JINSI HELIKOPTA INAVYOPAA
(Ufafanuzi mwepesi)
#Helicopter ni ndege inayotumia mbawa zinayozunguka juu (panga) kutengeneza '#lift' ili iweze kunyanyuka kupaa.
Kumbuka ndege ya kawaida inategemea kusukumwa na injini kwenda mbele ili mbawa zake zipitiwe na hewa ya kutosha kuweza kutengeneza mkandamizo wa hewa chini ya mbawa utakaosababisha kunyanyuka 'lift' na kupaa.
Kwa Helikopta hali ni tofauti kidogo, kwani panga ndiyo zinakimbia/kuzunguka (rotation) ili kuzalisha 'lift' kwa kusukuma hewa chini.
Lakini pia ina panga ndogo nyuma {mkiani} ili kuzuia bodi {#fuselage} kuzunguka pamoja na panga kubwa inapozunguka (torque effect)
'Helicopter' kiasili ni ndege isiyotaka kupaa kwasababu vidhibiti vyake (contros) lazima vifanye kazi kwa kupingana ili iweze kwenda sawa.
Hiyo ndiyo sababu 'Helicopter' inahitaji hesabu kubwa zaidi kupaisha.
Hii ndiyo sababu hata baadhi ya Helikopta zinazotoka na mfumo wa kujiendesha yenyewe {autopilot} ni gharama kiasi.
Rubani wa Helikopta muda wote hufanya kazi ya kuipa milinganyo tofauti {balance} kati ya panga kubwa na ndogo itakayomwezesha kupaa alivyokusudia.
UPAAJI
{Endapo kila kitu shwari}
Rubani huwasha mzunguko wa injini #rpm hadi ifike kiwango kinachohitajika kwa kutumia '#throttle' {inafanana na mkono wa #acceleretor ya pikipiki}
Baada ya hapo huvuta juu taratibu '#collective' {inafanana na #handbrake ya mkono ya gari za zamani}
Kazi ya 'collective' ni kubadili 'angle' ya mapanga ya juu {rotor blades angle} ili iwe na umbile linaloweza kukandamiza hewa chini na kupaa {mfano wa panga za feni zilivyokunjwa ili kuweza kusukuma upepo}.
Wakati wa kunyanyuka ina tabia ya kiwiliwili kutaka kuzunga na panga kubwa {#torque effect} hivyo rubani huzuia hali hiyo kwa kukanyaga pedeli ya kulia au kushoto kuiweka sawa, kutegemea bodi inazunguka upande gani.
Pedeli hizi zina'control panga ndogo mkiani kama ilivyo kwenye ndege ya kawaida pedeli zinavyo'control' kielekezi (#rudder) mkiani ili kukata kona.
Ikifika kimo anachohitaji kwenda juu hutumia "#cyclic" ambayo ni 'control stick' iliyopo katikati ya miguu ya rubani na kazi yake kuinamisha panga kubwa iwe kulia, kushoto, mbele au nyuma ili helikopta ielekee upande ambao panga litainamia.
Kama ni kwenda mbele atasukuma mbele taratibu "cyclic" ambayo itasababisha mzunguko wa panga la juu {#main_rotor_disk} kuinama kidogo mbele na kusababisha helikopta kufuata kuelekea huo.
Hii ni kwasababu panga kubwa litaanza kukandamiza hewa kwenda chini na nyuma na kusababisha helikopta kunyanyuka juu na kwenda mbele (lift & Thrust)
Rubani pia anaweza kuongeza nguvu ya injini kidogo kwenye 'throttle' yake au kuvuta "collective" ili kuongeza kasi ya panga kuzalisha nguvu hizo mbili kutegemea na haraka au uzito wa Helkopta wakati huo akikanyaga kiumakini pedeli kusahihisha uelekeo.
Zipo 'Helikopta ambazo hazina panga ndogo nyuma, ila panga mbili kubwa zilizo katika nguzo moja (rotor must) ambazo zinazunguka kinyume ili kuondoa tatizo la kiwiliwili kuzunguka na panga wanaita 'Coaxial rotor' au 'Counter rotating Blades' mfano Kamov #Ka52.
Pia kuna Helkopta nyengine yenye panga zote kubwa mbele na nyuma zinazozunguka kinyume mfano #Chinook CH-47 ili kuondoa hali ya 'torque'effect.
Helkopta ni mashine ya kufanya kazi nyingi ambazo ndege ya kawaida haiwezi kufanya.
Na hii kutokana na uwezo wa wa kuganda sehemu moja hewani (hovering), kugeuka papo kwa papo, kwenda ubavu au kurudi kinyume na kutua sehemu ambazo ndege ya kawaida haiwezi.
Kutokana na ugumu wa kupaisha Helikopta wanaanga wanatumia usemi ufuatao;
"kupaisha ndege ya kawaida ni kama kuendesha baiskeli ya tairi mbili, lakini kupaisha Helkopta ni kama kuendesha baiskeli ya tairi moja.
#Like & #share!
#Admins
View attachment 2622812