Mada maalum ya ndege toka FB

Mada maalum ya ndege toka FB

FB_IMG_1709636832037.jpg
FB_IMG_1709636828389.jpg
 
Ndege za American Airlines ndani ya uwanja wa ndege wa Dallas Fort Worth (DFW) muda huu.

Chanzo:
FR24
FB_IMG_1709640906997.jpg
 
Tairi iliyoanguka kutoka kwenye ndege ya United Airlines Boeing777 -200 (UA35) imeharibu baadhi ya magari ilipotua katika maegesho ya magari ya wafanyakazi katika katika uwanja wa SFO.

Chanzo:
twitter.com/aviationbrk/st…
FB_IMG_1709979158538.jpg
FB_IMG_1709979154219.jpg
FB_IMG_1709979150187.jpg
 
Ndege ya United Airlines Boeing 737 MAX 8 iliacha njia na kuchochora kwenye nyasi fupi baada ya kutua katika uwanja wa Houston hapo jana.
Hakuna ripoti ya majeruhi na mamlaka husika zinachunguza chanzo cha tukio hilo.

Chanzo:
FB_IMG_1709979041307.jpg
 
Rubani maarufu Bob Pardo, aliyesukuma F-4 iliyoharibika akiwa na F-4 Yake Juu ya Vietnam.

Pardo, ambaye F-4 yake iliharibiwa na kuvuja mafuta ingawa haikuwa mbaya sana, alisukuma Phantom nyingine kwa nyuma kwa karibu maili 90 kufikia anga yao.

Je, ni ngumu kiasi gani kwa ndege kusukuma ndege?

Soma zaidi:
FB_IMG_1709984536304.jpg
 
Ndege ya ITA Italia Trasporto Aereo Airbus A320neo imeharibika koni ya pua mbele kufuatia kugongana na ndege hai wakati wa kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Rome Fiumicino.

Ndege hiyo ilirejea kutua salama kwenye uwanja wa ndege dakika 45 baadaye.

Taarifa ya:
Aviationbrk/x
FB_IMG_1709991407224.jpg
 
Takwimu isiyo rasmi inasema, zaidi ya watu bilioni 5 hawajawahi kupanda ndege.
FB_IMG_1709995839163.jpg
 
𝗜𝗻𝗱𝗼𝗻𝗲𝘀𝗶𝗮 𝗶𝗻𝗮𝗶𝗰𝗵𝘂𝗻𝗴𝘂𝘇𝗮 𝗻𝗱𝗲𝗴𝗲 𝘆𝗮 𝗕𝗮𝘁𝗶𝗸 𝗔𝗶𝗿 𝗯𝗮𝗮𝗱𝗮 𝘆𝗮 𝗺𝗮𝗿𝘂𝗯𝗮𝗻𝗶 𝘄𝗼𝘁𝗲 𝘄𝗮𝘄𝗶𝗹𝗶 𝗸𝘂𝗽𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮𝗻𝗮 𝘄𝗮𝗸𝗶𝘄𝗮 𝘄𝗮𝗺𝗲𝗹𝗮𝗹𝗮 𝗸𝘄𝗮 𝗱𝗮𝗸𝗶𝗸𝗮 28 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮𝘁𝗶 𝘆𝗮 𝘀𝗮𝗳𝗮𝗿𝗶.

Wanaume hao wawili - ambao wote wamesimamishwa kazi kwa muda - walilala wakati wa safari ya ndege tarehe 25 Januari kutoka Sulawesi kuelekea mji mkuu Jakarta.

Mmoja wao aliripotiwa kuchoka kutokana na kusaidia kuwatunza mapacha wake wachanga.

Ndege hiyo aina ya Airbus A320 iliacha njia kwa muda lakini ikatua salama, huku abiria wote 153 na wahudumu wote wakiwa salama.

Rubani huyo mwenye umri wa miaka 32 alikuwa amemwambia rubani mwenzake kuchukua udhibiti wa ndege hiyo takriban nusu saa baada ya kupaa, akisema alihitaji kupumzika. Rubani msaidizi mwenye umri wa miaka 28 alikubali, kulingana na ripoti kutoka kwa wizara ya uchukuzi.

Lakini rubani msaidizi alilala pia bila kukusudia. Kulingana na ripoti hiyo, mkewe alikuwa ametoka tu kujifungua watoto mapacha wa mwezi mmoja na alikuwa akisaidia katika malezi ya watoto.

Taarifa ya:
@bbswahili
FB_IMG_1710150522902.jpg
 
An Airbus 380 is on its way across the Atlantic. It flies consistently at 800 km/h at 30,000 feet, when suddenly an Eurofighter with a Tempo Mach 2 appears.
The pilot of the fighter jet slows down, flies alongside the Airbus, and greets the pilot of the passenger plane by radio: "Airbus, boring flight, isn’t it? Now have a look here!"
He rolls his jet on its back, accelerates, breaks through the sound barrier, rises rapidly to a dizzying height, and then swoops down almost to sea level in a breathtaking dive. He loops back next to the Airbus and asks: "Well, how was that?"
The Airbus pilot answers: "Very impressive, but watch this!"
The jet pilot watches the Airbus, but nothing happens. It continues to fly straight, at the same speed. After 15 minutes, the Airbus pilot radios, "Well, how was that?
Confused, the jet pilot asks, "What did you do?"
The Airbus pilot laughs and says: "I got up, stretched my legs, walked to the back of the aircraft to use the washroom, then got a cup of coffee and a chocolate fudge pastry."
The moral of the story is: When you’re young, speed and adrenaline seem to be great. But as you get older and wiser, you learn that comfort and peace are more important.
This is called S.O.S.: Slower, Older, and Smarter.
Dedicated to all my senior friends ~ it’s time to slow down and enjoy the rest of the trip. [emoji847][emoji173]

Credit goes to the respective owner.

Follow Rise Above Inspire
FB_IMG_1710150575285.jpg
 
This is the wheehouse of the US aircraft carrier Saratoga at Bikini Atoll. The slits are battle covers over the porthole openings. The ship's wheel has rotted away, but everything else was still there in the early 2000s.
FB_IMG_1710170568316.jpg
 
Unampa Alama ngapi dogo kwenye ubunifu?

FB_IMG_1710170522302.jpg
 
Kuna muda unasoma 'comments' unabaki kucheka tu mwenyewe.
Hili tukio la mwaka juzi, ambapo Dash 8 ya Rw@nda ilichochora nje ya barabara na sababu ya awali ilitajwa kuwa njia kulowa maji.
Akaja mtu kwenye 'comment' akasema "Hapana, imepeleka abiria kuchimba dawa"

[emoji991]
Aviation24.be
FB_IMG_1710316041278.jpg
 
Wataliban aka 'Talis' juu ya Blackhawk mnamo 2023..[emoji3]
FB_IMG_1710592134922.jpg
 
𝗙𝗔𝗛𝗔𝗠𝗨 𝗞𝗪𝗔 𝗞𝗜𝗙𝗨𝗣𝗜 𝗞𝗨𝗛𝗨𝗦𝗨 𝗕𝗢𝗘𝗜𝗡𝗚 787 '𝗗𝗥𝗘𝗔𝗠𝗟𝗜𝗡𝗘𝗥'

#Boeing787 maarufu "#Dreamliner" ni jamii ya ndege za umbo pana injini mbili (Twin Wide body) inayoundwa na kiwanda cha #Boeing yenye makao makuu #Seattle nchini #Marekani.

Mradi wa kuunda ndege hii ulianzishwa rasmi mwanzoni mwa mwaka 2000 baada ya kampuni ya 'Boeing' kughairi wazo lake la kuleta ndege ya abiria iendayo kasi inayozidi sauti "Boeing Supersonic Cruiser" (mfano wa #Concord) kwa sababu ya gharama za mradi na mafuta.

Lengo la mradi huu ni kuunda ndege ya teknolojia ya kesho katika ufanisi wa mafuta, mazingira na uendeshaji hivyo awali ikaitwa #Boeing7E7.
Herufi 'E' ikimaanisha Umeme , Ufanisi, Mazingira au Nane (Electric/Efficiency/EnvironmentalFriendly/ #Eight).

Neno "Dreamliner" kwa maana "usafiri wa ndoto" limebatizwa kwa bahati nasibu ya kubuni jina kutoka mtandaoni.

Kwasasa kiwanda kinaunda ndege aina tatu za 'Dreamliner'
(#B787_3 baadae ilisitishwa)
#Boeing787_8 abiria zaidi ya 240,
#Boeing787_9 abiria 280 na
#Boeing787_10 abiria 310.

Mteja wa 'Dreamliner' huchagua injini kati ya #Rollsroyce_Trent_1000 au #General_Electric_GEnx.
Kasi wa juu ya ndege inafikia 944 km/saa.

Mnamo mwaka 2009 #Boeing787 ilifanya majaribio ya kwanza kutoka kiwandani.

Mwaka 2011 mteja wa kwanza shirika la "All Nippon Airways (#ANA) nchini #Japan ilikabidhiwa ndege yake.
October 2011 ANA ilizindua safari ya 'Dreamliner' kutoka #Tokyo kwenda #HongKong.

Kwa shahuku ya upya na sifa za "Dreamliner" abiria waligombea nafasi na ilibidi tiketi ziuzwe kwa njia ya mnada ambapo tiketi moja ilivunja rekodi kwa kununuliwa karibu milioni 70 za kitanzania.

Boeing ametumia miaka na mabilioni ya dola kuunda ndege na kile inachokiita 'visionary design' au "muundo wa maono"

JE, NDEGE HII INA MAAJABU GANI?

1> Dreamliner imetengenezwa kwa malighafi zenye mchanganyiko wa asilimia 50%, polima zilizoimarishwa na nyuzi za kaboni (mfano wa maplastiki) ambazo ni nyepesi lakini ngumu na hudumu kuliko aluminium za jadi.

Mchanganyiko huu umetumika pia katika baadhi ya ndege lakini si kiwango kikubwa kama ilivyo mbawa na kiwiliwili cha Boeing787.
Mchanganyiko wa malighafi umesaidia 'Dreamliner' kuwa nyepesi na kwenda masafa marefu kwa mafuta kidogo.

Mfumo wake wa hewa ndani una unyevu unaokaribia uhasilia kuliko ndege zingine.
Abiria ndani huhisi kama yupo ardhini kimo cha futi 6,000 usawa wa bahari akiwa juu angani ambapo ni uhalisia wa futi 2,000 zaidi ya ndege za kawaida.
Boeing wanasema mfumo huu unapunguza uchovu kwa abiria, macho makavu, maumivu ya kichwa au kukaukiwa koo.
Mfumo wa hewa ya unyevu si rafiki kukaa ndani ya ndege za kawaida kwani huweza kuleta kutu kwenye vyuma na kuchoka mapema.

"Smooth Ride Technology.
Hii ni programu ya kompyuta itumiayo 'sensor' kutupa mbali mawimbi yanayoizonga ndege.
Hesabu ya kompyuta (Algorithm) kupitia 'sensor' zilizofungwa nje ya ndege hukokotoa taarifa ya tabia za ndege au hali ya hewa nje kama upepo na kutuma taarifa katika mfumo wa kurekebisha makosa katika chombo (#flybywire).
Muda mwingi abiria huwa "comfortable" kipindi cha safari pasipo kujua teknolojia hii inazuia ndege kuyumba, kurushwa au kuhama automatiki.

Ndege hii ina nafasi kubwa ndani, taa zenye nuru ya anga, viti vipana, na nafasi zaidi ya mzigo kukaa juu vyote vinakupa utofauti katika ndege hii.

Ufanisi wa mafuta asilimia 20% kuliko ndege zenye ukubwa sawa hivyo mashirika yaendeshayo inasemekana kuokoa pesa na kupeleka ndege masafa marefu zaidi.
Wadau wa usafiri wa anga wanasema masafa marefu huruhusu waendeshaji kubuni njia mpya hivyo abiria kuwa na chaguo zaidi.

Chumba cha rubani angavu, vioo vipana zaidi vya ngamizi yenye kufanya kazi mbalimbali.
Pia teknolojia ya kioo kichwa juu (HUD) hurahisishia kazi marubani kuona data zote za msingi za kupaisha ndege yake pasipo kuinama kila wakati na kupoteza anachokiona nje ya ndege yake.
Teknolojia hii imetumika katika baadhi ya ndege za kisasa za kijeshi.

Dreamliner ina dirisha kubwa za abiria kimo cha inchi 19 hii ni asilimia 30% kubwa kuliko ndege nyengine za ukubwa wake.
Dreamliner ni ndege ya kwanza ya kibiashara kuwa na madirisha yanayofanya kivuli automatiki kuruhusu mwangaza wa jua kupenya kwa wingi utakao.

Dreamliner imepunguza uzito na kuburura kwa kuweka matumizi mengi ya umeme na kuunda umbile rafiki kuelea angani.
Umeme huendesha mambo mbalimbali ya msingi katika ndege zikiwemo mifumo ya breki na vidhibiti vya nje (control surfaces)
Umeme umepunguza matumizi mazito ya haidroliki na bomba nyingi za chuma na plastiki kupitisha vimiminika hivyo.

Umbile la mbawa zake mithili ya mbayuwayu kupinda kuelekea juu zaidi (extended dehydral) huifanya kuwa tulivu angani na kuelea kirahisi pasipo kutumia nguvu kubwa ya injini.

Injini za 'Dreamliner' hufanya kazi katika ukimya wa hali ya juu huku nguvu yake ikiongezwa mara dufu.
Kwa teknolojia mpya ya 'highbypass ratio' ambayo feni husukuma hewa nyingi zaidi nje kuelekea nyuma kuliko hewa inayopita ndani ya kiini cha injini kuchomwa na mafuta.
Hii inaongeza nguvu ya injini, kupunguza kelele na uchafuzi mazingira.

Mikato ya marinda mfano wa msumeno nyuma ya injini inafanya hewa mbili zinazosukumwa nje ya injini kuchanganyika taratibu pasipo kelele za kishindo zinapokutana.

Admin Mkuu,
M.S.Ferej
Aviation Media Tanzania.

Tafsiri kwa hisani ya Boeing

[emoji991] Picha
Kwa kielelezo tu/for reference only
FB_IMG_1710638443012.jpg
FB_IMG_1710638446096.jpg
 
Back
Top Bottom