FAHAMU AINA YA INJINI ZA NDEGE
(ufafanuzi rahisi)
Ndege inaweza kuwa na injini 1 hadi 8 na katika hizo ni injini za aina mbili ndiyo maarufu:
(1)-Injini za #Jet (Zenye mfano wa pipa lililolazwa)
(2)-Injini za #Piston (Nyingi pangaboi)
1> INJINI ZA JET
Hizi zimegawanyika kutokana na 'modification' za ufanisi na matumizi yake:
a)Turbojet/PureJet'
Mfumo wa ndege nyingi za awali miaka ya 70 kushuka chini pia ndege za kivita.
b)Turbofan
Hizi ni injini za mfumo wa ndege nyingi za sasa ambazo zinakuwa na kipenyo kikubwa cha feni
c)Turboshaft
Mfumo wa baadhi ya ndege za sasa hasa Helicopter n.k
d)Turbo Propeller au 'Turbo Prop'
Mfumo wa ndege za kisasa za masafa mafupi zenye mapangaboi yanayoendeshwa na mfumo wa 'gas turbine' badala piston.
Ramjet/Scramjet
Mfumo ulio katika ndege za majaribio za mwendokasi mara nyingi ufanya kazi kuanzia mara tatu hadi tano ya kasi ya sauti 'Hypersonic' mfano mfano makombora na ndege za majaribio.
Injini za mfumo wa jet zinafanya kazi kwa mfano wa sheria ya Tatu ya #Newton (#action & reaction):
1-Kunyonya hewa mbele (Sucking)
2-Kukandamiza (compression)
3-Kulipua hewa iliyokandamizwa kwa kuchanganya na mafuta (Ignition)
4-Kutoka nyuma kwa kasi na kuisukuma ndege mbele (Thrust)
Kwa kifupi wanasema #Suck_Squeeze_Bang_Blow yaani Nyonya-kandamiza-Lipua-Puliza nje (nyuma)
Mfano wa Puto lililopulizwa na kuachiwa hewani pasipo kuzibwa mdomo litasukumwa kwakuwa hewa itatoka mdomoni kwenda kinyume na uelekeo wa puto.
Ndege nyingi kubwa za kisasa zinatumia injini aina ya 'Turbofan' (#gas_driven) ambazo zinasemakana kuwa na nguvu kubwa na ulaji mdogo wa mafuta.
Unaweza kutambua injini hizi kwa haraka kuangalia feni kubwa lililo mbele ya injini (Sio mapangaboi)
i> #Turbojet (Purejet)
Hizi zina vifeni vidogo vya compressor mbele ambavyo hufanya kazi ile ile ya kunyonya hewa kuingiza ndani (#air_inlet)>Hewa kukandamizwa na vifeni (#compressor_blades)>Hewa kulipuliwa katika (#combustion_chamber)>Hewa iliyolipuliwa kutoka kwa kasi nyuma (thrust) kwenye #exaust_nozzle.
Hii ndiyo nguvu pekee inayosukuma ndege kwenda mbele.
Injini hii hutumia mafuta mengi kuliko injini ya 'Turbofan' na nyingi zinatumika zaidi kwenye ndege za kivita na ndege za zamani.
Ni injini nyembamba/kipenyo kidogo zaidi kuliko turbofan.
Injini hizi zinakula mafuta mengi na kuzalisha nguvu ndogo kwa kuwa ni teknolojia ya zamani.
ii> #Turbofan
Hii ni injini itumikayo katika ndege nyingi hasa kubwa za kisasa.
Uboreshaji na ukubwa wake zinaondoa katika uhalisia wa kuitwa injini za jet halisi.
Hizi pia zinavuta na kusukuma hewa kama injini ya 'turbojet' isipokuwa zinavuta hewa mbili.
Hewa ya kwanza ni ile inayoingia kwenye mfumo wa ndani ya injini (#inner_core) kama ifanyavyo injini ya 'Turbojet' na ya pili inavutwa na feni lake kubwa mbele kupita nje ya mfumo wa ndani na kupuliza moja kwa moja nyuma ya injini.
Nguvu ya feni hilo mbele kuzunguka inatokana na kuzunguka visahani nyuma ya injini(turbine) ambavyo vimeungwa na #shaft' hadi katika feni hilo.
Hewa ipitayo nje ya mfumo wa injini (#Bypass_air) na hewa ya ipitayo ndani ya injini zote husukuma ndege kwa wakati mmoja ingawa hewa ipitayo nje ndiyo nyingi yenye nguvu zaidi.
iii- #Turbo_Prop au #TurboPropeller
Hizi zina mfumo wa injini kama turbofan hapo juu lakini mbele inakuwa na mapanga badala ya feni.
Visaani vya Turbine vinapozunguka vinazungusha shaft ambayo huzungusha mapanga mbele ya injini.
Mfano wa ndege hizi ni Bombardier Dash-8, ATR, Cesna208 n.k
iv- #Turbo_Shaft
Injini za Turboshaft' hufanya kazi kama Turbo Prop isipokuwa shaft inaunganishwa na mapanga makubwa marefu.
Hii shaft inaweza kuwa imeunganishwa na mfumo wa Gear au ikawa Free Turbine.
Injini hizi nyingi zinatumika kwenye #Helicopter za kisasa ili kuipa nguvu zaidi ya Helicopter zinazotumia injini za Piston.
#Scramjet/Ramjet.
Hizi ni injini za majaribio kwa roketi au ndege inayoenda kasi Mara tano ya kasi ya sauti (5500km/h).
Zina uwezo wa kuanza kufanya kazi katika mwendo huo kwasababu haina utumbo unaozunguka ndani kufua upepo bali kasi kubwa ya hewa inayoingia mbele haihitaji tena kuvutwa na kukandamizwa bali hulipuliwa moja kwa moja na kusukuma chombo.
2-MFUMO WA INJINI ZA PISTON
Injini hizi zina mfumo wa Piston kama ilivyo kwenye injini za gari isipokuwa crankshaft yake imeungwa na Mapanga mbele (Propeller Blades)
Mapanga yanafanya kazi ya kuchota upepo mbele na kupuliza nyuma ambapo husababisha ndege kwenda mbele.
Ndege nyingi zenye injini za piston ni ndogo na zile za zamani ambazo nyingi hutumia mafuta ya AvGas.
Tukumbuke pia injini za ndege hazina mahusiano wala kiunganishi chochote na tairi za ndege.
Injini za mfumo wa jet hutumia sana mafuta ya #JetA (Mafuta ya taa yaliyoboreshwa) wakati Piston hutumia #AvGas (kama petrol iliyoimarishwa)
Kumbuka pia Tairi za ndege ni 'freewheel' na zimeunganishwa na mifumo ya 'brake' na kona tu.
Hakuna kitu kinachozungusha tairi kutoka kwenye injini bali zinafuata uelekeo wa kule ndege inaposukumwa.
#Admin
Aviation Media Tanzania