"𝗕𝗜𝗥𝗗 𝗦𝗧𝗥𝗜𝗞𝗘"
𝗡𝗱𝗲𝗴𝗲 𝗸𝘂𝗴𝗼𝗻𝗴𝗮𝗻𝗮 𝗻𝗮 𝗡𝗱𝗲𝗴𝗲.
Katika usafiri wa anga neno "#birdstrike" lina maana ya ndege hai kugongana na ndege chombo.
Hali hii inaweza kutokea wakati wa ndege kupaa, kuwa angani au kutua.
Muda mwingine hali hiyo ikitokea inaweza kupelekea ndege (chombo) kupata ajali (ingawa ni mara chache), kuharibika sehemu husika kama pua, kupasua kioo na kujeruhi rubani, kuharibu injini, mbawa n.k
Kiwango wa uharibifu huo kinategemea kasi, ugumu na uzito wa ndege hai na ndege chombo, pembe inayokutana wakati wa kugongana n.k
Wanahisabati na fizikia wanakokotoa hali hilo kwa njia ifuatayo;
F=MA (Force = Mass × Acceleration)
Kwa kiswahili,
#Nguvu ni sawasawa na Ujazo wa kitu zidisha na Kasi yake.
Ndege nyingi zinaundwa na malighafi za #Aluminium au mchanganyiko wa plastiki na nyuzi za kaboni (carbon_composite) "epoxy" ili kuifanya kuwa nyepesi.
Wepesi wa ndege ni pesa katika usafiri wa anga, kwakuwa itabeba abiria wengi, mafuta zaidi, mizigo ya ziada na kwenda mbali pasipo kutumia nguvu kubwa ya injini.
Kwahiyo kitu chochote kikiwa na kasi na uzito huwa kinasababisha uharibifu pale kinapogongana na kitu kingine.
Mfano, endapo kama risasi ingekuwa inarushwa na mkono isingeleta madhara tunayoyaona leo, lakini inapofyatuliwa na bunduki, kasi huwa kubwa na madhara yake inapogongana na kitu hufanya uharibifu zaidi..
Ikiwa kasi ya ndege chombo ni kilomita 200-900 kwa saa, jumlisha na kasi ya ndege hai, basi madhara au uharibifu hutokea pale vinapokutana.
Kishindo/nguvu ya mgongano huo unaweza kufikia tani au zaidi kutegemea kasi na uzito.
Ndege nyingi zinaundwa kwa viwango maalumu vya kukabiliana na hali hiyo lakini si mara zote zinaweza kuhimili kishindo hasa pale kasi inapokuwa kubwa pamoja na uzito/ugumu wa ndege kiumbe.
Mfano,
Wanasema, mbegu ya ubuyu inaweza kupasua kichwa endapo itarushwa kwa kasi inayozidi 900km/h.
Kwa waendesha pikipiki, wanafahamu maumivu ya punje ya mchanga inapogonga usoni barabarani kwa kasi ndogo tu isiyozidi hata 100 kilomita Kwa saa.
#Admin