Mada maalum ya ndege toka FB

Ndege zina iwezo wa kujirudisha nyuma kama ulivyoelezea, lakini watengeneza ndege hawashauri matumizi ya reverse thrusts kurudishia ndege nyuma kwa sababu ni hatari kwa usalama wa injini hasa hizi kubwa za jet zilizofungwa chini ya mabawa. Ni kawaida sana kwenye turbo props hasa ATRs kuona wakitumia kirudishia ndege nyuma na boeing C17 za kijeshi ambazo injini zake ziko juu kuliko kawaida.

View: https://youtu.be/33pKd8pove0?si=vAk_XNrmhVKV0CrM

View: https://youtu.be/HEz7VjL6oPM?si=NzOxnQOECAsrYy7J
 
Helikopta aina ya Mil Mi-26 (Kulia) ikiwa sambamba na Helikopta ya Bell 206 (kushoto) kwa kulinganisha ukubwa.

Mil-26 ni moja ya Helikopta kubwa kuwahi kutengenezwa Ulimwenguni ambapo ina uwezo wa kubeba mzigo wa hadi tani 20.

Pichani ndogo chini Mi-26 ikiwa imebeba ndege kwa kuning'iniza.

Chanzo:
Mtandaoni
 

Attachments

  • FB_IMG_1701965190983.jpg
    34.6 KB · Views: 8
"..China ni Nchi inayojitahidi sana kukimbizana na Ulimwengu wa Usafiri wa anga, haijalishi anatumia mbinu gani."

Hii ni X'ian, MA700, mradi wa ndege mapangaboi unaoendelea sasa.
Ukiitazama ni kama ndege za Dash-8 na ATR zimezaa Mtoto.

admin
 

Attachments

  • FB_IMG_1702144108283.jpg
    30.3 KB · Views: 8
Ndege ndogo ya mizigo aina ya Cessna Caravan imefanikiwa kwa mara ya kwanza kumaliza safari yake ya kwanza bila kuwa na Rubani katika safari iliyochukua dakika 12 ikiruka kutoka Hollister Airport huko Kaskazini mwa California huku ikiongozwa kwa msaada wa Robot.

Kampuni ya Reliable Robotics iliyotengeneza teknolojia hiyo imesema moja ya changamoto kwenye urushaji huo ilikua ni ndege kupita kwenye anga la chini tofauti na Ndege nyingine lakini hata hivyo itaendelea kufanyia maboresho kwa kiwango kinachotakiwa.

C.E.O wa Kampuni hiyo Robert Rose ameiambia CNN kuwa katika kuirusha Ndege hiyo maelekezo yote yanatumwa kwenye ndege kutoka ardhini ikiwemo yanayoelekeza jinsi ya kutua kwahiyo ndege inajua cha kufanya hata kama mawasiliano kutoka ardhini yatakatika ikiwa bado angani โ€”โ€”โ€” > โ€œndege ipo automatic usipoiambia isifanye kitu haifanyi, ukipoteza mawasiliano itafanya kitu cha mwisho ulichoiambiaโ€

โ€œUkipoteza uelekeo faida ya ndege hii ni tofauti na zile zenye Marubani, maana Rubani ambaye ni Binaadamu akipoteza uelekeo akitoa taarifa kwa walio Airport wanaweza kumpa maelekezo na akafanya tofauti na alivyoelekezwa lakini hii ikipoteza uelekeo robot atafanya kile anachoambiwa afanye na waliochini hivyo ni nzuri zaidi na itaepusha ajali zinazotokana na makosa ya kibinadamuโ€

Kampuni hii sasa inafanya kazi kwa ukaribu na Mamlaka ya anga Nchini Marekani ili kuidhinisha teknolojia hiyo kwa shughuli za kibiashara ikitarajia kuanza kutumika rasmi sokoni ndani ya miaka miwili ijayo. #MillardAyoUPDATES
 

Attachments

  • FB_IMG_1703240703093.jpg
    55.8 KB · Views: 7
Nakala ya ATC iliyotolewa na Wizara ya Ardhi, Miundombinu, Uchukuzi na Utalii ya Japani inaonyesha kuwa ndege ya JL516 ilikuwa imeruhusiwa kutua kwenye barabara ya 34R.

JA722A ilikuwa imeagizwa kushikilia njia ya mchepuko "Taxiway C5".
Maagizo haya yalisomwa kwa usahihi.

Taarifa ya:
twitter.com/aviationbrk/
 

Attachments

  • FB_IMG_1704451786299.jpg
    71.8 KB · Views: 6
.
 

Attachments

  • FB_IMG_1704451793831.jpg
    81.2 KB · Views: 6
.
 

Attachments

  • FB_IMG_1704451783509.jpg
    25.1 KB · Views: 6
TUNAKWAMA WAPI?

Surf Air Mobility (SAM), kampuni ya usafiri wa anga ambayo inabadilisha injini za Cessna Grand Caravans za umeme (Electric Engines) pamoja na Injini Mseto-umeme (Hybrid Powertrain) Alhamisi ilitia saini makubaliano ya kutoa teknolojia yake kwa baadhi ya waendeshaji nchini Kenya.

Kampuni hizo mbili, Safarilink na Yellow Wings, kila moja ilikubali kusimika injini hizo kufuatia uidhinishaji wake wa FAA, inayolengwa kuanza mwaka 2026.

Kampuni zote mbili zinalenga kuwa za injini za umeme mnamo 2027.

Kampuni ya Safarilink inaunganisha safari za ndani Kenya na Tanzania kwa kutumia ndege zao 12, nane kati yao Cessna 208Bs.

Taarifa zaidi:
 

Attachments

  • FB_IMG_1704649915599.jpg
    57.1 KB · Views: 7
๐—ฆ๐—ต๐—ถ๐—ฟ๐—ถ๐—ธ๐—ฎ ๐—น๐—ฎ ๐—ป๐—ฑ๐—ฒ๐—ด๐—ฒ ๐—น๐—ฎ ๐—จ๐—ฟ๐—ฎ๐—น ๐—น๐—ถ๐—บ๐—ฒ๐—บ๐—น๐—ถ๐—ฝ๐—ฎ ๐—บ๐—ธ๐˜‚๐—น๐—ถ๐—บ๐—ฎ ๐˜„๐—ฎ ๐˜€๐—ต๐—ฎ๐—บ๐—ฏ๐—ฎ ๐—น๐—ฎ ๐—ป๐—ด๐—ฎ๐—ป๐—ผ ๐—ธ๐—ผ๐—ฑ๐—ถ ๐˜†๐—ฎ ๐—บ๐˜„๐—ฎ๐—ธ๐—ฎ ๐—บ๐—บ๐—ผ๐—ท๐—ฎ ๐—ถ๐—น๐—ถ๐—ฝ๐—ผ๐˜๐˜‚๐—ฎ ๐—ป๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—ธ๐˜„๐—ฎ๐—บ๐—ฎ ๐—ป๐—ฑ๐—ฒ๐—ด๐—ฒ ๐˜†๐—ฎ๐—ผ ๐—ฎ๐—ถ๐—ป๐—ฎ ๐˜†๐—ฎ ๐˜†๐—ฎ ๐—”๐—ถ๐—ฟ๐—ฏ๐˜‚๐˜€ ๐—”320 ๐˜๐—ฎ๐—ป๐—ด๐˜‚ ๐—ฆ๐—ฒ๐—ฝ๐˜๐—ฒ๐—บ๐—ฏ๐—ฎ 2023.

Mnamo Septemba 12, 2023, rubani wa Ural Airlines alilazimika kutua Airbus A320 kwenye shamba la ngano Urusi baada ya kuwa na wasiwasi kwamba ndege hiyo isingefika Uwanja wa Ndege wa Novosibirsk (OVB) kwa sababu ya ukosefu wa mafuta. .

Kwa taarifa ya kina:
 

Attachments

  • FB_IMG_1704900371679.jpg
    25 KB · Views: 6
umenikumbusha mada kwenye topic tuliosoma kwenye maswala ya uokoaji...aisee umepita mule mule...

kipindi nasoma andiko lako ilikuwa inanijia sauti ya mkufunzi wangu mkaguzi {inspector} wa ZIMAMOTO na Uokoaji yani umeandika kwa sauti yake hakuna ambacho umesahau...umemcopy hadi nukta๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ​
 
. AirTanzania ndege mbili (2) za masafa marefu, Boeing 787-7 (Dreamliner) zilikwenda (kwa mujibu wa ATCL) katika Matengenezo ya kawaida (maintenance schedule) Malaysia tangu September 2023,


Ndege hizo zina usajili wa 5H-TCG (Mt. Kilimanjaro) na 5H-TCJ (Rubondo Island). Tangu wakati huo, ni ndege moja (5H-TCJ) imerudi kutoka katika matengenezo ya kawaida (maintenance schedule).


AirTanzania, kwa kuwa ndege hizi zilinunuliwa kwa fedha zetu, tunahitaji kufahamu, ndege yetu Boeing 787-7 5H-TCG (Mt. Kilimanjaro) ipo wapi tangu September 2023 ilipokwenda nchini Malaysia?


Lakini, tukitazama picha ya ndege ya Boeing 787-7 (Dreamliner) 5H-TCJ (Rubondo Island) ikiwa katika matengenezo Malaysia, inaonekana hadi madirisha yamefunikwa. Mmekwenda kuichapa rangi upya?


Boeing 787-8 Dreamliner bei ni $224.6M sawa na BILIONI MIA TANO na MILIONI MIA SITA na zaidi.. (TZS 562.5 bilioni). Lakini ndege inashinda muda mwingi katika matengenezo kuliko angani.


Kwa mujibu wa taarifa ya CAG kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021, ndege hizi mbili zilihesabu hasara yenye thamani ya TZS 23.6 bilioni wakati ATCL ikipata hasara ya jumla ya TZS 36.5 bilioni.


Gharama za uendeshaji Boeing 787-7 (Dreamliner) zilizidi mapato na kusababisha hasara ya TZS 23.6 bilioni. Bombardier Dash-8 Q300 imekwama kwa zaidi ya miaka mitatu kutokana na matengenezo.


Bombardier Dash-8 Q300 yenye usajili wa 5H-MWF inabeba abiria 50. imetupwa nchini Malta kwa miaka 3 tangu mwaka 2020 ilipokwenda kwa ukarabati ambao unagharimu zaidi ya TZS 13.9 bilioni.


MMM, Martin Maranja Masese
 

Attachments

  • 20240112_050852.jpg
    108 KB · Views: 13
.
 

Attachments

  • 20240112_050847.jpg
    357.5 KB · Views: 11
"๐—ž๐—ฎ๐—บ๐—ฏ๐—ฎ๐—ฟ๐—ฒ ๐—ธ๐—ฎ๐—ฝ๐—ถ๐—ด๐—ถ๐˜‡๐˜„๐—ฎ ๐—ฐ๐—ต๐—ถ๐—ป๐—ถ"

NTSB inatoa ripoti ya mwisho kuhusu ajali iliyohusisha Piaggio P.180 Avanti II, N327A, iliyotokea Mei 27, 2023, katika Uwanja wa Ndege wa Sugar Land (SGR/KSGR),Texas baada ya ndege hiyo kupaa kiasi kisha kurudi chini.

Sababu ya ajali: Kushindwa kwa rubani kukamilisha orodha ya vipengee vya ukaguzi vinavyohitajika kabla ya safari ya ndege na kusanidi ipasavyo mikunjo ya kupaa. (Flaps Setting)

Ripoti: https://data.ntsb.gov/carol-repgen/api/Aviation/ReportMain/GenerateNewestReport/192276/pdf - Hati: NTSB Docket - Docket Management System

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii habari haiko sawasawa na uhalisia. 5H-TCG ndiyo iliyorudi, na ilikaa kule kuanzia October 8 hadi November 22. 5H-TCJ uliyosema imerudi iliharibika August 12 Guanzhou China na ikasafirishwa kwenda matengenezo ya Malaysia November 9. Ipo huko hadi sasa.
 
Asante kwa ufafanuzi na masahihisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
๐—”๐—œ๐—ฅ๐—•๐—จ๐—ฆ ๐—ฌ๐—”๐—”๐—ก๐—š๐—จ๐—ฆ๐—›๐—” ๐—ง๐—”๐—œ๐—ฅ๐—œ ๐—ž๐—จ๐—ง๐—ข๐—ž๐—” ๐—”๐—ก๐—š๐—”๐—ก๐—œ

Ndege ya LATAM Brasil aina ya Airbus A319-100, yenye usajili PT-TMO ikifanya safari ya ndege LA-3923 kutoka Rio de Janeiro Santos Dumont kwenda Sao Paulo Congonhas,SP (Brazil), ilikuwa ikishuka kuelekea Sao Paulo ambapo marubani waliamua kuchepuka kwenda kutua Sao Paulo Guarulhos baada ya kupata tatizo gurudumu za kutua mnamo Februari 7, 2024.

Ndege hiyo ilipita chini chini 'runway' ya Guarulhos namba 10L, ili waongoza ndege mnarani waweze kubaini tatizo, ambapo waligundua kukosekana kwa gurudumu moja kuu la kushoto la ndani.

Ndege hiyo baadae ilitua njia ya kuruka namba 10L bila tatizo lolote.

Taarifa ya:


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ