Mada maalum ya ndege toka FB

KWANINI NDEGE ZA ABIRIA HAZINA VITI VYA KUCHOMOKA NJE WAKATI WA DHARURA?
(Ejection Seat)

Kama ukitoa gharama kwa kiti kimoja chenye makadirio kati ya milion 350 hadi 900 za kitanzania, usimikaji wake pia ni mgumu zaidi.

Viti vya kufyatuka nje 'Ejection Seat' husimikwa kwenye baadhi ya vyombo vya anga za mbali na ndege za kivita ili kujaribu kuokoa maisha ya rubani pindi inapotokea dharura ya kushindwa kuokoa ndege au kudunguliwa.

Viti hivi hujumuisha parachuti, vitungi vya oksijeni, mavazi ya joto, mfumo wa vilipuzi vya kupaisha kiti ambapo uzito hufikia kilogramu 80 hadi 150.
Viti hivi maarufu kama "Martin Baker' huchomoka kwa kasi kubwa kwa kutumia vipulizi vya Gas na baadae kuchomoa mwamvuli angani.

Kujaribu kusimika viti hivi ndani ya ndege za abiria kiujumla vitaongeza uzito wa ndege, kuchukua nafasi, kupunguza idadi ya abiria hivyo kupunguza uchumi wa mafuta na faida ya ndege kifupi 'impractical'
(Usingependa kukata tiketi ya safari moja Dar-Mwanza kwa milioni 5).

*Italazimu abiria kupata mafunzo na muda kuelekezwa kikamilifu jinsi ya kutumia viti hivyo (operational training) ingawa bado asilimia kubwa watajeruhiwa au kupoteza maisha kwenye mchakato wa kujichomoa wakati wa tukio.

Juu ya kiti cha ndege abiria kuna stoo za kuhifadhi mizigo (Overhead storage), nyaya za umeme n.k vyote vitahitajika kuondolewa.
Hata hivyo paa ya ndege haiwezi kufunguka kwa urahisi bila kuathiri mfumo wa hewa na udhibiti wa ndege.

Abiria watahitajika kuvaa vifaa vya oksijeni na mavazi yenye uwezo wa kuhimili baridi kali la nje kukidhi mahitaji ya watu kwa maumbile na rika zote.

Muda wote utahitajika kujifunga mikanda kadhaa kwenye kiti chako kitu ambacho hutofurahia safari.

Kumbuka kama abiria mwenye hofu, ndege ikiyumba kidogo anaweza kufyatua kiti chake hivyo italazimu watu wote kufyatua kwakuwa ndege itakuwa si salama tena.

Kiti huwa kinachomoka kwa kasi kubwa sana hivyo kuhimili uvutano wa ardhi utaokuelemea "G-Force" ifikayo hadi 20Gs ni ngumu pasipo mafunzo maalum.

20Gs ni sawa na mwili kuwa na uzito mara 20 ya uzito wako.
Kitendo hiko damu hukimbilia miguuni, viungo ndani ya mwili wako mfano moyo, figo, mapafu uhisi kuvutwa kuelekea miguuni.
Baadhi ya marubani huzimia (black out) kwasababu ya ubongo kukosa hewa inayosambazwa na damu.

Haya yote yanahitaji ndege mpya iliyofanyiwa tafiti na uwekezaji wa muda mrefu kitu ambacho gharama zake za manunuzi ya ndege husika hakuna shirika/kampuni iliyo tayari kumiliki ndege na kuuza tiketi bei inayozidi #Concord kwa mwendo wa kawaida.

Ndege yeyote hupata faida kupakia abiria wengi na mizigo, ndiyo maana ndege nyingi za kisasa zinaundwa kwa malighafi nyepesi za "plastic composites" badala ya vyuma, umeme badala ya "hydraulics na cable" n.k ili kupunguza uzito.

Yote tisa, kumi hakuna uhakika wa kutua ukiwa hai baada ya kujichomoa.
Kumbuka hata baadhi ya marubani wa ndege za kivita hupata majeraha au kupoteza maisha hata baada ya kujichomoa.

Mawazo hayo ni mfano wa kuruka kwenye gari lililo pasua tairi katika mwendo mkali.

Hili si wazo zuri kiusalama, kibiashara, wala kiuchumi, pamoja na lile la kuweka 'parachute' ndege nzima au abiria mmoja mmoja kama tulivyoeleza post iliyopita.
#Link
( https://www.facebook.com/)

*Ndege ni salama zaidi kama ilivyo, baadhi ya ajali zitokeazo sasa nyingi ni makosa ya kibinaadamu zaidi (uzembe) kuliko ya kiufundi.

Hitilafu hata ya ndege hata kuzima injini zote bado ina uwezo wa kutua salama ukilinganisha na ndege ya kivita ambayo ni ngumu kudhibiti baada kuzima injini kwasababu ya umbile la mbawa ndogo.

Kama unahitaji ku'share makala kwenye 'group' taja 'reference'.

#Admin

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania kukabidhiwa ndege yake ya kwanza kabisa ya mizigo wiki hii.
Ndege hiyo aina ya Boeing 767-300F ilikuwa miongoni mwa oda za ndege nne za Boeing zilizonunuliwa na Tanzania katika maonyesho ya ndege ya Dubai 2021.

Ndege nyingine zilizopangwa kukabidhiwa baadaye mwaka huu ni pamoja na 787-8 Dreamliner na Boeing mbili aina ya #B737MAX.

[emoji3575] Ndege hizo nne zina thamani ya zaidi ya $726 milioni kwa bei zilizoorodheshwa

Unaweza kuingia kwenye kurasa yetu ya Instagram kutzama video ya ndege husika.

Chanzo:

[emoji991]
Airliners.net

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KWANINI NDEGE HUSUKUMWA KURUDI NYUMA?

#Asilimia nyingi ya ndege zina mfumo wa 'reverse' ambao mara nyingi hutumika kupunguza kasi wakati wa kutua (#Braking)
Kwa Ndege za Mapangaboi (#Propeller) hutumia panga zake kubadili '#Angle au #Shape' hivyo badala ya kusukuma hewa kwenda nyuma inasukuma kuelekea mbele na kusababisha ndege kupunguza kasi yake pale inapotua.

Hali kadhalika na kwenye injini zenye mfumo wa #Jet hufungua injini zake katikati na kuielekeza hewa inayopulizwa nyuma na injini kuelekezewa kwenda mbele.

#Injini za mfumo wa 'jet nyengine zinafungua vimilango vyake vidogo katikati au nyuma ya injini na kufanya hewa inayosukumwa nyuma kuvuja na kubadilishwa uelekeo kwenda mbele hivyo kupunguza kasi ya ndege.

Ndege nyingi kubwa zina mifumo mitatu ya 'Brake' ikiwemo
1>#Reversers' za Injini (#ReverseThrust)
2>#Tairi na
3>#Spoilers au #Speedbrake' zilizopo juu ya mbawa.

Hivi vyote mara nyingi hufanya kazi kwa pamoja ili kupunguza kasi ya ndege inapotua ili kusimama haraka.

#Hii yote husaidia kutozipa mzigo mkubwa 'brake' za tairi za ndege ambazo huweza kupasua tairi, kuharibika, kuwaka moto au mda mwingine kuteleza endapo barabara (#Runway) imetuama maji.

KWANINI #REVERSE" HAITUMIKI KURUDISHA NDEGE NYUMA KUTOKA KWENYE MAEGESHO
BADALA YAKE HUSUKUMWA NYUMA (#Pushback) NA VIGARI MAALUMU? (#Tug)

1>Kuepuka kelele kali za injini
2>Kuepuka ulaji mafuta
3>Kuepuka hatari ya kugongana na vitu vingine maana Rubani si rahisi kuona nyuma.
4>Kuepuka uharibifu wa injini kwa kunyonya taka na vumbi sababu upepo wa 'reverse hutokea pembeni ya injini kwa kasi #pressure kubwa kuelekea mbele.

(Picha kwa hisani ya mtandao)

#LIKE & #SHARE"*

#Admin Admin

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPO TAYARI KUKATA TIKETI YA MWAKA 2028;?

Tarehe 2 Juni saa 12:00 CET, SAS - Scandinavian Airlines itafungua nafasi za viti kupitia www.flysas.com/electric kwa safari zake za kwanza za kibiashara za ndege za umeme nchini Sweden, Norway, na Denmark.
Shirika la ndege SAS litaweka nafasi ya viti 30 kwa kila moja ya safari 3 za uzinduzi zinazotarajiwa kufanyika mnamo 2028.

Bei ya tiketi ya safari ya kwanza ya ndege itakuwa SEK / NOK / DKK 1946 (Hii hata admin sijaelewa) kama heshima kwa mwaka ambao shirika hilo la ndege SAS ilianza kuruka kwa mara ya kwanza.

#SAS inashirikiana na #Heart_Aerospace kuendeleza ndege za umeme.
Mnamo Septemba 2022, SAS ilitia saini barua ya kutoa msaada kuhusu ndege mpya ya umeme ES-30 kuja kuwa sehemu ya ndege zake za kikanda.

Chanzo:
@aeronews

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TAARIFA YA TCAA KUHUSU TUHUMA ZA NDEGE MPYA KUFANYA SHUGHULI HARAMU.

INASOMEKA...

"Mamlaka imepokea kwa mstuko taarifa za uongo kutoka kwa tovuti ya MYFLYRIGHT zinazosambaa katika mitandao ya kijamii, kwamba tasnia ya usafiri wa anga nchini Tanzania imegubikwa na utata, ikieleza kuwa ndege ya mizigo ya Air Tanzania aina ya Boeing 767-300F imetuhumiwa kwa shughuli haramu na kwamba ilipatikana na zaidi ya tani 30 za mizigo ambayo haijatangazwa na Mamlaka ya Forodha.

Huu ni uwongo mtupu unaojaribu kupotosha na kuharibu sifa nzuri ya sekta ya Usafiri wa Anga nchini Tanzania.

Umma unafahamishwa kuwa ndege mpya ya Air Tanzania Boeing 767-300F mizigo bado haijawasilishwa katika nchi yetu, kwa hivyo haifanyi kazi katika Umoja wa umma wa Tanzania. Tumeshtushwa kabisa na taarifa za uongo za makusudi kutoka kwa MYFLYRIGHT.

Mamlaka inachunguza kwa umakini suala hili na haitasita kuchukua hatua zinazofaa za kisheria dhidi ya yeyote atakayebainika kuhusika"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
DKK ni Danish Krone
NOK ni Norwegian Krones
SRK ni Swedish Krona

Hizo ni ela zao kwa mjibu za Google
 
"MKANGANYIKO"

Kumekuwa na hoja za mvutano kutoka katika mitandao kadhaa ya kijamii kuhusu ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 767-300F (Air Tanzania Cargo) kuwa ya kwanza barani Afrika, kumilikiwa au kuendeshwa nchini Tanzania.

Kifupi kuhusu ndege ya mizigo aina ya Boeing 767, Tanzania sio nchi ya kwanza kumiliki au kuendesha ndege husika.
Tunaona Shirika la ndege Ethiopian Airlines tayari linaendesha Boeing767 ya mizigo kutokea mnamo mwaka 2022.

Ifahamike vizuri kuwa, ndege ya mizigo aina ya Boeing767-300F ( Air Tanzania Cargo) ndiyo ndege ya kwanza mpya barani Afrika iliyoundwa maalumu kubeba shehena/mizigo kutoka kiwandani.

Kuhusu ndege ya mizigo aina ya Boeing767-300ER (BDSF) inayoendeshwa na shirika la ndege Ethiopian Airlines, hii ni ndege iliyobadilishwa matumizi kutoka kubeba abiria na kuwa ndege ya mizigo (Si halisi/mpya kutoka kiwandani)

Ubadilishaji huu wa ndege kutoka kubeba abiria na kuwa ndege ya mizigo kwa upande wa shirika la Ethiopian, haujafanywa na kiwanda cha Boeing, bali umefanywa na kampuni ya usafiri wa anga ya Israel iitwayo BEDEK Aviation Group.

Unaweza kugundua ndege hiyo ya mizigo aina ya Boeing 767 kutoka Ethiopia inaishia na -300ER(BDSF) au -300BDSF kwa maana ya "BEDEK SPECIAL FREIGHTER" tofauti na ndege ya Tanzania Boeing 767-300F (FREIGHTER) ambayo ni toleo halisi la kubeba shehena kutoka kiwandani.

#Admin

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Dada" anasukuma chuma kama Ferrari.
Futi 39,000,
Kasi 981km/saa (within speed limits)
Huu mwendo ni 'Supersonic' kasoro kiduchu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…