Mada maalum ya ndege toka FB

Mada maalum ya ndege toka FB

Nathalia Gadelha, mwenye umri wa miaka 20, ametambuliwa na familia yake kuwa alikuwa msaidizi wa rubani (Co-pilot) aliyefariki katika ajali ya ndege aina ya Learjet 60 iliyotokea Greenacres, Florida, Marekani, Novemba 01, 2026.

Gadelha alianza safari yake ya urubani akiwa na umri mdogo, ambapo alipata leseni ya urubani binafsi (Private Pilot License) Oktoba 2023 akiwa na miaka 17, hata kabla hata ya kupata leseni ya udereva wa magari.

Alipata mafunzo kupitia programu ya Aviation Academy ya shule za Palm Beach County na baadaye kuendelea na mafunzo katika chuo cha urubani cha American Flyers. Ndoto yake ilikuwa kuwa rubani wa ndege za abiria katika shirika kubwa la ndege.

Gadelha alikuwa miongoni mwa watu tisa (09) waliokuwamo ndani ya Learjet 60 iliyopata ajali hiyo, ambapo watu wote walipoteza maisha.

Bodi ya Kitaifa ya Usalama wa Usafiri wa Marekani (NTSB) imeanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo, ikichunguza mabaki ya ndege, hali ya hewa na taarifa za rada.

Chanzo:
New York Post.
1793669637763.jpg
 
Back
Top Bottom