege.

Hapa ngoja nishuke kidogo..
Taa hizi mara nyingi huwa zinatoa taarifa kwa rubani/ chombo kingine angani kuwa ndege ipo upande gani.

Mfano:
Hasa usiku,


KIMULIMULI
(#Beacon)
Hizi ni taa zenye rangi nyekundu na zinaweza kuwaka au kuzunguka ili kutoa mwangaza wa onyo na inaweza kuwa juu ya ndege, tumboni au juu ya mkia.
Kifupi taa nyekundu ya kimulimuli huwa inatuonya au kutupa tahadhari juu ya hatari au kutosogelea chombo/sehemu husika.

'FLASHI'
(#Strobe)
Au tunaitaga "mweku mweku" wakuu au sio?
Hizi taa ni nyeupe zenye mwangaza mkali wa kuwaka na kuzima au kupokezana (flash)
Taa hizi kawaida huwekwa karibu na ncha za mbawa pia inaweza kuwa na mkiani.
Hizi zinaongeza muonekano wa ndege hata ikiwa mbali na unaweza kutofautisha kati ya ndege na nyota.
Usiku usipokuwa makini unaweza kuona ndege ukajua nyota.

TAA ZA KUTEMBEA NDEGE
(#Taxi_Lights)
Hizi ni taa za kiwango cha kati ambazo zinaweza kuwekwa kwenye pua ya ndege au mwanzo wa mbawa karibu na inapokutana na kiwiliwili cha ndege.
Hizi kazi yake kumulika ndege inapotembea kwenye njia zake za mchepuko kutoka barabara kuu (taxiways)

TAA ZA KUFUATA KONA
(#Runway_Turnoff_Light)
Taa za Turnoff zinafanana na taa za kutembea ndege isipokuwa taa hizi huweza kupinda kuangaza/kumulika kule tairi la mbele linapokata kona.

TAA ZA KUTUA
(#landing_Light)
Hizi ni taa zenye mwangaza wa kiwango cha juu zinazotumika kuangazia barabara ya kuruka na kutua na pia kuwezesha ndege kuonekana na marubani wengine kirahisi inakuwa inapaa au na kutua.
Huwa zinamulika mbele kwa mwangaza mkali zaidi.

TAA KAGUZI MBAWA
(#Wing_Inspection_Light)
Taa hizi zenye mwangaza wa kutosha zimewekwa pembeni ya kiwiliwili (fuselage)na zinamulika nyuma kuangazia mbawa pamoja na injini.

TAA ZA NEMBO
(#Logo_Lights)
Hizi ni taa zinazomulika nembo ya ndege mkiani.
Mashirika na makampuni mengi ya usafiri wa anga hupenda kuweka nembo zao kwenye mkia uliosimama wima.

#Admin

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NI MUDA GANI NDEGE HUBADILISHWA TAIRI?

Tairi za ndege huweza kubadilishwa pale zinapokuwa zimetumika kutua kuanzia mara 100 hadi 400 kutegemea na aina ya ndege na uzito.
Lakini idadi ya kutua haimaanishi kuwa ndiyo kipimo kamili.
Tairi inaweza kubadilishwa kama imeonekana ina nyufa, imeisha, imelika, imekatika, kupata pancha n.k

Lakini pia idadi ya matumizi ya kutua kwa tairi za ndege inaweza kupungua kwa kuathiriwa na sababu kama;
hali ya hewa, kutua kwanguvu, kutua kwenye upepo unaosukuma ndege ubavu, kutumia mfumo wa kuzuia uterezi, barabara mbovu, matumizi makali ya breki, hivi vyote vina athari katika kufupisha maisha ya tairi.

Mfano tairi za #Airbus380 yanadumu kutua kwa takriban hadi mara 300, ambayo ni miezi sita ya operesheni.

Baadhi ya Mashirika ya ndege sasa uvesha upya lapu la kashata kwenye tairi (retread) ili kupunguza gharama kununua tairi mpya.
Baadhi ya matairi yaliyobandikwa lapu yanadumu kutua hadi mara 100 zaidi.

Kutegemea na ndege, ukubwa na aina ya tairi, gharama ya kununua tairi moja kwa makadirio inaweza kuwa kati ya 100,000 hadi 15,000,000.

Ndege ndogo kabisa huwa na tairi ndogo mfano wa bajaj na kuongezeka umbile kulingana na ukubwa wa ndege.
Lakini tairi kubwa kabisa kuwahi kutokea ni kutoka Convair B-36 ambalo lilikuwa zaidi ya futi 6.
Ndege nyingi uanzia tairi 03 hadi 32 za #Antonov225.

Mamlaka za usafiri wa anga na mashirika husika pia ndiyo yenye wajibu kusimamia sera na kanuni za udhibiti wa ubora na usalama wa tairi ili kutokuleta madhara.

Chanzo:
Aviation forum

[emoji328]
Swiss

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ile iliyofyonza maji na kuteleza Mwanza miaka ya 2009 kama sikosei ilishatengenezwa au iliishia hapo
 
Kwann imwage mafut
Au unamaanish ndege ikianz kupaa inawez ku lift mzgo mkubwa (fully tank ) na ikiwa haijaend mbali (mafuta mengi) haiwez tua kwa usalama
 
Kasi ya sauti ni kama maili 768 kwa saa (kilomita 1,236 kwa saa) kwenye usawa wa bahari.
Kasi hizi zinarejelewa au kujulikana kama Mach.

Nambari ya Mach ni uwiano wa kasi ya ndege na kasi ya sauti.

Wakati kasi ya ndege inapozidi kasi ya sauti, inasemekana kuvunja kizuizi cha sauti (breaking sound barrier)

Ndege ambayo inatembea chini ya kasi ya sauti wanaita "Subsonic", na ndege inayotembea zaidi kuliko Mach 1 wanaita "Supersonic"
Chombo ambacho kinatembea kasi mara tano ya sauti "Mach 5" wanaita "Hypersonic"

Leo, tunatambua ya kwamba kizuizi cha sauti (Sound barrier) ni ongezeko la ghafla la uvutaji/mburuto wa tabiahewa (aerodynamic drag) ambayo hutokea wakati kitu kinakaribia kasi ya sauti.

Mara nyingi kwa muonekano wa nje hasa kwa ndegevita za kijeshi inapokimbia kupita/kuvunja kasi moja ya sauti (Mach 1) inakuwa inapita/kuzungukwa na mvuke wa duara (Sound barrier/ Pressure wave) na kishindo cha sauti ya mlipuko.
Mara nyingine ikizidi kasi ya sauti basi utasikia ndege inapita ndipo muungurumo wa injini unafuata nyuma.

Admin/
NASA topics

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Boeing 737 Cockpit [emoji1944]
#fun [emoji3575]

#aviation #aviationphoto #aviation4u #aviationdaily #aviationlovers #aviationgeek #aviationphotography

[emoji328]: Alexey.Emk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…