𝗙𝗔𝗛𝗔𝗠𝗨 𝗞𝗪𝗔 𝗞𝗜𝗙𝗨𝗣𝗜 𝗞𝗨𝗛𝗨𝗦𝗨 𝗕𝗢𝗘𝗜𝗡𝗚 787 '𝗗𝗥𝗘𝗔𝗠𝗟𝗜𝗡𝗘𝗥'
#Boeing787 maarufu "#Dreamliner" ni jamii ya ndege za umbo pana injini mbili (Twin Wide body) inayoundwa na kiwanda cha #Boeing yenye makao makuu #Seattle nchini #Marekani.
Mradi wa kuunda ndege hii ulianzishwa rasmi mwanzoni mwa mwaka 2000 baada ya kampuni ya 'Boeing' kughairi wazo lake la kuleta ndege ya abiria iendayo kasi inayozidi sauti "Boeing Supersonic Cruiser" (mfano wa #Concord) kwa sababu ya gharama za mradi na mafuta.
Lengo la mradi huu ni kuunda ndege ya teknolojia ya kesho katika ufanisi wa mafuta, mazingira na uendeshaji hivyo awali ikaitwa #Boeing7E7.
Herufi 'E' ikimaanisha Umeme , Ufanisi, Mazingira au Nane (Electric/Efficiency/EnvironmentalFriendly/ #Eight).
Neno "Dreamliner" kwa maana "usafiri wa ndoto" limebatizwa kwa bahati nasibu ya kubuni jina kutoka mtandaoni.
Kwasasa kiwanda kinaunda ndege aina tatu za 'Dreamliner'
(#B787_3 baadae ilisitishwa)
#Boeing787_8 abiria zaidi ya 240,
#Boeing787_9 abiria 280 na
#Boeing787_10 abiria 310.
Mteja wa 'Dreamliner' huchagua injini kati ya #Rollsroyce_Trent_1000 au #General_Electric_GEnx.
Kasi wa juu ya ndege inafikia 944 km/saa.
Mnamo mwaka 2009 #Boeing787 ilifanya majaribio ya kwanza kutoka kiwandani.
Mwaka 2011 mteja wa kwanza shirika la "All Nippon Airways (#ANA) nchini #Japan ilikabidhiwa ndege yake.
October 2011 ANA ilizindua safari ya 'Dreamliner' kutoka #Tokyo kwenda #HongKong.
Kwa shahuku ya upya na sifa za "Dreamliner" abiria waligombea nafasi na ilibidi tiketi ziuzwe kwa njia ya mnada ambapo tiketi moja ilivunja rekodi kwa kununuliwa karibu milioni 70 za kitanzania.
Boeing ametumia miaka na mabilioni ya dola kuunda ndege na kile inachokiita 'visionary design' au "muundo wa maono"
JE, NDEGE HII INA MAAJABU GANI?
1> Dreamliner imetengenezwa kwa malighafi zenye mchanganyiko wa asilimia 50%, polima zilizoimarishwa na nyuzi za kaboni (mfano wa maplastiki) ambazo ni nyepesi lakini ngumu na hudumu kuliko aluminium za jadi.
Mchanganyiko huu umetumika pia katika baadhi ya ndege lakini si kiwango kikubwa kama ilivyo mbawa na kiwiliwili cha Boeing787.
Mchanganyiko wa malighafi umesaidia 'Dreamliner' kuwa nyepesi na kwenda masafa marefu kwa mafuta kidogo.
Mfumo wake wa hewa ndani una unyevu unaokaribia uhasilia kuliko ndege zingine.
Abiria ndani huhisi kama yupo ardhini kimo cha futi 6,000 usawa wa bahari akiwa juu angani ambapo ni uhalisia wa futi 2,000 zaidi ya ndege za kawaida.
Boeing wanasema mfumo huu unapunguza uchovu kwa abiria, macho makavu, maumivu ya kichwa au kukaukiwa koo.
Mfumo wa hewa ya unyevu si rafiki kukaa ndani ya ndege za kawaida kwani huweza kuleta kutu kwenye vyuma na kuchoka mapema.
"Smooth Ride Technology.
Hii ni programu ya kompyuta itumiayo 'sensor' kutupa mbali mawimbi yanayoizonga ndege.
Hesabu ya kompyuta (Algorithm) kupitia 'sensor' zilizofungwa nje ya ndege hukokotoa taarifa ya tabia za ndege au hali ya hewa nje kama upepo na kutuma taarifa katika mfumo wa kurekebisha makosa katika chombo (#flybywire).
Muda mwingi abiria huwa "comfortable" kipindi cha safari pasipo kujua teknolojia hii inazuia ndege kuyumba, kurushwa au kuhama automatiki.
Ndege hii ina nafasi kubwa ndani, taa zenye nuru ya anga, viti vipana, na nafasi zaidi ya mzigo kukaa juu vyote vinakupa utofauti katika ndege hii.
Ufanisi wa mafuta asilimia 20% kuliko ndege zenye ukubwa sawa hivyo mashirika yaendeshayo inasemekana kuokoa pesa na kupeleka ndege masafa marefu zaidi.
Wadau wa usafiri wa anga wanasema masafa marefu huruhusu waendeshaji kubuni njia mpya hivyo abiria kuwa na chaguo zaidi.
Chumba cha rubani angavu, vioo vipana zaidi vya ngamizi yenye kufanya kazi mbalimbali.
Pia teknolojia ya kioo kichwa juu (HUD) hurahisishia kazi marubani kuona data zote za msingi za kupaisha ndege yake pasipo kuinama kila wakati na kupoteza anachokiona nje ya ndege yake.
Teknolojia hii imetumika katika baadhi ya ndege za kisasa za kijeshi.
Dreamliner ina dirisha kubwa za abiria kimo cha inchi 19 hii ni asilimia 30% kubwa kuliko ndege nyengine za ukubwa wake.
Dreamliner ni ndege ya kwanza ya kibiashara kuwa na madirisha yanayofanya kivuli automatiki kuruhusu mwangaza wa jua kupenya kwa wingi utakao.
Dreamliner imepunguza uzito na kuburura kwa kuweka matumizi mengi ya umeme na kuunda umbile rafiki kuelea angani.
Umeme huendesha mambo mbalimbali ya msingi katika ndege zikiwemo mifumo ya breki na vidhibiti vya nje (control surfaces)
Umeme umepunguza matumizi mazito ya haidroliki na bomba nyingi za chuma na plastiki kupitisha vimiminika hivyo.
Umbile la mbawa zake mithili ya mbayuwayu kupinda kuelekea juu zaidi (extended dehydral) huifanya kuwa tulivu angani na kuelea kirahisi pasipo kutumia nguvu kubwa ya injini.
Injini za 'Dreamliner' hufanya kazi katika ukimya wa hali ya juu huku nguvu yake ikiongezwa mara dufu.
Kwa teknolojia mpya ya 'highbypass ratio' ambayo feni husukuma hewa nyingi zaidi nje kuelekea nyuma kuliko hewa inayopita ndani ya kiini cha injini kuchomwa na mafuta.
Hii inaongeza nguvu ya injini, kupunguza kelele na uchafuzi mazingira.
Mikato ya marinda mfano wa msumeno nyuma ya injini inafanya hewa mbili zinazosukumwa nje ya injini kuchanganyika taratibu pasipo kelele za kishindo zinapokutana.
Admin Mkuu,
M.S.Ferej
Aviation Media Tanzania.
Tafsiri kwa hisani ya Boeing
[emoji991] Picha
Kwa kielelezo tu/for reference only