KWANINI NDEGE ZA ABIRIA HAZINA VITI VYA KUCHOMOKA NJE WAKATI WA DHARURA?
(Ejection Seat)
Kama ukitoa gharama kwa kiti kimoja chenye makadirio kati ya milion 350 hadi 900 za kitanzania, usimikaji wake pia ni mgumu zaidi.
Viti vya kufyatuka nje 'Ejection Seat' husimikwa kwenye baadhi ya vyombo vya anga za mbali na ndege za kivita ili kujaribu kuokoa maisha ya rubani pindi inapotokea dharura ya kushindwa kuokoa ndege au kudunguliwa.
Viti hivi hujumuisha parachuti, vitungi vya oksijeni, mavazi ya joto, mfumo wa vilipuzi vya kupaisha kiti ambapo uzito hufikia kilogramu 80 hadi 150.
Viti hivi maarufu kama "Martin Baker' huchomoka kwa kasi kubwa kwa kutumia vipulizi vya Gas na baadae kuchomoa mwamvuli angani.
Kujaribu kusimika viti hivi ndani ya ndege za abiria kiujumla vitaongeza uzito wa ndege, kuchukua nafasi, kupunguza idadi ya abiria hivyo kupunguza uchumi wa mafuta na faida ya ndege kifupi 'impractical'
(Usingependa kukata tiketi ya safari moja Dar-Mwanza kwa milioni 5).
*Italazimu abiria kupata mafunzo na muda kuelekezwa kikamilifu jinsi ya kutumia viti hivyo (operational training) ingawa bado asilimia kubwa watajeruhiwa au kupoteza maisha kwenye mchakato wa kujichomoa wakati wa tukio.
Juu ya kiti cha ndege abiria kuna stoo za kuhifadhi mizigo (Overhead storage), nyaya za umeme n.k vyote vitahitajika kuondolewa.
Hata hivyo paa ya ndege haiwezi kufunguka kwa urahisi bila kuathiri mfumo wa hewa na udhibiti wa ndege.
Abiria watahitajika kuvaa vifaa vya oksijeni na mavazi yenye uwezo wa kuhimili baridi kali la nje kukidhi mahitaji ya watu kwa maumbile na rika zote.
Muda wote utahitajika kujifunga mikanda kadhaa kwenye kiti chako kitu ambacho hutofurahia safari.
Kumbuka kama abiria mwenye hofu, ndege ikiyumba kidogo anaweza kufyatua kiti chake hivyo italazimu watu wote kufyatua kwakuwa ndege itakuwa si salama tena.
Kiti huwa kinachomoka kwa kasi kubwa sana hivyo kuhimili uvutano wa ardhi utaokuelemea "G-Force" ifikayo hadi 20Gs ni ngumu pasipo mafunzo maalum.
20Gs ni sawa na mwili kuwa na uzito mara 20 ya uzito wako.
Kitendo hiko damu hukimbilia miguuni, viungo ndani ya mwili wako mfano moyo, figo, mapafu uhisi kuvutwa kuelekea miguuni.
Baadhi ya marubani huzimia (black out) kwasababu ya ubongo kukosa hewa inayosambazwa na damu.
Haya yote yanahitaji ndege mpya iliyofanyiwa tafiti na uwekezaji wa muda mrefu kitu ambacho gharama zake za manunuzi ya ndege husika hakuna shirika/kampuni iliyo tayari kumiliki ndege na kuuza tiketi bei inayozidi #Concord kwa mwendo wa kawaida.
Ndege yeyote hupata faida kupakia abiria wengi na mizigo, ndiyo maana ndege nyingi za kisasa zinaundwa kwa malighafi nyepesi za "plastic composites" badala ya vyuma, umeme badala ya "hydraulics na cable" n.k ili kupunguza uzito.
Yote tisa, kumi hakuna uhakika wa kutua ukiwa hai baada ya kujichomoa.
Kumbuka hata baadhi ya marubani wa ndege za kivita hupata majeraha au kupoteza maisha hata baada ya kujichomoa.
Mawazo hayo ni mfano wa kuruka kwenye gari lililo pasua tairi katika mwendo mkali.
Hili si wazo zuri kiusalama, kibiashara, wala kiuchumi, pamoja na lile la kuweka 'parachute' ndege nzima au abiria mmoja mmoja kama tulivyoeleza post iliyopita.
#Link
(
)
*Ndege ni salama zaidi kama ilivyo, baadhi ya ajali zitokeazo sasa nyingi ni makosa ya kibinaadamu zaidi (uzembe) kuliko ya kiufundi.
Hitilafu hata ya ndege hata kuzima injini zote bado ina uwezo wa kutua salama ukilinganisha na ndege ya kivita ambayo ni ngumu kudhibiti baada kuzima injini kwasababu ya umbile la mbawa ndogo.
Kama unahitaji ku'share makala kwenye 'group' taja 'reference'.
#Admin
Sent using
Jamii Forums mobile app